|
|
| S.L.P. 55105,
SIMU 181365, DSM
TAHARIRI HAKI YA KUABUDU MASHULENI:
ZIPO haki za msingi za binadamu ambazo hazina bei wala hazitegemei ridhaa ya mtu yeyote. Na haki si fadhila ambayo mtu aweza kupewa na kupokonywa wakakati wowote. Uhai na kuishi ni haki ya msingi ya binadamu yeyote na katiba za nchi zote duniani hata zile za kidikteta zimeitambua haki hii japo kwa maandishi tu. Linaloandamana na haki hii ni haki ya mtu kulindwa yeye na mali yake. Mantiki ya haki hii ni kuwa uhai, heshima na mali ya mtu ni vitu vitakatifu. Uhai ni amana anayopewa mtu na Mola wake na hayupo yeyote aliyeidhinishiwa kumpora uhai huo bila sheria. Ndio maana tutaendelea kuhoji, kulikuwa na sheria gani iliyoidhinisha kuuliwa kwa Waislamu pale Mwembechai. Swali hili haliwezi kupata jibu maridhawa bila ya suala hili kufikishwa mahakamani. Damu ya watu imemwagwa, ni haki yetu wafiwa kuelezwa ni sheria gani ya nchi iliyo halalisha kukiukwa ile haki ya msingi ya kuishi watu wale. Haki nyingine inayoambatana na haki hii ni haki ya imani. Kwamba kila mtu ana haki ya kuamini dini atakayo, kuabudu na kuitangaza dini hiyo. Haki hiyo nayo si ya mjadala, fadhila wala yenye kutegemea ridhaa ya mtu. Kuitukuza siku ya Sabato ni moja ya mambo ya msingi katika imani ya watu wengine na hivyo ni haki yao ya kikatiba kupumzika siku hiyo. Kwa mantiki hiyo, ni makosa na kukiuka katiba kwa mamlaka yoyote kuihujumu haki hiyo kwa visingizio vyovyote viwavyo. Mfano hawezi kutokea mkuu wa shule akapanga mtihani ufanyike siku ya Jumamosi kwa kisingizio kwamba Wasabato ni wachache. Au akawazuia wanafunzi Wakatoliki wa bweni kwenda Kanisani siku ya Jumapili kwa hoja kwamba wengine wakipewa ruhusa hiyo huishia kijijini kunywa ulanzi. Inachoweza kufanya shule ni kuweka utaratibu wa kuwapata na kuwaadhibu hao wanaohujumu fursa hiyo na sio kuwanyima wengine haki yao. Ni kwa msingi huo huo hatutarajii Mkuu yeyote wa shule au sehemu ya kazi awazuie mabinti wa Kiislamu kuvaa hijab kwa kisingizio cha uchache wao au kuvaa sare. Wala hatutarajii kusikia wanafunzi Waislamu wazuiwe kwenda kuswali Ijumaa kwa hoja eti ni wachache na wanafunzi wengi Waislamu hawaswali. Suala la imani na ibada si jambo la kupigiwa kura, kwamba wengi wape. Ni haki ya msingi ya kikatiba hata akiwa mtu mmoja ni lazima haki yake hiyo iheshimiwe. Na tunadhani ni muhimu Masheikh wetu na Jumuiya za Kiislamu wachukue fursa hii kuwaelimisha waumini hasa hasa sehemu za kazi, mashuleni na vyuoni, juu ya haki zao hizi za msingi. Lakini ni muhimu vile vile serikali yetu ikawa makini juu ya masuala haya. Miongoni mwa mambo yanayochochea kuwepo mahusiano mabaya kati ya raia na serikali ni raia kuhisi wanaonewa, kupuuzwa na kudhulumiwa haki zao. Na ili kuzuia hali hiyo isitokee ni vyema yanapoibuka malalamiko yatizamwe kwa uadilifu na kama kweli wapo viongozi wanaokiuka katiba na maadili ya nchi wachukuliwe hatua za kisheria. |
TAHARIRI HAKI YA KUABUDU MASHULENI: Hoja ya uwingi isizuie haki ya wachache Aliyeandika Yesu si Mungu bado akabiliwa
na kesi
Wazazi walia na Mkuu wa shule
Mkwawa
Serikali iache kudhulumu
Waislamu - Bakwata
KESI YA MIRATHI: Hukumu ya
Jaji Agostino yatupwa
Sumaye sasa atoa ‘waadhi’ Msikitini
Sekondari ya Kiislamu Sumbawanga,
mtihani kwenu – Sheikh Akilimali
37 wasilimu Mwanza
Akamatwa kwa kusoma gazeti la ANNUUR ! MGOGORO WA CHWAKA NA MARUMBI: Serikali
ya Dk. Salmin itafute ufumbuzi
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 4 Kwa nini walengwa wa mabomu wawe ni
Marekani?
Profesa amekosea kusema kwamba...
Ugaidi ni ugaidi, hata wa Marekani
ni ugaidi
UGAIDI: Chanzo si magaidi, ni dhuluma
ya Marekani
Jengeni familia bora
Tuwasaidie Waislamu kielimu
na kiuchumi - Bi Zuhura
Tumieni uhuru wenu vyema
Hoja za kutofautisha Yesu na Issa
ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 4
Mihadhara ya Wakristo yatawala Handeni
Ziara ya Kadinali Pengo Moro
Aonyesha ujuzi wa kutengeneza
Trekta
Waislamu wasizifanye sharia
za dini kuwa nzito – Sheikh Mzonge
Sengerema waomba msaada
Chakula na Lishe
|