NASAHA
Na. 082 Jumatano Januari 10 - 16, 2001
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
MAONI YETU 
 

Mapinduzi Zanzibar yameleta kilichokusudiwa?

Historia ya ulimwengu inaonesha kuwa nchi nyingi ziliwahi kutawaliwa na nchi au mataifa mengine. Hata hivyo, karibu kila nchi iliyotawaliwa ilianzisha mapambano, awamu kwa awamu, ili kujikomboa kuweza kukomesha dhuluma zilizokuwa zikifanywa na taifa tawala.

Wazanzibar, kama ilivyokuwa kwa wananchi katika nchi nyingine kadhaa, hususan zile za dunia ya tatu, walipigania uhuru wa nchi yao. Hatimaye uhuru huo ukapatikana Desemba, 1963.

Hata hivyo, Zanzibar, pamoja na uhuru huo, ilibaki chini ya Sultan. Ingawa Sultan hakuwa miongoni mwa watu wa mataifa yakiyokutana Berlin, Ujerumani, mwaka 1884 katika mktano wa kuigawa Afrika, Wazanzibari hawakuridhia hali hiyo. Waliona kuwepo kwa Sultan kama mkuu wa nchi yao ilikuwa ni 'kiwimngu' cha aina fulani juu ya uhuru wao huo walioupata mwaka 1963.

Wazanzibari wakaazimia kukiondosha kiwingu hicho na kwa hilo hawakufanya ajizi, kwani: Januarai 12, 1964, walifanya mapinduzi ya kumwondoa Sulatan.

Walitamni na waliamua kuwa huru, kuwa na uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe bila kuingiliwa na yeyote asiye mzazibari au asiyetetea maslahi ya wazanzibari. 

Walitamani, waliamua na walipanga kuindesha nchi yao katika namna wanayoona inawafaa wao ili mradi hawaingili uhuru wa nchi nyingine kama jinsi wao walivyopenda wasiingiliwe.

Hiyo ndio hali iliyopelekea kuondolewa kwa Sultan aliyeingia madarakani kuitawala Zanzibar baada ya ukoloni wa Mwingereza kukoa Visiwani humo.

Jambo la kujiuliza wakati huu ambapoWazanibar wanajiandaa kuadhimisha miaka 37 ya mapinduzi hayo yaliyokusudia kuipa Zanzibar uhuru wa kweli, je kile 'kiwingu' juu ya uhuru wao kimeondoka au kimezidi kufunga na hivyo kuweka kiza kinene zaidi? Je, Wazanzibar wapo huru ki-kweli kweli?

Hatudhani kama ni hivyo kwa sababu historia imekwisha tuonesha juhudi za Wazanzibari kutaka kujihakikishia uhuru wao pasipo kuwepo 'kiwingu' hazijafanikiwa.

Bila shaka imo katika kumbukumbu za Wazanzibari wengi kwamba wananchi wa Zanzibar walipoonesha hofu ya nchi yao kutaka kumezwa kwa visingizio vya 'Siasa za Chama' na Azimio la Arusha, aliyeuwa Rais wa Zanzibar kwa wakati huo, Marehemu Abeid Karume, aliwahakikishia Wazanzibar kwamba wasiwe na wasiwasi kwani Azimio la Arusha lingeishia Chumbe, kisiwa kilicho baina ya Tanzania Bara (wakati huo Tanganyika) na Zanzibar. Hivyo Zanzibar isingemezwa kwa kisingizio cha muungano!

Lakini leo hii tunapoitazama hali ya mambo visiwani humo, je ni kweli mambo ya kuingilia uhuru w Wazanzibari yameishia Chumbe kama alivyoahidi Marehemu Karume? HAPANA. Historia haioneshai hivyo.

Rais aliyepewa madaraka visiwani humo baada ya kuuawa kwa Abeid Karume, 1972, alikuwa ni Aboud Jumbe.

Jumbe, pamoja na kuifafanua serikali ya Zanzibar, na kuisogeza karibu zaidi na wananchi kwa kuanzisha Baraza la Wawakilishi, alizigundua hila za kuwaondolea Wazanzibari uhuru wao. Ili kuikabili dhuluma hiyo, Jumbe alindaa waraka ili hatari hiyo ikazungumzwe. 

Lakini, lilipofika kunakohuska, suala hilo halikuzungumzwa, na badala yake 'akajadiliwa' Jumbe mwenyewe! Suala la kuwepo hila za kuumeza uhuru wa Zanzibar likawekwa kando. Na matokeo ya 'kujadiliwa' Jumbe leo ni historia.

Kana kwamba Wazanzibari hawakuweka akilini yaliyomkuta Jumbe, aliyekuwa rais wa Zanzibar kabla ya Amani Karume kutangazwa na kuapishwa kuwa rais wa Zanzibar mwaka jana, Dk.Salmini Amour, alitenda jambo akidhani Zanzibar ni huru! 

Dk. Salmin alikusudia Zanzibar iingie uanachama wa OIC kwa lengo la kutaka kupata misaada ya masharti nafuu na pia ushirikiano wa kiuchumi na nchi wanachama ili kuikwamua nchi yake kutoka katika hali mbaya ya kiuchumi iliyotokana, pamoja na mambo mengine, na kuanguka kwa zao la karafuu katika soko la dunia ambalo ndilo lilikuwa zao kuu la biashara visiwani humo.

