AN-NUUR
Na.165 Jamadul Awwal 1419, Septembe 4 - 10, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Ugaidi: chanzo si magaidi, ni dhuluma ya Marekani 

Ugaidi ni utaratibu wa kutumia nguvu ili kumlazimisha mwingine kuachia haki zake alizozing’ang’ania. Ni utaratibu wa matumizi ya nguvu ili kumlainisha mwingine au kulipiza kwa yale uliyotendewa. Fuatana na Mwandishi Hassan Kimangale... 

Watu waliotambulika sana kwamba ni magaidi wakubwa ni Carlos, Muammar Ghadaf, Yasir Arafat, Garang, Dr Savimbi, D’la Khama n.k. Nchi zinazoitwa za kigaidi ni Libya, Iran, Sudan na Palestina. Lakini swali je, zinaitwa na nani, Na kwa vigezo gani? 

Ugaidi tunaweza kuugawa katika sehemu mbili ule wa vita vya msituni na ule wa kulipua mabomu kwa kuyatega au kwa kujilipua . Kwa kile kiitwacho mashambulizi ya kujitoa muhanga. 

Hadi hivi karibuni kumbukumbu zinaonesha kuwa Yasir Arafat si gaidi tena na Dr. Savimbi nusura asiwe gaidi kama angalikubali kujiunga na serikali ya Angola. 

Kwa bahati mbaya Mwenye Mamlaka ya kumuita mwingine gaidi ni Marekani kwa kawaida huwaita magaidi pale wanapotishia maslahi yake. 

Matumizi ya nguvu ya karibuni ni yale ya; bomu la Oklahoma City huko Marekani, Mabomu ya Nairobi na Dar es Salaam. Shambulizi la bomu kule Ireland ya Kaskazini, Mashambilizi ya Miza huko Sudani na Afghanistan yotge haya yaliua watu ambao hawahusiki na ugomvi wa wale watega mabomu na wategewa au watupa Miza na watupiwa. 

Huko Nairobi na Dar tunaambiwa watega mabomu wanataka kuwalazimisha Wamarekani kuondoka katika miji mitakatifu ya Kiislamu lakini Nairobi na Dar siyo wanapotakiwa waondoke. 

Huko Ireland na Oklahoma tunambiwa wanalipiza kisasi kwa kutotambuliwa maoni yao hasa kwa Ireland Ukatoliki kutotambuliwa. 

Kule Sudan na Afghanstan tunaambiwa Marekani inawashikisha abadu magaidi dunia nzima kwa kuipiga Sudan na Afghanstan. 

Jambo la kusikitisha ni kuwa kule Nairobi na Dar wale mia tatu waliokufa na wale elfu tano walioumia hawahusiki kabisa na hawajui hata hayo madai ya watega bomu. Kadhalika kule Sudan pia na Afghanistan wale waliouliwa na Miza za Mamarekani hawakujua hata madai ya Marekani. Hapa ndipo tunapoona kwamba utaratibu huu wa kupigwa na Juma wa Kwediboma na kwenda kumpiga Hamisi Kiwalani kwa kuwa ni mzigua kama Juma ni wa uonevu. 

Kwa kuua watu Afghanistan Marekani haikulipiza kisasi bali imefanya mauaji mapya ya kigaidi. Maana si onyo kwa walioua Dar na Nairobi bali ni msiba kwa waliopoteza watoto wao na watakuwa na haki ya kulipiza kisasi. Hali hii haipunguzi ugaidi inaongeza ugaidi. 

Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu ataona kuwa madai ya magaidi na ya Marekani ni sahihi magaidi wanadai kwamba Marekani imevamia sehemu zao na kufanya kila aina ya uchafu tangu ulevi hadi kutembea uchi hivyo kudhalilisha desturi zao. Marekani inamlinda Israeli akivamia haadhibiwi. Marekani inapoendeleza unafiki haitaki kulalamikiwa na haisikilizi malalamiko, hata yale ya kweli. Mfano mzuri ni ule wa Iraki. Wao wanasema ili haki itendeke basi timu ya ukaguzi wa silaha Iraki iwe ya kimataifa iwe na wajumbe toka Urusi, Uchina, Uingereza Ufaransa na kadhalika. Hiyo ni hoja ambayo kila mtu mwenye akili timamu angeikubali. Marekani wameikataa. Wao ndio walalamikaji, polisi, hakimu na bwana jela. Unamtazamia mwenye kunyimwa haki kwa dhuluma ya wazi hivi afanyeje na ikiwa hata umoja wa Mataifa unaona lakini umenunuliwa. 

Marekani nao wanasema sisi tupo kwenye ardhi hizo kulinda maslahi yetu hasa ya kiuchumi hatuwezi kuondoka kule. Hilo pia ni dai sahihi. 

Mvutano huu umegeuka kuondoana kwa kutumia mabavu. Magaidi wanatega mabomu na kuua hao maadui zao Wamarekani. Wamarekani nao wanalipiza kwa kuua adui zao magaidi. 

Sisi hatuna tatizo hadi hapo. Lakini shida yetu kubwa ni pale mabomu yanapoua watu wasiohusika na tena wala si Wamarekani.. Wamarekani kupiga Miza na kuua watu wasio husika eti wanalipiza kisasi kwa kuwa Usama bin Laden anaishi kule. Huu ni uamuzi wa mwenda wazimu. Mbona hawajaua ndugu wa Mmarekani aliyeua kule Oklahoma City kama kulipiza kisasi ni kuua yoyote ili mradini raia wa nchi atokayo muuaji. Mbona hawaja kipiga mabomu kiwanda kilichotengeneza bomu lililoua kule Olahoma City kama kila kiwanda kilichotengeneza kemikali zinazoweza kutengeneza bomu huangamizwa ikigundulika bomu lililolipuka lina kemikali za kiwanda kile. 

Kama ugaidi ni kutumia nguvu basi Marekani ni magaidi. Vitendo vya kuua Afghanistan na sudani ni kama vile vya kuua Nairobi na Dar hatuvikubali. Kama vingine wale wale wakosaji sisi tungeviunga mkono lakini kuuliwa wasiohusika hatuungi mkono. 

Hata hivyo bado kuna swali na kujiuliza kwanini mtu ang’ang’ania kuishi nyumbani kwako na vinapomfukuza atoe panga na kujeruhi wanao? Umfanyeje mtu huyo kama ndiye polisi, hakimu na mtawala wa sehemu hiyo? Itabidi umvizie umuue. 

Kwa upande mwingine tunapenda kuwapa mwanga Waislamu kwamba Marekani haikupiga Afghanstani na Sudan kulipiza kisasi. Inajua Sudan haihusiki na ingengoja hadi mwisho isingepata fursa ya kuzipiga maana ingejulikana kwamba hazihusiki. Sudan Libya, Iraki na sasa Afghanistan zilikuwa mdomoni mwa Marekani hata kabla ya uchunguzi. 

Pengine tungejiuliza kwanini Richard Butler anapotoa taarifa zake kuhusu uchunguzi wa silaha kule Iraki husema "Iraq bado ina silaha za hatari zinazoweza kuangamiza" Hivi Umoja wa Mataifa unaangamiza silaha za Iraki kwa manufaa ya Israeli? Marekani haipo Iraki kuondosha kitisho cha Israeli ili Israeli iendelee kukalia ardhi za Kiislamu na Marekani nayo sasa imeanza mradi huo wa kuzikalia kwa kisingizio cha ulinzi. Kumbuka unapokuwa mjinga unakuwa mradi wa mtu mwingine. 

Tutambue kuwa hao wanaoitwa magaidi wanafanya hayo si kwa kupenda bali wanadhulumiwa na njia za kidiplomasia zimekataliwa, na umoja wa mataifa umenunuliwa. Chanzo si magaidi ni dhuluma ya Marekani kwa wanaadamu wengine. Ni vita ileile ya Magharibi dhidi ya Uislamu. 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 
 

 TAHARIRI 
HAKI YA KUABUDU MASHULENI: Hoja ya uwingi isizuie haki ya wachache 

Aliyeandika Yesu si Mungu bado akabiliwa na kesi 
Na Mwandishi Wetu 

Wazazi walia na Mkuu wa shule Mkwawa 
Na Mwandishi Wetu, Iringa 

Serikali iache kudhulumu  Waislamu - Bakwata  
Na Mwandishi Wetu

KESI YA MIRATHI: Hukumu ya Jaji Agostino yatupwa 
Na Mwandishi Wetu 

Sumaye sasa atoa ‘waadhi’ Msikitini 
Na Mwandishi Wetu, Arusha 

Sekondari ya Kiislamu Sumbawanga, mtihani kwenu – Sheikh Akilimali 
Na Harun Rashid, Sumbawanga 

37 wasilimu  Mwanza 
Na Mwandishi Wetu, Mwanza 

Akamatwa kwa kusoma gazeti la ANNUUR ! 

MGOGORO WA CHWAKA NA MARUMBI: Serikali ya Dk. Salmin itafute ufumbuzi 
Na Mwandishi Wetu, Pemba 

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 4 

Kwa nini walengwa wa mabomu wawe ni Marekani? 
Na Maalim Ali Bassaleh 

Profesa amekosea kusema kwamba... 
Na A.M. Hamza 

Ugaidi ni ugaidi, hata wa Marekani ni ugaidi 
Na Maalim Ali Bassaleh 

Dhana ya Udugu wa kiislamu 

UGAIDI: Chanzo si magaidi, ni dhuluma ya Marekani 
Na HASSAN KIMANGALE 

Jengeni familia bora 
Na Abuu Said, Iringa 

Tuwasaidie Waislamu kielimu na kiuchumi - Bi Zuhura 
Na SAID RAMADHANI KISSIMBA 

Tumieni uhuru wenu vyema 
Na Abuu Zaina, Iringa 

Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu,  ni uzushi mtupu! - 4  
Na Muhibu Said 

Mihadhara ya Wakristo yatawala Handeni 
Na Mwandishi Wetu, Handeni 

Ziara ya Kadinali Pengo Moro  
Na Mussa Ally, Morogoro 

Aonyesha ujuzi wa kutengeneza Trekta 
Na Mwandishi Wetu 

Waislamu wasizifanye sharia za dini kuwa nzito – Sheikh Mzonge 
Na Ashraf  Yusuf, Moshi 

Sengerema waomba msaada 
Na Idd Katimba, Mwanza 
 
Mafundisho ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi: 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Matunzo ya mtoto mwenye lishe duni 

Matangazo 
 

 

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita