|
|
| Chakula
na lishe
Matunzo ya mtoto mwenye lishe duni Na Mujahiid Mwinyimvua NENO lishe duni tunaweza kulitafasiri kama ile hali ya mwili wa binadamu (au kiumbe kingine) kukosa chakula (virutubisho) vya kutosha. Watoto laki moja na nusu (150,000) hufa kila mwaka Tanzania kwa sababu ya lishe na afya duni. Tatizo la lishe duni linasababishwa na sababu kadhaa zikiwemo upungufu wa chakula katika kaya (umasikini), maisha katika kambi za wakimbizi (vita), mama kukosa muda wa kutosha wa kumnyonyesha na kumlisha mtoto, maradhi, na elimu ndogo juu ya lishe bora. Kama una mtoto mwenye lishe duni ambae dalili zake ni pamoja na mtoto huyo kuwa dhaifu na mwenye kukonda, fuatilia makala hii ili uweze kuongeza elimu yako katika kulikabili tatizo la lishe duni. Kama tatizo la lishe duni ni maradhi ya mtoto, ni vyema mtoto huyo apelekwe hospitali kwa matibabu. Sambamba na matibabu apatiwe huduma nyingine kama itakavyoelezwa hapa chini. Tatizo la upungufu wa chakula katika kaya kama moja ya sababu ya lishe duni kwa mtoto, linasababishwa na mambo kadhaa, mojawapo ni umasikini. Katika kulikabili tatizo hilo, wananchi kwa upande wao waongeze nguvu katika kilimo (kwa wakulima) na wasiokuwa wakulima waongeze utendaji wao wa kazi. Wafanyakazi wakiongeza bidii katika kazi, uzalishaji au utoaji huduma utaongezeka, jambo ambalo linaweza kuwafanya waajiri kuongeza kipato cha wafanyakazi wao. Serikali nazo kwa upande wao, waongeze juhudi katika kuondoa umasikini, adui maradhi na adui ujinga. Vile vile serikali mbalimbali duniani zishirikiane ili kuondoa tatizo la vita katika dunia hii, kwa vile vita ni tatizo lingine kubwa linalochangia lishe duni kwa njia mbalimbali. Katika juhudi za kusaidia serikali zetu katika kupambana na adui ujinga, makala hii inachangia juhudi hizo kwa kuielimisha jamii namna bora ya kumtunza mtoto mwenye lishe duni. Mtoto mwenye lishe duni anatakiwa alishwe mara kwa mara na mzazi au mlezi ahakikishe kuwa mtoto anamaliza chakula alichomwandalia. Makala zetu za nyuma zilieleza kwa kina chakula kinachostahili kwa watoto. Hata hivyo, kwa faida ya wasomaji wangu wapya nitagusia swala hilo kwa ufupi. Kipindi cha utoto (siku moja hadi miaka 18 au zaidi kidogo) ndicho pekee kinachojishughulisha na ukuaji wa mwili wa binadamu. Kwa kuzingatia ukweli huo, watoto lazima wapatiwe kwa wingi vyakula vyenye kujenga mwili. Vyakula hivyo ni vile vya protini, kwa mfano maziwa ya mama na ya wanyama, nyama, mayai n.k. Sawia na vyakula hivyo, watoto pia lazima wapatiwe matunda ya kila aina, mboga za majani, maji ya kunywa na vyakula vyenye kutia nguvu na joto mwilini kama vile ugali, wali, mikate, karanga, siagi, n.k. Mara nyingine mtoto mwenye lishe duni huwa hana hamu ya kula chakula. Katika kama hiyo mzazi (mlezi) anatakiwa kutumia muda wake mwingi kumbembeleza mtoto na pia awe mvumilivu. Kulimsha mtoto chakula mara kwa mara kunaondoa uwezekano wa mtoto kuwa na kiwango kidogo cha chakula aina ya sukari katika damu (mwili). Kiwango kidogo cha sukari katika damu (au mwili kwa ujumla) kinaweza kuleta uharibifu wa ubongo (brain demage) na hatimaye kifo. Mtoto mwenye lishe duni hujisikia baridi sana hasa nyakati za usiku. Jambo hilo linaweza pia kusababisha kifo cha mtoto hasa mwenye umri wa chini ya miaka mitano. Ili kulikabili jambo hilo lazima mtoto awekwe katika mazingira ya joto la kawaida (joto lisiwe kali). Kuna njia mbalimbali zinazoweza kumfanya mtoto awe na joto linalotakiwa. Miongoni mwa njia hizo ni kumfunika mtoto na blangeti au kumvalisha nguo nzito hasa nyakati za usiku. Vile vile mtoto alishwe chakula mra kwa mara kama nilivyosema hapo awali (chakula kikisagwa mwilini hutoa joto). Pia mtoto asiwekwe karibu na dirisha au feni au kiyoyozi (Air condition). Zaidi ya hayo, mtoto lazima awekwe katika hali ya usafi na mwili wake usiwe na maji maji. Pia mzazi aongeze huruma na mapenzi kwa mtoto na acheze naye kwa muda wa kutosha. Kucheza na mtoto huinoa akili yake (mental development). Sambamba na hatua hizo familia/jamii nayo inapaswa kumpongeza mzazi
(mlezi) anayemtunza mtoto vyema na lazima asaidiwe anapokuwa na matatizo.
|
TAHARIRI HAKI YA KUABUDU MASHULENI: Hoja ya uwingi isizuie haki ya wachache Aliyeandika Yesu si Mungu bado akabiliwa
na kesi
Wazazi walia na Mkuu wa shule
Mkwawa
Serikali iache kudhulumu
Waislamu - Bakwata
KESI YA MIRATHI: Hukumu ya
Jaji Agostino yatupwa
Sumaye sasa atoa ‘waadhi’ Msikitini
Sekondari ya Kiislamu Sumbawanga,
mtihani kwenu – Sheikh Akilimali
37 wasilimu Mwanza
Akamatwa kwa kusoma gazeti la ANNUUR ! MGOGORO WA CHWAKA NA MARUMBI: Serikali
ya Dk. Salmin itafute ufumbuzi
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 4 Kwa nini walengwa wa mabomu wawe ni
Marekani?
Profesa amekosea kusema kwamba...
Ugaidi ni ugaidi, hata wa Marekani
ni ugaidi
UGAIDI: Chanzo si magaidi, ni dhuluma
ya Marekani
Jengeni familia bora
Tuwasaidie Waislamu kielimu
na kiuchumi - Bi Zuhura
Tumieni uhuru wenu vyema
Hoja za kutofautisha Yesu na Issa
ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 4
Mihadhara ya Wakristo yatawala Handeni
Ziara ya Kadinali Pengo Moro
Aonyesha ujuzi wa kutengeneza
Trekta
Waislamu wasizifanye sharia
za dini kuwa nzito – Sheikh Mzonge
Sengerema waomba msaada
Chakula na Lishe
|