Lakini 'maelekezo' toka Dodoma ambako ndiko Jumbe alidhibitiwa, yalimwambia kwamba Zanzibar haina uhuru huo wa kujiamulia mambo yake kama jinsi walivyotamani Wazanzibari kiasi cha kuamua kumwondoa Sultan.

Ili kuhakikisha kuwa Rais wa Zanznibar hajaribu tena jambo kama hilo, katiba zikabadilishwa: kuanzia hapo Rais wa Zanzibar akapigwa 'stop' kuwa makamu wa Rais wa Muungano. 

Pamoja na yote hayo hitimisho liliandaliwa ili wale ambao walikuwa hawaelewi, miongoni mwa wazanzibar, waelewe. Hitimiho hilo lilikuja na sura nyingi.

Mojawapo ni pale wana-CCM Zanzibar walipomtaka Dk. Salmin aendelee kuwaongoza wakiamini kwamba maamuzi ya ndani ya nchi yao ni ya kwao wenyewe kwa vile nchi yao ni huu na walikwisha ondoa 'kiwingu' cha Sultan, Januari 12, 1964.

Lakini wapi! 'Dodoma' ikawaambia HAPANA. "Ninyi Wazanzibari hamna uhuru huo". Na ili kuliweka wazi zaidi suala hilo, baadhi ya wanasheria kutoka Chuo Kikuu wakawaambia (kama kuwashangaa na kuwauliza) Wazanzibari: "hivi ninyi hamelewi tu kuwa nchi yenu ni mkoa sawa na Dar es Salaam?"

Sura ya pili ya hitimisho lile ni pale Mahakama tya Rufaa nchini ilipotoa ufafanuzi wake juu ya hadhi ya Zanzibar kwamba Zanzibar si nchi (dola).

Sura ya tatu ya hitimisho la kuwafaya wazanzibari waelewe kwamba nchi yao haina ule uhuru wa kujiamulia mambo yake bila kuingiliwa kama wananchi wake walivyotaraji wakati wakimng'oa Sultan, ni pale Wazanziabri wana-CCM walipompendekeza mgombea wa kiti cha Urais na kumpa kura nyingi Dk. Mohamed Bilal. Lakini walipolifikisha jina hilo Dodoma, Wazanzibari wakaambiwa: "huyo (Dk. Bilal) siyo, bali atakuwa huyu (Amani Karume)".

Kufikia hapa tunapenda kuhoji: Hivi katika mazingira kama haya Wazanzibari wakitaka kuyapeleka mambo haya katika mahakama ya kimataifa, bado anweza kutokea mtu awaambie hiyo haifai?!

Kwani haifahamiki kwamba nchi mbili zinapoungana huwa kuna mkataba unaokubaliwa na pande zote mbili?

Tuonavyo sisi, ikiwa mtu atasimama katika misingi ya haki basi ataona kwamba ipo haja kwa Wazanzibari wote, bila kujali kambi za vyama vyao vya siasa, wanatakiwa kuyaunga mkono yale yaliyosemwa na Bw. Duni Haji kwamba sasa ipo haja ya kulifikisha suala la Zanzibar katika mahakama ya kimataifa.

Ni muhimu kwa wazanzibari wasibaki wakishesabu idadi ya miaka na miongo tangu kufanyika kwa mapinduzi hayo ya 1964; lakini ni muhimu, tena zaidi, kutazama iwapo kilichokusudiwa katika kuleta mapinduzi hayo kimepatikana.

Kwa kuwa kwa kiasi kikubwa tumeona jinsi Tanzania Bara ilivyogeuka 'kiwingu' juu ya uhuru wa Wazanzibari baada ya kuondolewa kwa Sultan, ipo haja ya msingi kwa akina Duni Haji na akina Amani Karume, wakapekuwa kuusaka ulipo mkataba ulioziunganisha nchi mbili hizi ambazo kila moja ilikuwa na uhuru wake kamili: Tanganyika na Zanznibar. Pengine hapo ndipo panaweza kuwa ni kizingiti kuelekea yalipo yaliyokusudiwa wakati wa mapinduzi ya Januari 12.
 

Juu
 

YALIYOMO
 

MAONI YETU
Mapinduzi Zanzibar yameleta kilichokusudiwa?

Wananchi wamwambia Mkapa:
Mbumbumbu wa demokrasia waliomo katika chama tawala ni hatari zaidi

Waislamu watakiwa kuwa watekelezaji wa maamuzi

‘Hajj Trust’ yaongeza huduma kwa mahujaji

DONDOO MUHIMU

MAKALA
Jamii ijihadhari viongozi wasaliti

MAKALA
Msimamo wa Pengo haushangazi

KALAMU YA MWANDISHI
Kitendawili cha millenia: Urais bila dola

MAKALA
Dhana ya kumwabudu Mungu anayeafiki udhalimu lazima tuikatae

MAKALA
Mapinduzi Zanzibar: Dhuluma bado ipo

MAKALA
CCM haiwezi kuondosha umasikini Tanzania

MAKALA
Tirivyogo la sekta ya elimu

Mwenye Macho……
Demokrasia haiwezi kujengwa kwa kuvunja katiba

HABARI ZA KIMATAIFA

MASHAIRI

MICHEZO

  • Baadaya Mkapa kushindwa kusaidia: Prof. Lipumba aombwa kuiombea Tanzania FIFA
  • Mtwa aanza kulala mapema
  • Salvatory aitwa Mtibwa

  •  

       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita