|
|
Mihadhara
ya Wakristo yatawala Handeni
UTAFITI uliofanywa na vijana wanaharakati wa Kiislamu wilayani Handeni umegundua kuwa zaidi ya asilimia 95 ya wananchi wa Handeni ni Waislamu na zaidi ya asilimia 98 ya mihadhara iliyofanyika na inayoendelea kufanyika ndani ya wilaya ya Handeni ni ya Wakristo tu. Sababu hasa zinazosababisha Uislamu kuzorota na kushindwa kufanya mihadhara ya dini yao ni kukosekana kwa chombo madhubuti cha kutetea Uislamu na kuanzisha mihadhara ya kuwazindua Waislamu na wasio Waislamu kurudi kwenye Uislamu. Uchunguzi umeonyesha kuwa mfumko wa mihadhara ya Wakristo toka awali ilikuwa ikifanyika kwa wingi na kwakuwakebehi Waislamu kwa kusema kuwa mtu yeyote wa Handeni asiye Mkristo hasa asiye mlokole hataingia peponi, vile vile mihadhara ya Wakristo imekuwa ikiwadanganya watu wa Handeni kuwa Yesu ni Mfalme wa Handeni na Yesu ni Mungu. Halikadhalika, mabinti wa Kiislamu hudanganywa na hatimaye kufanya ufuska na kuozwa ndoa za haramu kwa vijana wa dini nyingine. Huu ni mpango wao maalum watu hao wa Handeni kuhakikisha kuwa wanafanya kila hila ili kufanya ufuska na mabinti wa Kiislamu mwisho wanawaoa kabisa kiharamu. Baada ya hapo huwapa mafunzo ya dini zao na kuwatumia katika mihadhara yao ili kuwapotosha mabinti wengine wa Kiislamu. Takwimu ndogo tuliyoifanya inaonyesha kuwa zaidi ya mabinti tisa wa Kiislamu wilayani hapa tayari wamepotoshwa na kuingia katika dini hiyo na wengine wanaosoma, kundi hilo linawanyemelea kwa kuwadanganya kuwa watawaoa na kuwajengea nyumba ili waingie kwenye mtego. Huu ni msiba mzito ndugu Waislamu popote mlipo duniani. Jambo jingine la kusikitisha ni kuona kuwa baadhi ya Masheikh wilayani Handeni hushiriki katika harakati za kuzuia mawaidha na mihadhara ya Kiislamu kwa mfano Ijumaa moja baadhi ya vijana wa kundi la Tabligh wa mjini Chanika walizuiliwa kutofanya kazi ya kutoa mawaidha baada ya sala ya Ijumaa. Imamu wa Msikiti huo wa Kijiji cha Kwenjugo alizuia ujumbe huo wa Mwenyezi Mungu bila ya sababu yoyote ile ya msingi, alieleza kwa uchungu Ustadh Yasini ambaye alikuwa ni miongoni mwa vijana waliokwenda huko. Kutokana na kero hizo zote, baadhi ya wanaharakati wilayani Handeni wamegundua kuwa ili kuondokana na kero hizo pamoja na kero nyingine, Waislamu ni muhimu sana kuanzisha tawi la Al-Malid ambalo litahakikisha kuwa linashirikiana kikamilifu na vyombo vyote vya Kiislamu vyenye msimamo pamoja na Waislamu katika kuamsha na kuutangaza Uislamu kwa njia za mihadhara. Ustadh Fikirini Salimu akizungumza na vijana wenzake mara kwa mara nje ya Msikiti wa wilaya huwaambia kuwa ili haki na nusra ya Waislamu iweze kupatikana kwa kasi Handeni upo umuhimu wa kuwasiliana na uongozi wa Al-Malid Taifa ili kufanya mihadhara ya mara kwa mara kwa kuanzia Handeni Mjini hadi vijijini. "Tusipofanya harakati hizi dada zetu watazidi kuziniwa na Makanisa yatazidi kushamiri Handeni. Majuzi baada ya mawaidha ya Sheikh Hamim Boza wilayani Handeni yamesababisha makundi ya mikutano ya Wakristo kufanyika kwa kasi wilayani Handeni kwa mbwembwe na kebehi kwa Waislamu. "Kwa hiyo sisi vijana wa Kiislamu pamoja na baadhi ya wazee wenye msimamo
tunaomba kuwa popote walipo viongozi wa Al-Malid Taifa yaani Sheikh H.
Boza, Riko, Mwaipopo, Mazinge, Hussein E. Feruzi, Kipozeo, Magezi n.k.
msikie kilio chetu sisi Waislamu wa Handeni ili mje mapema kushirikiana
nasi kuunusuru Uislamu wilayani Handeni" alimalizia Ustadh Fikiri.
|
TAHARIRI HAKI YA KUABUDU MASHULENI: Hoja ya uwingi isizuie haki ya wachache Aliyeandika Yesu si Mungu bado akabiliwa
na kesi
Wazazi walia na Mkuu wa shule
Mkwawa
Serikali iache kudhulumu
Waislamu - Bakwata
KESI YA MIRATHI: Hukumu ya
Jaji Agostino yatupwa
Sumaye sasa atoa ‘waadhi’ Msikitini
Sekondari ya Kiislamu Sumbawanga,
mtihani kwenu – Sheikh Akilimali
37 wasilimu Mwanza
Akamatwa kwa kusoma gazeti la ANNUUR ! MGOGORO WA CHWAKA NA MARUMBI: Serikali
ya Dk. Salmin itafute ufumbuzi
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 4 Kwa nini walengwa wa mabomu wawe ni
Marekani?
Profesa amekosea kusema kwamba...
Ugaidi ni ugaidi, hata wa Marekani
ni ugaidi
UGAIDI: Chanzo si magaidi, ni dhuluma
ya Marekani
Jengeni familia bora
Tuwasaidie Waislamu kielimu
na kiuchumi - Bi Zuhura
Tumieni uhuru wenu vyema
Hoja za kutofautisha Yesu na Issa
ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 4
Mihadhara ya Wakristo yatawala Handeni
Ziara ya Kadinali Pengo Moro
Aonyesha ujuzi wa kutengeneza
Trekta
Waislamu wasizifanye sharia
za dini kuwa nzito – Sheikh Mzonge
Sengerema waomba msaada
Chakula na Lishe
|