AN-NUUR
Na.165 Jamadul Awwal 1419, Septembe 4 - 10, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Wazazi walia na Mkuu wa shule Mkwawa 

Na Mwandishi Wetu, Iringa 

WAZAZI ambao hawakutaka majina yao yafahamike wamemuandikia barua Katibu Mkuu Wizara ya Elimu kumlalamikia kuwa wanafunzi watano wa kike wa Kiislamu wa shule ya sekondari ya Mkwawa wanatukanwa, wananyanyaswa na kusumbuliwa kwa sababu ya kuvaa hijabu. 

Barua hiyo iliyonakiliwa kwa Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Elimu, Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya sekondari ya Mkwawa na Afisa Elimu wa Mkoa wa Iringa imenukuu waraka wa Wizara ya Elimu wenye Kumbukumbu Na.EDC/10/60/VOL.1/4/7 wa Agosti 28, 1995 kwa walimu wakuu wa shule za sekondari na vyuo vya elimu nchini iliyowataka watekeleze mara moja agizo la Rais la kuwaruhusu wanafunzi wasichana wa Kiislamu kuvaa hijabu za rangi zitakazoamuliwa na uongozi wa shule, kama msingi wa lalamiko lao. 

Walioandika barua hiyo wamedai Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Mkwawa wamesikika akijigamba kuwa katika kipindi chote atakachokuwa Mkuu wa shule hiyo, wasichana wa dini ya Kiislamu hawataruhusiwa kuvaa hijabu; labda watakuja kuvaa wakati yeye amehama. Hata hivyo wanafunzi wa Kiislamu mpaka jana walikuwa wanavaa vazi hilo. 

Waandishi wa barua hiyo iliyopatikana mjini hapa mwishoni mwa mwezi Agosti, wamesema kwa kuwa Wizara inapotoa agizo tegemezi ni agizo kutekelezwa, wanashangaa kwa Mwalimu Mkuu wa Mkwawa akatae kutekeleza agizo la Wizara linatolotokana na agizo la Rais. 

Wameelezea mategemeo yao kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu atachukua hatua zinazostahili kulipatia suala hili ufumbuzi haraka iwezekanavyo. 

Imefahamika mwanafunzi pekee aliyekuwa anavaa hijabu mwaka jana alilazimika kuihama shule hiyo kwa sababu hizo hizo.

Juu
 
 

Serikali iache kudhulumu Waislamu - Bakwata  

Na Mwandishi Wetu, Mwanza 

SERIKALI imedaiwa kuonyesha dalili za udini na ubaguzi katika utendaji wake jambo ambalo ni kinyume na maadili na katiba ya nchi. 

Hayo yamesemwa na viongozi wa Bakwata mkoani Mwanza hivi karibuni. 

Akitoa mfano Makamu Mwenyekiti wa Bakwata, Sheikh Idrissa Omar amesema kwamba hivi karibuni serikali iligawa eneo lililokuwa Ranchi ya Mabaki kwa taasisi za dini ambapo ni Kanisa la KKKT na Katoliki pekee waliopewa. 

Sheikh Idrissa alisema kwamba hilo lilifanywa kisirisiri kiasi kwamba Waislamu hawakujua kabisa mpango wa kuigawa ardhi hiyo baada ya Ranchi kufungwa. 

Akitoa mfano zaidi amedai kwamba serikali imewanyang’anya Waislamu eneo lao la Wakf na kuligawa kwa shule za msingi Mbugani, Nyakabungo na Mirongo. 

Sheikh Idrissa Omar amedai kwamba eneo hilo lilitolewa Wakf kwa Waislamu mwaka 1965 na familia ya Virj, lakini baadae wakaambiwa kwamba umiliki wao umefutwa. 

Toka wakati huo, amedai Sheikh Idrisa kwamba Waislamu wa Mwanza kupitia ofisi ya Bakwata mkoa wamekuwa wakiilalamikia serikali warudishiwe eneo lao hilo lakini imekuwa vigumu kwa serikali kukielewa kilio chao.Sheikh Idrissa ambaye alikuwa akiwasilisha malalamiko na madai haya ya Waislamu kwa Serikali kupitia kwa Meya wa Mji wa Mwanza, alitaja pia kutaifishwa kwa baadhi ya nyumba za Wakf. 

Aidha, alizungumzia jinsi serikali inavyojihusisha na sherehe za Kikristo kama ‘Christmas’ tofauti na inavyofanya wakati wa sherehe za Waislamu. 
 
Juu
 

KESI YA MIRATHI: 
Hukumu ya Jaji Agostino yatupwa 

Na Mwandishi Wetu 

JOPO la Majaji watatu limetengua hukumu ya Jaji Agostino Ramadhani ya Mirathi iliyowahusu Bw. Anwar Z. Mohamed na Said Seleman Masuka. 

Katika hukumu yake ya Juni 10, 1997, Jaji Ramadhani alihoji hukumu ya Jaji Msumi ya Septemba 5, 1996 iliyotengua wasia unaodaiwa kuachwa na Rukia Ahmed kwamba mume wake Bw. Anwar Z. Mohamed arithi mali yake yote. 

Katika hukumu yake, Jaji Msumi wa Mahakama Kuu wakati huo alitoa hoja kwamba kwa mujibu wa sheria za Kiislamu hakuna wasia kwa urithi na hakuna wasia zaidi ya theluthi ya mali. 

Uamuzi huo wa Jaji Msumi ulipingwa vikali na Jaji Korosso akiitaka mahakama ipuuze na waitupilie kwa mbali sheria hiyo ya Kiislamu kwa madai kwamba inavunja haki ya Kikatiba kifungu cha 24 kinachompa mtu haki ya kumiliki mali na kuitumia atakavyo. 

Hata hivyo, Jaji Msumi alisisitiza kwamba sheria za Mirathi za Kiislamu ni sehemu katika Qur’an na ni lazima Waislamu warithiane kwa sheria hii. 

Na akaonya kwamba kuichezea sheria hiyo ni sawa na kuichezea Qur’an, jambo ambalo alisema Jaji Msumi hadhani kwamba yupo mtu mwenye kuitakia mema nchi hii, anayeweza kulikaribisha. 

Jaji Ramadhani kwa upande wake alidai kwamba Jaji Msumi amejichanganya mwenyewe katika hukumu yake kwamba amezingatia "udini" na uzalendo badala ya sheria. Na alisisitiza kanuni ya kutotambua sheria au kanuni zinazokiuka haki za Kikatiba. 

Kwa kuzingatia hoja hiyo, Jaji Agostino Ramadhani alimpa muda zaidi mlalamikaji kukata rufaa japokuwa ulikuwa umepita dhidi ya hukumu inayotengua wasia anaodai kuachiwa na mkewe arithi mali yote (watoto wasipate kitu). 

Ni hukumu hiyo ya Mheshimiwa Jaji Ramadhani; J.A wa Mahakama ya Rufaa, kutoa muda zaidi ya kukata rufaa baada ya muda wa kisheria kupita, iliyotenguliwa. 

Waliotengua hukumu hiyo ni Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufaa; L.M. Makanja, D.Z. Lubuva na B.A. Samatta. 

Kwa hukumu hiyo, hukumu ya kuzuiwa kutekelezwa kwa wasia unaodaiwa wa marehemu Rukia Ahmed kwamba mali yake yote irithiwe na mume wake inabaki kama ilivyokuwa, kwa maana hiyo watoto wa marehemu huyo nao hawatapata haki yao ya kurithi kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. 

Katika kesi hii aliyekuwa mume wa marehemu Rukia Ahmed alidai kwamba mke wake alimuachia wasia wa kurithi mali yake yote. 

Watoto wa marehemu walipinga kutambuliwa kwa wasia huo kwani ni kinyume cha sheria za Kiislamu. 

 

Juu 
 

YALIYOMO
 
 
TAHARIRI 
HAKI YA KUABUDU MASHULENI: Hoja ya uwingi isizuie haki ya wachache 

Aliyeandika Yesu si Mungu bado akabiliwa na kesi 
Na Mwandishi Wetu 

Wazazi walia na Mkuu wa shule Mkwawa 
Na Mwandishi Wetu, Iringa 

Serikali iache kudhulumu  Waislamu - Bakwata  
Na Mwandishi Wetu

KESI YA MIRATHI: Hukumu ya Jaji Agostino yatupwa 
Na Mwandishi Wetu 

Sumaye sasa atoa ‘waadhi’ Msikitini 
Na Mwandishi Wetu, Arusha 

Sekondari ya Kiislamu Sumbawanga, mtihani kwenu – Sheikh Akilimali 
Na Harun Rashid, Sumbawanga 

37 wasilimu  Mwanza 
Na Mwandishi Wetu, Mwanza 

Akamatwa kwa kusoma gazeti la ANNUUR ! 

MGOGORO WA CHWAKA NA MARUMBI: Serikali ya Dk. Salmin itafute ufumbuzi 
Na Mwandishi Wetu, Pemba 

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 4 

Kwa nini walengwa wa mabomu wawe ni Marekani? 
Na Maalim Ali Bassaleh 

Profesa amekosea kusema kwamba... 
Na A.M. Hamza 

Ugaidi ni ugaidi, hata wa Marekani ni ugaidi 
Na Maalim Ali Bassaleh 

Dhana ya Udugu wa kiislamu 

UGAIDI: Chanzo si magaidi, ni dhuluma ya Marekani 
Na HASSAN KIMANGALE 

Jengeni familia bora 
Na Abuu Said, Iringa 

Tuwasaidie Waislamu kielimu na kiuchumi - Bi Zuhura 
Na SAID RAMADHANI KISSIMBA 

Tumieni uhuru wenu vyema 
Na Abuu Zaina, Iringa 

Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu,  ni uzushi mtupu! - 4  
Na Muhibu Said 

Mihadhara ya Wakristo yatawala Handeni 
Na Mwandishi Wetu, Handeni 

Ziara ya Kadinali Pengo Moro  
Na Mussa Ally, Morogoro 

Aonyesha ujuzi wa kutengeneza Trekta 
Na Mwandishi Wetu 

Waislamu wasizifanye sharia za dini kuwa nzito – Sheikh Mzonge 
Na Ashraf  Yusuf, Moshi 

Sengerema waomba msaada 
Na Idd Katimba, Mwanza 
 
Mafundisho ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi: 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Matunzo ya mtoto mwenye lishe duni 

Matangazo 
 

 

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita