|
|
| Aliyeandika
Yesu si Mungu bado akabiliwa na kesi
- Adaiwa kujeruhi imani ya wengine
Na Mwandishi Wetu KIJANA Latifu Ismail Khan ambaye alikamatwa kwa kuandika baiskeli yake "Yesu si Mungu" bado anakabiliwa na kesi ya jinai kwa kile kilichodaiwa kwamba ni kuhatarisha amani. Kesi hiyo ambayo ipo katika mahakama ya Mwanzo mjini Korogwe imepangwa kuzungumzwa tena Septemba 22, 1998. Kwa mara ya kwanza kijana huyo alikamatwa Machi 28, mwaka huu na kupelekwa mahakamani Aprili 1, ambapo Mwendesha Mashitaka (polisi) Bw. Emanuel Kalenga alidai kwamba mtuhumiwa alihatarisha amani kwa kuandika kwenye baiskeli yake kwamba "Yesu si Mungu". Mtuhumiwa alikanusha na kwa vile upande wa mashitaka ulidai kwamba upelelezi umekamilika, mahakama ilipanga kesi ianze kusikilizwa. Katika kesi hii inayoshitaki ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mashahidi wake ni polisi wawili ambao kijana Latifu amewataja kwamba ni Bw. Stamili na Robert. Akiongea na mwandishi wa habari hizi mjini Korogwe Agosti 31, Latifu amedai kwamba kesi hiyo imeshazungumzwa mara moja tu, kwani mashahidi wamekuwa hawaji mahakamani. Kwa mara ya kwanza amesema ilizungumzwa Mei 24, ambapo shahidi wa kwanza Bw. Stamili alishuhudia kuona baiskeli kuandikwa "Yesu si Mungu" na akadai kwamba kwa kufanya hivyo mtuhumiwa alijeruhi imani ya watu wengine na hivyo kuhatarisha amani. Katika utetezi wake Bw. Latifu alitaka kujua kutoka kwa shahidi endapo kutangaza imani tofauti na watu wengine iwe kwa maneno au kwa maandishi kunahatarisha amani. Kwa maelezo ya Latifu, polisi Stamili (shahidi) alijibu kwamba kuna watu wanalalamika, ambapo alitakiwa na mshitakiwa awalete mahakamani hao wanaolalamika. Mpaka kesi ilipoahirishwa kwa mara ya mwisho Agosti, 28, bado Bw. Stamili alikuwa hajawaleta walalamikaji hao. Pamoja na hayo Bw. Latifu alitaka kujua kwa shahidi kwamba ni imani ipi inayokubalika mbele ya sheria za Tanzania; Yesu ni Mungu au Yesu si Mungu, ambapo alijibu kwamba zote zinakubalika. Shahidi wa pili Bw. Robert alikuwa atoe ushahidi wake Agosti 28, lakini hakutokea mahakamani. Kwa mujibu wa maelezo ya Bw. Latifu kesi imepangwa kusikilizwa tena Septemba 22, 1998. Akiongea na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwao mjini Korogwe, Bw. Latifu Ismail Khan ametoa wito na kuwakumbusha Waislamu wote kwamba wamche Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha na kuhakikisha kwamba hawafi ila wamekuwa Waislamu kamili. Wakati huo huo, mshiriki maarufu wa mihadhara ya kidini Jijini Dar es Salaam, Ustaadh Uliza Rashid amerejeshwa rumande baada ya dhamana yake kufutwa kwa madai ya kutohudhuria mahakamani mara kadhaa wakati wa kesi yake ikitajwa. Ustaadh Uliza ameshitakiwa kwa tuhuma ya kuhusika na vurugu zilizotokea mwaka jana (1997) katika mhadhara uliofanyika katika maeneo ya Mwananyamala jirani na kituo cha polisi cha Msisiri. Mapema mwaka huu wakati akizungumza na viongozi wa dini katika ukumbi
wa Karimjee, Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Ali Ameir aliagiza kufutwa kesi
zote zinazohusiana na mihadhara ya kidini iliyofanyika kabla ya kikao hicho
na aliahidi kwamba serikali ilikuwa ikifungua ukurasa mpya wa mawasiliano
na dini zote.
|
TAHARIRI HAKI YA KUABUDU MASHULENI: Hoja ya uwingi isizuie haki ya wachache Aliyeandika Yesu si Mungu bado akabiliwa
na kesi
Wazazi walia na Mkuu wa shule
Mkwawa
Serikali iache kudhulumu
Waislamu - Bakwata
KESI YA MIRATHI: Hukumu ya
Jaji Agostino yatupwa
Sumaye sasa atoa ‘waadhi’ Msikitini
Sekondari ya Kiislamu Sumbawanga,
mtihani kwenu – Sheikh Akilimali
37 wasilimu Mwanza
Akamatwa kwa kusoma gazeti la ANNUUR ! MGOGORO WA CHWAKA NA MARUMBI: Serikali
ya Dk. Salmin itafute ufumbuzi
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 4 Kwa nini walengwa wa mabomu wawe ni
Marekani?
Profesa amekosea kusema kwamba...
Ugaidi ni ugaidi, hata wa Marekani
ni ugaidi
UGAIDI: Chanzo si magaidi, ni dhuluma
ya Marekani
Jengeni familia bora
Tuwasaidie Waislamu kielimu
na kiuchumi - Bi Zuhura
Tumieni uhuru wenu vyema
Hoja za kutofautisha Yesu na Issa
ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 4
Mihadhara ya Wakristo yatawala Handeni
Ziara ya Kadinali Pengo Moro
Aonyesha ujuzi wa kutengeneza
Trekta
Waislamu wasizifanye sharia
za dini kuwa nzito – Sheikh Mzonge
Sengerema waomba msaada
Chakula na Lishe
|