NASAHA
Na. 082 Jumatano Januari 10 - 16, 2001
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
MAKALA

Jamii ijihadhari viongozi wasaliti

Na Mikidadi Osman

HAPO Oktoba mwaka uliopita wasomi wa vyuo vikuu vya hapa nchi hii, waliitisha mgomo kwa nia ya kuitaka serikali itatue matatizo makubwa yaliyopo katika vyuo vya elimu ya juu, wanafunzi hao walikuwa wakidai, ongezeko la posho kwa kuwa kiwango cha sasa hakitoshi, pili waliitaka serikali ifute awamu ya tatu ya uchangiaji gharama, kwa Watanzania walio wengi hawana uwezo wa kulipa, na hili halina ubishi, kwani ni Watanzania wangapi wana uwezo wa kulipa shilingi zaidi ya milioni moja 1,000,000/- kwa mwaka wakati hizo shilingi 150,000/- tu za sekondari leo hii zinawashinda, tatu waliitaka serikali pia iboreshe mazingira ya kusomea, kwani mazingira ya usomaji ni mabaya mno, vitabu havitoshi, viti pia havitoshi, magodoro, vyumba vipo katika hali ya 'uchovu sana', n.k.
 

HATA hivyo serikali ikatumia njama kwa kila hali kuionesha jamii kwamba wanafunzi hao hawana shukrani, wasiojali maslahi ya nchi yao! Hatima yake wanafunzi hao wakasimamishwa masomo kwa miezi miwili, na baadaye kulazimishwa kukubali msharti yaliyowekwa na serikali kama wanataka kurudi masomoni, wanafunzi walio wengi walifanya hivyo na sasa wanaendelea na masomo. 

Hata hivyo, wapo baadhi ya wanafunzi ambao hawakuruhusiwa kufika chuoni kwa sababu ambazo zimetolewa na serikkali kutoka kwa 'vibaraka' wao hapo chuoni, wapo waliosimamisha masomo eti walihusika kuwashawishi wanafunzi wenzao wagome, wapo waliofutiwa udhamini, wapo pia ambao wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ambazo ni za uzushi tu na ni upuuzi mtupu. 

Tujiulize maswali yafuatayo, Je inawezekana kwa wanafunzi hao wachache wasiofika 25 kuwashawishi wenzao zaidi ya 5,000 kugoma? Au hao wengi waligoma kwa sababu waliamini kuwa wanadai haki zao na si kushawishiwa? Je ni harakati gani ya kudai haki ambayo haina viongozi? Je kuwa kiongozi wa wanafunzi maana yake ni kuitetea serikali kwa wanafunzi au kuwatetea wanafunzi pale wanapodai haki zao za msingi? 

Pamoja na hayo, wanafunzi wanaoshikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kubandika vipeperushi vyenye maneno ya kukashifu uongozi wa chuo na pia kutishia kumuua 'Rais' wa chuo Bw. Kusaja John, ni wanafunzi wangapi waliopo hapo chuoni wana uhakika na tuhuma hizo? Kwa nini tusiamini kuwa serikali inatumia vyombo vyake vya mahakama na habari kuonesha kuwa hao ndiyo waovu kama walivyofanya kwa wananfunzi wote kwa kuionesha jamii kuwa wanafunzi hao hawana shukrani, wakati wanadai haki zao? 

Nilibahatika kuongea na wanafunzi kadhaa hapo chuoni, nawengi wao wanakubali kuwa "Rais' wa chuo hicho ni Msaliti, pamoja na wanafunzi wengine ambao walishirikiana naye. 

Kwa sasa wanafunzi waliokuwa wakitetea maslahi yao wenzao hawapo chuoni, na wanafunzi wanaendelea na masomo yao hivyo basi ningependa kuwashauri wanafunzi hao yafuatayo: 

* Wautake uongozi wa chuo uwafahamishe kwa maandishi kuwa moja ya sifa za kuwa kiongozi wa wanafunzi ni kuitetea serikali kwa wanafunzi au sivyo. 

* Uongozi wa chuo utakiwe kueleza bayana kwamba uhuru wa kutoa mawazo chuo kikuu haupo, na chuo kikuu cha Tanzaniani sawa na shule ya msingi. 

* Katika uchaguzi ujao wa kiongozi wanafunzi wawe makini katika kuchagua viongozi, kwani sasa viongozi hawapo, waliobaki watatoa hoja gani za kuomba kura kwa wenzao - wakati sasa wapo kimya. 

* Wanaoendelea na masomo, lakini wajue wameshakuwa 'jamii saliti' ambayo imeonesha uchovu mkubwa. 

Pamoja na hayo, mgomo wa wanafunzi wa Vyuo Vikuu unatupa picha kwamba jamii ya Watzania inaweza kusimama na kudai haki kama itakuwa imara dhidi ya viongozi wenye tabia ya 'usaliti' kwani katu hawawezi kutetea mapinduzi ya kijamii. 
 

Juu
 

YALIYOMO
 

MAONI YETU
Mapinduzi Zanzibar yameleta kilichokusudiwa?

Wananchi wamwambia Mkapa:
Mbumbumbu wa demokrasia waliomo katika chama tawala ni hatari zaidi

Waislamu watakiwa kuwa watekelezaji wa maamuzi

‘Hajj Trust’ yaongeza huduma kwa mahujaji

DONDOO MUHIMU

MAKALA
Jamii ijihadhari viongozi wasaliti

MAKALA
Msimamo wa Pengo haushangazi

KALAMU YA MWANDISHI
Kitendawili cha millenia: Urais bila dola

MAKALA
Dhana ya kumwabudu Mungu anayeafiki udhalimu lazima tuikatae

MAKALA
Mapinduzi Zanzibar: Dhuluma bado ipo

MAKALA
CCM haiwezi kuondosha umasikini Tanzania

MAKALA
Tirivyogo la sekta ya elimu

Mwenye Macho……
Demokrasia haiwezi kujengwa kwa kuvunja katiba

HABARI ZA KIMATAIFA

MASHAIRI

MICHEZO

  • Baadaya Mkapa kushindwa kusaidia: Prof. Lipumba aombwa kuiombea Tanzania FIFA
  • Mtwa aanza kulala mapema
  • Salvatory aitwa Mtibwa

  •    Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita