|
|
Wanawake wa Kiislamu mikoa ya kusini wameungana na wenzao wa sehemu mbali mbali nchini katika matamko ya kuitaka Serikali iwachukulie hatua waliohusika na mauaji Mwembechai. Wanawake hao wa miji ya Lindi, Newala, Mtwara, Nachingwea na Masasi, walitoa matamko hayo katika makongamano tofauti yaliyofanyika katika miji hiyo wiki iliyopita. Aidha waliazimia kuwa na mshikamano miongoni mwao na kuunda jumuiya itakayosimamia shughuli mbali mbali za kijamii kanda hiyo. Wakizungumza katika makongamano hayo, wahadhiri mbali mbali waliilaumu Serikali kwa kushindwa kuunda tume ambayo wamesema ingechunguza tukio zima la Mwembechai na kutoa taarifa ya kina kama ilivyokwisha wahi kufanywa katika matukio mengine yanayofanana na hili. Walihoji ni kwa vipi polisi wavamie msikiti, kupiga na kudhalilisha waumini ambako ni kinyume na katiba ya nchi, Serikali isione umuhimu wa kufuatilia suala hilo mbali ya kuwatuhumu waathirika na kuwasweka rumande miezi kadhaa kabla ya kuwafikisha mahakamani. Wakizungumzia kudumaa kwa mikoa ya kusini kimaendeleo, waliilamu Serikali kwa kuitelekeza mikoa hiyo tangu nchi ipate uhuru. Walitoa mfano wa ubovu wa barabara kuu ya Dar es Salaam hadi Liwale na kusema kwamba umechangia kwa kiasi kikubwa kuiweka nyuma mikoa hiyo. Walionyesha wasi wasi kwamba huenda kutelekezwa kwa mikoa ya kusini kunatokana na idadi kubwa ya wakazi wa kanda hiyo kuwa Waislamu. Makongamano hayo yaliazimia pamoja na mambo mengine kuandaa kongamano kubwa la kanda ya kusini mwakani 1999 kula kiapo cha kutokurudia makosa ya kuwaweka madarakani watu ambao hawako tayari kufanya uadilifu. Wakati huo huo, wanawake wa Kiislamu wilaya ya Newala wamechanga shilingi 20,000 kwa ajili ya marehemu Ustaadh Swaleh Isa na kijana Chuki Athumani aliyepooza baada ya kupigwa risasi na polisi Jijini Dar es Salaam. Marehemu Ustaadh Swaleh aliyepigwa risasi na kufa papo hapo katika maeneo ya Mwembechai Jijini alikuwa mzaliwa wa Lindi. Swaleh alipigwa risasi na polisi Februari 13, mwaka huu katika kile kilichodaiwa na viongozi kuwa ni jitihada za polisi "kujihami" dhidi ya mawe yaliyokuwa yakirushwa na waumini wa dini ya Kiislamu. |
YALIYOMO
Maoni Kuwa na mawazo ya kufugwa tunajidharaulisha Sakata la
mabucha ya Nguruwe kuibuka upya
Bakwata yairushia polisi makombora Ngaramtoni MACHO YA
SHUTUMA
Serikali
yatakiwa iwachukulie hatua wauaji
Historia ya Msikiti wa Ngaramtoni Silaha yetu
ni kura ya pamoja
Anuani
ya fikra
Tunahitaji
"UN' ya Waislamu!
Kongamano la wanawake wa Kiislamu Newala lafana Umuhimu
wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo - 2
Kesi mojawapo ya mihadhara yafutwa Wasaidieni watoto wenye vipaji - Prof. Kilonzo Mahafali ya kidato cha nne Thaqafa: Wazazi wakumbushwa wajibu wao Wanafunzi
Mwanza wadai haki za kuabudu mashuleni kwa usawa
Saidianeni katika shida - Sheikh Abdallah Waislamu, Wakristo Rufiji watakiwa kuunda umoja Someni muiokoe jamii kimaadili Kesi
nyingine ya Waislamu Mwembechai yaahirishwa
Kusilimu kwa Wakristo kwaleta kero Mwanza Nzasa waomba msaada wa chakula, madawa Katibu wa Bakwata Moro ang'olewa Msikitini Chakula
na lishe
|