|
|
|
Kaka yangu na rafiki zake, wiki mbili zilizopita, walikuwa wakija nyumbani na nyuso za furaha, wakiwa wanaelezana kwamba mambo ni mazuri mwaka huu, kwani kila mtihani walioupata ulikuwa ndio wenyewe. Niliifahamu mipango yao yote. Kaka yangu alipewa hela za kununulia mitihani hiyo na mjomba. Rafiki zake walipewa na wazazi au ndugu zao. Mjomba alipoambiwa kwamba mitihani aliyoitolea fedha ilikuwa ndiyo yenyewe, alifurahi mno. Nilibahatika kuwaona pia baadhi ya ndugu na wazazi wa wale rafiki zake kaka. Wote hao walikuwa wakifurahi na kushukuru Mungu kuwa fedha zao hazikupotea bure, na wakawa na matumaini kwamba watoto wao wangefaulu kwa maksi za juu, na pengine kupelekwa kwenye shule za "watoto wenye akili nyingi." Lakini mara bomu likalipuka. Mitihani ikafutwa. Kaka yangu, rafiki zake, mjomba wangu, pamoja na wazazi na ndugu wa rafiki zake kaka wakawa wameudhika kupindukia. Fedha zao zimepotea, kurudishiwa haiwezekani. Waliokula wamekula na walioliwa wameliwa. Ni ule ule usemi usemao: wajinga ndio waliwao! Cha kushangaza ni kwamba, wale waliokuwa na furaha walipopata mitihani, na wale waliotoa fedha, eti sasa hivi ndio wamegeuka kuwa WAZALENDO wa kumshutumu Waziri wa Elimu kuwa ndiye anayewajibika. Midomo yao iko wazi kwa kelele: "Ajiuzulu! Ajiuzulu!" Kha! Sasa mimi nauliza: Hivi huyu Juma Kapuya anaambiwa ajiuzulu kwa sababu kawaumbua vibaka au? Mimi nadhani, wale ambao hawakubahatika kupata mitihani, ilibidi wamshangilie sana bwana.... Ah! samahani....Profesa Juma, kwa vile amewaumbua vibaka hawa. Ama wale ambao wameliwa hela zao, au walibahatika tu kupata mitihani ile, wapige tu kelele kwa vile wameumbuka! Kama mimi na akili yangu ya kitoto, ambayo bado haijaathirika na umri, ningepewa nafasi ya kutoa ushauri, ningewaambia wahusika kwamba, vibaka ni wale watendaji, na sio Juma. Watendaji ni tangu wanaotunga mitihani, wanaochapa, wanaoiweka kwenye mabahasha, wanaoisafirisha kuitawanya mikoani, na vile vile wanaoipokea huko ikifika. Katika hatua zote hizo nilizozitaja, Juma yuko katika section gani? Labda na yeye alikuwa akiipachika mitihani hiyo kwenye mabahasha!!! Akili ya kitoto kama yangu hailikubali hili. Sasa kama mambo ndio hivi, yaani likipatikana kosa la kiutendaji tu basi waziri anajiuzulu, nadhani wa kwanza kujiuzulu angekuwa ni yule wa Wizara ya Mambo ya Ndani, maana watu wa nchi hii hawaishi kwa raha kwa jinsi vibaka na majambazi wanavyowasumbua na kuwaua. Vile vile, kila Wizara ina uozo wake kiutendaji, mbona mawaziri wake hawatajwi? Au kwa vile huyu Juma amenasibishwa na "waswahili" wenzake ndio maana imekuwa nongwa? Mnataka refa ambaye angeacha mcheze rafu zenu tu bila ya kupiga filimbi? He! Watu wazima mtaacha lini chuki, husuda, uzandiki, udini na unafiki? |
YALIYOMO
Maoni Kuwa na mawazo ya kufugwa tunajidharaulisha Sakata la
mabucha ya Nguruwe kuibuka upya
Bakwata yairushia polisi makombora Ngaramtoni MACHO YA
SHUTUMA
Serikali
yatakiwa iwachukulie hatua wauaji
Historia ya Msikiti wa Ngaramtoni Silaha yetu
ni kura ya pamoja
Anuani
ya fikra
Tunahitaji
"UN' ya Waislamu!
Kongamano la wanawake wa Kiislamu Newala lafana Umuhimu
wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo - 2
Kesi mojawapo ya mihadhara yafutwa Wasaidieni watoto wenye vipaji - Prof. Kilonzo Mahafali ya kidato cha nne Thaqafa: Wazazi wakumbushwa wajibu wao Wanafunzi
Mwanza wadai haki za kuabudu mashuleni kwa usawa
Saidianeni katika shida - Sheikh Abdallah Waislamu, Wakristo Rufiji watakiwa kuunda umoja Someni muiokoe jamii kimaadili Kesi
nyingine ya Waislamu Mwembechai yaahirishwa
Kusilimu kwa Wakristo kwaleta kero Mwanza Nzasa waomba msaada wa chakula, madawa Katibu wa Bakwata Moro ang'olewa Msikitini Chakula
na lishe
|