|
Na. 035 Jumatano Februari 16 - 22, 2000 |
|
|
|
|
|
Vyakula vitupatiavyo mafuta Na Chamosi, H.J. BAADA ya kuona kwa muhtasari faida au umuhimu wa mafuta mwilini, ni vyema tukafahamu tutayapataje au tutaupatiaje mwili wetu mafuta hayo. Kwa kukukumbusha ndugu msomaji, ni wewe ndie unaewajibika na afya ya mwili wako, na wala si mtu mwingine atakaye kujalaumiwa juu ya afya yako mbovu. KWA hakika kila jambo lina mjuzi wake stadi (specialist). Lakini mjuzi wa yote yaliyodhahiri na yaliyofichikana ni Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye hasa anafahamu umuhimu wa mafuta mwilini mwetu. Chanzo cha awali kabisa cha mafuta mwilini tunaweza kukipata pale mwanzo mwili unapoanza kuumbwa. Bila shaka sote twafahamu "yai" ndio asili yetu ya mwanzo. Mimba ndogo kabisa ya siku moja, tayari huwa na mafuta. Baada ya hapo mimba huendelea kukua kwa kupata mafuta kutoka kwa mama kupitia kitovuni. Kama tulivyoona umuhimu wake hapo nyuma, mafuta husaidia kuyeyusha vitamini kama vitamini A, D, n.k. Vitamini hizi hutumika sana katika ukuaji bora wa mtoto tumboni. Hivyo basi kina mama wajawazito wapewe lishe bora ili waweze kuwa na ziada ya kuwapatia watoto wao tumboni. La sivyo watapoteza mafuta yao na kusababisha kukonda na kudhoofu na hata kupelekea mtoto aliyetumboni kudhoofu na kuwa na mtindio wa ukuwaji wa viungo, mfano ubongo. Chanzo cha pili cha mafuta mwilini ni pindi mtoto anapozaliwa. Kwa kawaida kabisa, mtoto azaliwapo chakula chake ni maziwa ya mama. Maziwa ya mama huwa na mafuta kwa kiwango kinachomfaa mtoto. Hivyo basi kina mama wawanyonyeshe watoto wao waziwa yao ili wapate mafuta kwa afya bora. Ama kwa wale wanaowapa watoto wao maziwa mengine kama ya ng'ombe, ya unga, mbuzi n.k. huwa kuna tofauti ya viwango vya mafuta. Maziwa mengine huwa na mafuta mengi zaidi ya kiwango anachopaswa mtoto kupatiwa. Na kila kinachozidi huishia kwenye madhara. Hivyo ni vyema kuwanyonyesha watoto wetu maziwa ya mama. Ama baada ya hapo tuangalie vyanzo vinavyopatikana katika vyakula. Vyakula vimegawanyika katika makundi. Kuna kundi la wanga, mboga mboga, matunda, nyama na maziwa. Vyakula aina ya wanga ni kama nafaka (mahindi, ulezi, mtama n.k.), Unga wa "dona" yaani unga wa mahindi usiokobolewa ni chanzo kizuri sana cha mafuta, au hata yale yaliyokobolewa kidogo au bila kulowekwa. Iwapo utashindwa kula unga wa dona tumia angalau kwenye uji. Aidha kama vyakula vyenye asili ya wanga ambavyo hupikwa kwa kutiwa mafuta, mfano vitumbua. Lakini hapa nimekusadia kazungumzia vile tu vyanzo asilia. Matunda pia huwa ni chakula kizuri kitupatiacho mafuta ya asili. Miongoni mwao ni parachichi, zeituni, na maganda ya matunda mbalimbali kama embe, mapera n.k. Hivyo nivyema kwa waangalifu wakati wa utayarishaji wa matunda na kwamba matunda yasimenywe sana. Mboga za majani pia hutupatia kiwango fulani cha mafuta. Mfano ni kabichi na (saladi). Kuna aina nyingi za matunda au mbegu za matunda ambazo ni vyanzo vizuri vya mafuta. Mfano mbegu za alizeti, pamba, nazi chikichi (maweze), mbegu za ubuyu, n.k. Na iwapo waweza kula matunda yake moja kwa moja ni vizuri. Au pia waweza kukamua nyumbani wewe mwenyewe. Ndugu msomaji kama wewe ni mkulima sina shaka unajua jinsi ya kukamua, na ndugu msomaji kama wewe ni mtu wa mjini, basi na usubiri watu wakukamulie viwandani watuletee mjini. Mfano mafuta ya mpishi n.k. Au jitahidi kutumia nazi, kutafuna mbegu za ubuyu n.k. Ama maziwa huwa ni chanzo kingine cha mafuta mwilini. Si mtoto peke yake anayepaswa kinywa maziwa bali kiumbe yeyote aliye hai maadam hayamletei matatizo. Maziwa yaweza kuwa ya ng'ombe, mbuzi na kondoo. Pamoja na kutupatia mafuta maziwa hutupatia manufaa mengi tu kama vitamini A. Wengine huondoa mafuta kwenye maziwa ambayo huitwa samli. Hivyo iwapo kama huwezi kunywa maziwa waweza kutumia samli katika mapishi yako. Mayai pia hutupatia mafuta tuyalapo. Waweza kuyala kupitia vyakula kama keki au kula mayai moja kwa moja yakiwa yamechmshwa au kukaangwa. Samaki, nyama ya wanyama mbalimbali huwa pia ni chanzo cha mafuta mwilini. Vyanzo vyote hivi ndugu msomaji waweza kupata moja kwa moja bila kuchanganya na kitu kingine. Na iwapo huwezi kutumia moja kwa moja, bado pia unaweza kupata kwa njia mbalimbali. Mfano kula vyakula vilivyopikiwa mafuta kama chapati, sambusa, maandazi, kababu, wali, na vyakula vingine vyote vilivyotiwa mafuta wakati wa mapishi. Kumbuka: mafuta yatokanayo na mimea ni bora zaidi kuliko mafuta yatokanayo
na wanyama. Hivyo jiepushe na vyanzo vya wanyama na jiweke karibu kabisa
na vyakula vyenye asili ya mimea.
|
YALIYOMO
Tahariri:
Wanafunzi wa Kiislamu shule za sekondari za serikali Dar wanyanyaswa Kanisa liliishinikiza serikali-Waislamu Sakata ya mabadiliko ya Katiba Zanzibar Kukiri kosa na kuomba radhi ndio kipimo cha utu Ushauri
Nasaha
MAKALA
MAKALA
Kalamu
ya Mwandishi
Makala
MAKALA
Riwaya
LISHE
|
|
|
|
|