AN-NUUR
Na.165 Jamadul Awwal 1419, Septembe 4 - 10, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
BARUA
 
[Nani gaidi Usama au Clinton?] . [Madrasa ziboreshwe] . [Wapenda amani wa Tanzania mbona kimya] . [Utamaduni wa Kimagharibi utatuangamiza] . [Marekani ishitakiwe] . [Mauaji ya Mwembechai ni nusra kwetu]
 

Nani gaidi Usama au Clinton? 

Ndugu Mhariri 

KWA mara ya kwanza najitokeza kutoa maoni yangu katika gazeti lako tukufu. 

Tukio la milipuko ya mabomu iliyotokea hapa Jijini Dar es Salaam na huko Nairobi Kenya, limepewa sura ya kigaidi na kushutumiwa kwa Usama bin Laden kuwa yeye ndiye aliyehusika na tukio hilo la kinyama, japo hakuna ushahidi wa kutosha kama kweli amehusika. 

Ni kweli kwamba tukio hili ni la kutisha na limesikitisha wengi kwani limeua raia wasio na hatia na kuwajeruhi wengine. 

Lakini kwa upande mwingine Clinton amefanya tendo la kigaidi zaidi na la kinyama ambalo linastahili kulaaniwa na kila mpenda haki, tendo la Clinton kuchukua sheria mkononi na kuteketeza raia wasiokuwa na hatia ni unyama mkubwa, hapo hataambiwa kuwa ni gaidi wa kimataifa. 

Ndiyo maana hata viongozi kama Katibu Mkuu wa OAU na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hawakumuunga mkono hata kidogo kutokana na unyama alioafnya; kuzishambulia Sudan na Afghanistan. Japo wameonyesha kutokuwa wakali kama ilivyokuwa katika kulipuliwa balozi. 

Lakini hilo halitasemwa kwa kuwa aliyefanya ni mtawala wa ulimwengu; ila tukumbuke usemi usemao "one man’s is another man’s freedom fighter" 
 

Njaritta M. 
Dar es Salaam. 
 
 

Madrasa ziboreshwe 

Ndugu Mhariri 

NINAOMBA nafasi kidogo kwenye gazeti letu ili nitoe maoni yangu kwa waalimu wa madrasa kuboresha masomo ndani ya madrasa zao. 

Ipo haja kubwa hivi sasa kufanya ukarabati ndani ya vyuo vyetu ili masomo yote yapatikane humo vyuoni kulingana na hali ilivyo. 

Vijana wetu wanapokwenda mashuleni hawapatikani kwenye madrasa ila siku ya Jumamosi na Jumapili tu kutokana na masomo ya ziada (tution) na kuwafanya kukosa masomo ya dini kwa wiki nzima. 

Mimi ninapendekeza kuanzishwa masomo yote kwa utaratibu mzuri ndani ya madrasa kuanzia chekechea, tution na darasa la akina mama. 

Wanawake wa Kiislamu watakapoelimika na vijana wao wa kike watapata msukumo mzuri wa kujua maadili mema ya Kiislamu. Wala hawatashawishi kushiriki kwenye maonyesho ya uchi kama Miss Aspen (Miss Tanzania). 

Waalimu wa madrasa kushirikiana na wazazi ipo haja kufikiria pendekezo langu na Insha Allah mfanyie kazi na pindi nikihitajika katika hili yakuleta maendeleo ya elimu mimi ndugu yenu nipo tayari kujitolea. 

Alhaj Y. Zakaria, 
P.O. Box 4362, 
Dar es Salaam. 
 Juu
 

Wapenda amani wa Tanzania mbona kimya 

Ndugu Mhariri 

BAADA ya milipuko ya mabomu kwenye balozi za Marekani Dar es Salaam na Nairobi wale wanaojiita wapenda amani na watetezi wa haki za binadamu walishutumu na kulaani vikali mashambulizi hayo. 

Lakini muda si mrefu Marekani ikafanya mashambulizi kama yale yaliyofanywa na wale wanaowaita magaidi, tena Marekani imefanya mashambulizi hayo kwa uwazi na kujigamba. 

Sasa kwa upande wetu sisi yetu macho na masikio. Je, wale wapenda amani wa Tanzania watainua midomo yao kulaani na kushutumu mashambulio hayo ya Marekani? 

Mwanakombo, 
Muheza. 
 
 

Utamaduni wa Kimagharibi utatuangamiza 

Ndugu Mhariri 

NINAOMBA unipe nafasi katika gazeti lako ili niweze kuzungumza machache ambayo ameniwezesha Allah (sw). 

Katika gazeti lako la Agosti 21 mwaka 1998 namba 163 katika ukurasa wa kumi na sita kuna habari inayozungumzia nasaha zilizotolewa na Sheikh Juma Salim Mbukuzi akiwataka vijana wa Kiislamu kujihadhari na utamaduni wa Kimagharibi unaoingizwa nchini ukiwa na nembo ya maendeleo. 

Sheikh aligusia ulevi, uzinifu na mavazi yasiyositiri mwili. Hayo yote naomba yapigwe vita na ikiwezekana yatoweke kabisa. 

Kuna lingine ambalo limenifanya niandike barua hii ambalo linazidi kuota mizizi hasa katika mkoa wetu huu wa Dar es Salaam. 

Hivi sasa kumezuka mtindo kila unapokuta ndoa za Waislamu sherehe zao zimeambatana na matarumbeta ambayo wanayakodi kwa gharama kubwa kabisaa na vikundi vingi vya matarumbeta hayo vinatoka Makanisani. Hivi Waislamu tumesahau Mtume (saw) alivyotuelekeza katika suna zake jinsi ya kusheherekea sherehe zetu? 
 

Salum Omar Yusuph, 
S.L.P. 75697, 
Temeke, 
Dar es Salaam. 
 Juu
 

Marekani ishitakiwe 

Ndugu Mhariri 

Milipuko iliyotokea Ijumaa, Agosti 7, 1998 kule jijini Nairobi na hapa Dar es Salaam katika ofisi za balozi za Marekani imeleta tafsiri za namna tofauti kwa Watanzania na duniani kote. 

Kwanza ninasikitishwa sana na tabia ya baadhi ya Watanzania na vyombo vya habari ya kutojenga tabia ya kuwa wachunguzi wa mambo na kupata uhakika ila kutanguliza hisia zao na kuhukumu waonavyo. Aidha, imeonyesha namna gani hata uongozi na vyombo vya Dola walivyo na mtazamo finyu katika kuelewa na kufuatilia mambo.  

Hapana shaka kwamba kumekuwa na udhaifu mkubwa katika kutafuta kweli iliyo nyuma ya milipuko iliyotokea. Kinachozingatiwa zaidi ni udini na utaifa yaani ni lazima walipuaji wawe ni Waislamu (siasa kali) au Waarabu na hivyo kuanza kazi bila ujuzi wowote ila kamatakamata na kupambiwa sana na vyombo vya habari vyote nchini ambavyo takribani vyote vinatenda kazi zao kwa kufuata itikadi za kisiasa na kidini.  

Hata kama itagunduliwa ni hao wanaoshukiwa lakini bado inapaswa sisi sote kujiuliza ni kwanini walipuaji wachukue hatua hiyo. Na kwanini iwe ni Marekani tu na hao ‘Waarabu’? Waislamu si wajinga kama inayodhaniwa bali ni watu mahir wanaoujua wajibu wao vilivyo kulingana na mazingira waliyomo. 

Walimwengu tungekuwa wakweli tungalifuatilia historia ya matukio kama hayo kisha tukaangalia sababu zinazowapelekea walipuaji kufanya hivyo; halafu tukaangalia pia historia inayotawala katika mahusiano ya serikali ya Marekani kimataifa ambayo ni mabaya kwa baadhi ya nchi au jumuiya za wananchi wa nchi kadha duniani. Hili liko wazi kwa wafuatiliaji wa mambo . Hivyo si rahisi kwa mtu kufanya madhara kwa mwema wake; bali kanuni iliyo wazi ni kudhuriana ima kwa kisasi au uonevu. 

Serikali ya Marekani ina sehemu yake katika vurugu zote na migogoro duniani na imekuwa wazi mno na kujiamini kuwa ni ‘mbabe’ wa dunia (Superpower) katika harahkati zake za kuegemea upande mmoja na kushinikiza au kuathiri mwingine kwa gharma zake na kwa malengo yasiyo ya kibinadamu. 

Hili limekuwa ni kero duniani na hata nchini Marekani wananchi wapenda haki wamekuwa wakilikemea sana na ndio maana baadhi ya milipuko imekuwa ikifanywa na Wamarekani wenyewe. Hivyo basi vita hiyo ipo na bila shaka ni kutoka sehemu zote duniani ambapo athari hizo zimefika. 

Alipokuwa akizungumzia mauaji ya kinyama pale Mwembechai, Makamu wa Rais, Dk. Omar Juma alitutaka wananchi tusiwalaumu polisi kwa kuua bali tuwalaumu wale waliwatuma wananchi wale marehemu kufanya vurugu iliyowalazimisha polisi kufyatua risasi! Basi kwa mantiki ya Mkuu wa pili wa nchi viongozi wetu Tanzania na ulimwenguni kote wasiwalaumu walipuaji wa mabomu tu, bali waulize pia kwanini?  

Aidha Marekani ni taifa kubwa lililoendelea katika sayansi na teknolojia na ni taifa lenye mbinu za hali ya juu za usalama. Inahitaji maandalizi makubwa mno kuweza kulihujumu kiasi kile tofauti na nchi nyingine changa. Na ndio sababu, kwa kulijua hilo, Rais wa Marekani Bw. Bill Clinton alisema "tutawatafuta [walipuaji hao wa mabomu] kwa gharama yoyote bila kujali itachukua muda mrefu kiasi gani ... tunajua kuwa wao ni maadui zetu na wana mitandao ya ugaidi wa kimataifa". Tukiyazingatia hayo, inatushangaza: eti katika siku tatu tu baada ya milipuko hiyo nguvu za dola za Tanzania zinadai zimekwisha watia mbaroni wahusika hao na wakuonewa siku zote ni waarabu na wasomali - ‘Mujahiddina’! Haya yote yanatoa tafsiri ya udini uliopo nchini na kutokuwa makini na mambo. 

Katika vita haizingatiwi raia mwema au asiye na hatia; na ndiyo sababu serikali ya Marekani iliwaua kwa makombora raia wasio na hatia huko Iraq, Libya na Lebanon na hapa kwetu ni Mwembechai. Ni Marekani hiyo hiyo inaendelea kusababisha mateso makubwa na hata vifo kwa raia wa Sudan kwa kumuunga mkono gaidi na muuaji mkubwa Bw. John Garang. Hali ni hiyo hiyo huko Palestina na Algeria. 

Inatusikitisha kwa viongozi wetu kutosema yaliyo ya haki. Makamu wa Rais Dk. Omar alipotembelea ubalozi wa Maerkani alisema kwamba "walipuaji hawa wanaua watu wasio na hatia"; lakin mbona serikali yetu haijawahi kuiambia Marekani kuwa inaua watu wasio na hatia huko Iraq na Libya kwa kulazimisha kuwepo kwa vikwazo dhidi ya nchi hizo. 

Yatupasa tuutambue ukweli kwamba wanaodhulumiwa na Marekani wanaweza kufikia ukomo wa uvumilivu na hii ni hali ya hatari sana kwa mwanadamu! Pengine niukumbushe umma duniani kote maneno aliyopata kusema Mwandishi mashuhuri wa riwaya Mtanzania Bw. Edi Ganzel, katika utangulizi wa riwaya yake ya Kitanzi kwamba mwanadamu ni mnyama kama wanyama wengine ila tu ni ustaarabu ndio unaomfanya adumishe amani, lakini akichokozwa na akachokozeka basi ukali na unyama wake ni zaidi hata wa yule mnyama wa porini, akimaanisha kuwa hapo mwanadamu huwa tayari kufanya lolote, hataogopa tena ‘virungu na risasi’ za poilisi wa Tanzania wala ‘maroketi’ ya Mmarekani! 

Wakati umefika sasa kwa jumuiya ya kimataifa kuimbia Marekani yafuatayo: 

1. Marekani yenyewe ndiyo inayochochea ugaidi. 

Pole (kifuta machozi) alichotuletea Bi. Madeline Albright, Waziri wa Mambo yaNchi za Nje wa Marekani, si chochote si lolote kwani tayari kuna ‘dazeni’ ya watoto ambao wamefanywa yatima baada ya baba zao kuuliwa, wapo dada zetu ambao sasa ni wajane baada ya waume zao wapenzi kuuawa na mabomu hayo ‘ya Marekani’. Hawa wanahitaji kusoma kula kuvaa na mengi mengineyo kwa siku kadhaa zijazo! 

Na zaidi ya yote hayo sasa Marekani ishitakiwe kwa kusababisha vifo vya watu wasio na hatia na pia hasara ya mali. 

Abubakar Msham, 
Dar es Salaam 
 
 Juu

Mauaji ya Mwembechai ni nusra kwetu 

Ndugu Mhariri 

NAOMBA nafasi japo pembeni. Napenda kuwafahamisha ndugu zangu Waislamu kutokana na akili yangu kuhusu hii kadhia ya Mwembechai. Nawaomba Waislamu tusihuzunike wala tusilegee wala tusikate tamaa kwa sababu hiyo ni nusra kwetu itokayo kwa Allah (sw). 

Imetuwezesha kuwajua wanafiq na waumini wa kweli. Imezibua hisia za waliolala sasa wameamka. Imesaidia kuifahamisha dunia uonevu tunaofanyiwa. La muhimu sasa ni kufanya shura za mara kwa mara ili tutafute njia za kujikomboa na dhulma hizi. Na tujue kwamba haki haiombwi. 
 

Arafa I. Gora, 
C/o Mama Msabaha,\ 
Dar es Salaam. 

Juu 
 

YALIYOMO
 
 
TAHARIRI  
HAKI YA KUABUDU MASHULENI: Hoja ya uwingi isizuie haki ya wachache  

Aliyeandika Yesu si Mungu bado akabiliwa na kesi  
Na Mwandishi Wetu  

Wazazi walia na Mkuu wa shule Mkwawa  
Na Mwandishi Wetu, Iringa  

Serikali iache kudhulumu  Waislamu - Bakwata   
Na Mwandishi Wetu 

KESI YA MIRATHI: Hukumu ya Jaji Agostino yatupwa  
Na Mwandishi Wetu  

Sumaye sasa atoa ‘waadhi’ Msikitini  
Na Mwandishi Wetu, Arusha  

Sekondari ya Kiislamu Sumbawanga, mtihani kwenu – Sheikh Akilimali  
Na Harun Rashid, Sumbawanga  

37 wasilimu  Mwanza  
Na Mwandishi Wetu, Mwanza  

Akamatwa kwa kusoma gazeti la ANNUUR !  

MGOGORO WA CHWAKA NA MARUMBI: Serikali ya Dk. Salmin itafute ufumbuzi  
Na Mwandishi Wetu, Pemba  

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 4  

Kwa nini walengwa wa mabomu wawe ni Marekani?  
Na Maalim Ali Bassaleh  

Profesa amekosea kusema kwamba...  
Na A.M. Hamza  

Ugaidi ni ugaidi, hata wa Marekani ni ugaidi  
Na Maalim Ali Bassaleh  

Dhana ya Udugu wa kiislamu  

UGAIDI: Chanzo si magaidi, ni dhuluma ya Marekani  
Na HASSAN KIMANGALE  

Jengeni familia bora  
Na Abuu Said, Iringa  

Tuwasaidie Waislamu kielimu na kiuchumi - Bi Zuhura  
Na SAID RAMADHANI KISSIMBA  

Tumieni uhuru wenu vyema  
Na Abuu Zaina, Iringa  

Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu,  ni uzushi mtupu! - 4   
Na Muhibu Said  

Mihadhara ya Wakristo yatawala Handeni  
Na Mwandishi Wetu, Handeni  

Ziara ya Kadinali Pengo Moro   
Na Mussa Ally, Morogoro  

Aonyesha ujuzi wa kutengeneza Trekta  
Na Mwandishi Wetu  

Waislamu wasizifanye sharia za dini kuwa nzito – Sheikh Mzonge  
Na Ashraf  Yusuf, Moshi  

Sengerema waomba msaada  
Na Idd Katimba, Mwanza  
  
Mafundisho ya Quran  

Barua za wasomaji  

Mashairi:  

Masomo ya dini ya Kiislam  

Chakula na Lishe  
Matunzo ya mtoto mwenye lishe duni  

Matangazo  
 
 

 

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita