|
Na. 035 Jumatano Februari 16 - 22, 2000 |
|
|
|
|
|
Matokeo kutoathiri sera ya mashamba HARARE, Zimbabwe. Kura ya maoni iliyopigwa wiki iliyopita nchini Zimbabwe licha ya kutoa ushindi mkubwa kwa walio dhidi ya serikali ya chama cha ZANU-PF kinachoongozwa na Rais Mugabe bado matokeo hayo hayatoathiri sera ya Serikali ya kuchukua mashamba kutoka kwa Wazungu na kuwagawia Wazalendo wa nchi hiyo ambao wengi wao ni Waafrika weusi. Kura ya maoni iliitishwa ili kutoa maoni juu ya muswada wa kumuongezea madaraka Rais. Katika matokeo ya kura hiyo robo tatu asilimia wameupinga muswada huo. Zimbabwe inatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa Bunge mwezi Aprili mwaka huu. Muswada huo uliokwama uliokuwa na lengo kumuongezea Rais madaraka umetafsiriwa na walio dhidi ya chama cha ZANU-PF kuwa ni agenda ya Rais Mugabe kumbakiza madarakani kwa muda zaidi. Rais Mugabe amekuwa Rais wa nchi hiyo kwa muda wa miaka ishirini hadi
hivi sasa. Pamoja na matokeo hayo, msimamo wa serikali bado ni ule ule
wa kuwagawia mashamba walio maskini kutoka kwa matajiri. Kwa muda mrefu
hivi sasa Zimbabwe imekuwa katika mgogoro wa lipi lifanyike katika kuwapatia
mashamba wasiokuwa nayo, walio wengi, kutoka kwa wamiliki wachache.
Afrika yasifiwa kutoa mazao bora BANKOOK, Thialand. Ripoti ya Umoja wa Matiafa imeisifu Afrika kuwa ni Bara linaloendelea
kuongoza kwa ubora wa mazao yake. Katika mkutano wa mawaziri, ripoti hiyo
ya UNCTAD imesema kuwa Afrika inaonesha kuwa ni maskani njema katika kutia
rasilimali baadaye mwaka huu. Mazao yanayozalishwa katika bara la Afrika
ni pamba ambayo huzalishwa kwa wingi huko Sudan na baadhi ya sehemu za
Tanzania na zao la buni ambalo hulimwa kwa wingi maeneo ya milima na ukanda
baridi wa bara hili. Mazao mengine ni mkonge, korosho na mengi ni ya mazao
ya kilimo. Katika mkutano huo nchi zinazoendelea zimezitolea mwito nchi
tajiri kurekebisha mifumo ya kibiashara ambayo haileti nafuu kwa nchi maskini.
Vile vile nchi hizo zimezitaka nchi tajiri kuzifutia madeni nchi changa.
Mwaka jana mataifa saba tajiri duniani yaliahidi kuzifutiamadeni nchi zinazodaiwa
kwa masharti kuwa madeni hayo yatumike katika huduma za jamii.
UNITA waendeleza mapigano WINDHOEK, Namibia. Waiganaji wa UNITA wamendeleza wimbi la mapigano katika harakati za kudai haki ya kupewa fursa sawa ya utawala nchini Angola dhidi ya Serikali iliyopo madarakani. Wapiganaji hao waliwaua wananchi kadhaa wiki hii katika mji wa Antagrara. Rais Sam Nujoma wa Namibia ameahidi kushirikiana na serikali iliyopo madarakani katika kupambana na UNITA. Hata hivyo pamoja na kuwa Rais Nujoma ameahidi kufanya hivyo kwa upande wa mpaka wa Namibia, Umoja wa Makanisa ya Kikatoliki nchini humo yameilaumu Serikali ya Rais Nujoma kwa kuona kuwa vita ndio njia pekee ya kuleta suluhisho la amani katika eneo hilo. Makanisa hayo licha yakuikemea serikali hiyo yametaka njia ya mazungumzo itumike ili kuleta suluhisho la amani. Angola imekuwa katika vita na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa miongo kadhaa hali ambayo imegharimu maisha ya Waafrika wa nchi hiyo kwa kiasi kikubwa. Imeelzwa kuwa chanzo kikuu cha mgogoro huo ni kutokana na tofauti za
kiitikadi kati ya itikadi ya kijamaa ya chama tawala cha MPLA na ile ya
kibepari ya UNITA huku kila upande ukitetea itikadi ya wazo mpachiko na
kuacha mfumo maridhawa wa Kiafrika.
Rais wa Ujeramani ziarani mashariki ya kati JERUSALEM Rais wa Ujerumani Bwana Yohannes Rao ameanza ziara ya siku kumi na moja, ziara ambayo itamchukua katika nchi mbili pamoja na Israel. Nchi atakazozitembelea Rais huyo katika ziara hiyo iliyoanza jana ni Palestina na Misri. Akiwa huko Israel anatarajiwa kulihutubia Bunge la nchi hiyo pamoja kuhamasisha kuongeza ukaribu wa urafiki kati ya Wajerumani na Wayahudi. Wajerumani na Wayahudi wamekuwa katika uadui kutokana maangamizo makubwa ya Wayahudi yaliyofanywa na Wajerumani kipindi cha utawala wa Adolf Hitler, hali ambayo kizazi kilichopo kinajitahidi kuihusisha kwa kufanya ushirikiano wa aina mbalimbali. Rais Rao akiwa nchini Palestina anatarajiwa kugusia suala la amani ya Mashariki ya Kati pamoja na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Ziara hiyo itamalizikia Misri kwa kukutana na Rais Hosni Mubaraka. Rais Hosni Mubaraka anatarajiwa kuzungumzia pamoja na mambo mengine kuhusu kukatishwa ziara iliyokuwa ifanyike nhini mwake mwaka jana na Waziri wa Ujerumani Bwana Yoska Fisher. |
YALIYOMO
Tahariri:
Wanafunzi wa Kiislamu shule za sekondari za serikali Dar wanyanyaswa Kanisa liliishinikiza serikali-Waislamu Sakata ya mabadiliko ya Katiba Zanzibar Kukiri kosa na kuomba radhi ndio kipimo cha utu Ushauri
Nasaha
MAKALA
MAKALA
Kalamu
ya Mwandishi
Makala
MAKALA
Riwaya
LISHE
|
|
|
|
|