|
|
Ikufuatia dua ya ufunguzi iliyotolewa na Bi. Halima Mnyamanzi kutoka AL-AZIZ Islamic Centre Masasi. Qur’an ilisomwa na Ukt Halima Nanjocha, kisha Mwenyekiti wa akinamama wa Newala Mama Ndija aliwakaribisha washiriki wote kuwatambulisha wageni. Ilisomwa risala ya akinamama wa Newala iliosomwa na Katibu wao Sharifa Ntangashari. Kongamano lilikusanya akinamama kutoka Newala, Lindi, Mtwara, Masasi, Nachingwea, Dodoma, Dar es Salaam na Kilwa. Jumla ya washiriki walikuwa 2800. Mada mbalimbali zilitolewa katika mtiririko ufuatao:- Mada ya kwanza ilihusu vazi la Hijab - Ilitolewa na Ukht. Fatma Juma ambaye alielezea ulazima wa vazi hili la Kiislamu, na alikemea sana tabia ya kwenda uchi na kuvaa nguo fupi, na akailaumu Serikali kwa kuruhusu mashindano ya kuwa uchi, yanaitwa ya urembo, wakati ni kumkashifu mwanamke. Aliwataka akinamama waliopo maofisini, wizarani, hospitali, michezoni, jeshini, na kwingineko wavae Hijabu wasidhani huko waliko hakuna Mungu. Akigusia tukio la Mwembechai alisema Serikali ya CCM iliwauwa akinamama, kuwadhalisha na kuwakashifu, wakati wakiwa msikitini,"huu ni unyama wa wazi, nashangaa kwanini mpaka leo wanaume hawajalipia kisasi, wakati Mtume (s.a.w.) alipigana vita na Mayahudi wa Qainuqaa kwa kumvua mwanake Hijabu", alisema na kuongeza. "Sijui kama kuna wanaume wa kweli hapa Tanzania." Akamalizia kwa kusema umefika wakati "sisi wanawake tuanze kazi." Mada ya pili ilikuwa juu ya Nafasi ya Waislamu hapa ulimwenguni. Mada hii ilitolewa na Mwenyekiti wa Idara ya Uhamasishaji wa Kamati ya akinamama Taifa Ukht Arafa. Yeye alizungumzia lengo la kuumbwa mwanadamu na sababu ya kuletwa hapa duniani na lipi wanatakiwa kufanya. Alieleza kuwa Muislamu ndio khalifa na ndio kiongozi wa Ulimwengu na ndio mwenye kuimarisha haki na usawa. Alisisitiza kuwa makafiri wao ni waharibifu na lengo lao ni kustarehe na kula. Hata siku moja hawapo tayari kupata matatizo bali hufanya juhudi za makusudi kuwatia wenzao matatizoni. Umefika wakati alisema Waislamu washike nafasi yao ya kuongoza dunia. Alisisitiza kuwa Uislamu ni mfumo kamili wa maisha, popote pale alipo Muislamu anatakiwa autekeleze Uislamu wake, iwe ni ofisini, nyumbani, shambani, Bungeni, vitani, michezoni n.k. Alimaliza mada yake kwa kuwataka Waislamu wote wake kwa waume wahamasishane juu ya kurejesha hadhi yao na kuchukua nafasi yao na kwamba Qur’an ndio katiba yao na umefika wakati sasa Waislamu waanzishe chama cha siasa chenye misingi ya Kiislamu na waanze kufanya kampeni. Mada ya tatu ilikuwa juu ya tukio la Mwembe Chai. Mada hii ilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Akinamama Taifa, Bi Fatma Lazaro. Alielezea chanzo na asili ya tukio la Mwembechai toka kauli ya Rais kule Tabora. Alisisitiza kwamba Waislamu wanaidai Serikali iunde tume huru ya uchunguzi, walioua wafikishwe mahakamani na wote waliodhalilisha wanawake wachukuliwe hatua za kisheria. Akinamama wengi walitokwa na machozi baada ya kusikia tukio la Mwembe Chai. Akazungumzia hali ya miji ya Waislamu. Alisema barabara kuu ya Dar es Salaam hadi Liwale ni mbovu sana haipitiki kabisa kuanzia Mnazi Mmoja mpaka Mtwara barabara ni mbovu kabisa haipitiki kwanini maeneo ya Waislamu barabara ni mbovu", alihoji. Kongamano liliendelea mpaka saa kumi na moja na nusu kwa maonyesho mbalimbali ya Hijabu na mengineyo. Hatimae kutoa maoni na maazimio yafuatayao:- 1. Kufanya kongamano kubwa sana la Kanda ya Kusini mwakani 1999. 2. Kutokurudia makosa mwaka 2000. 3. Kudumisha umoja na mshikamano na kuunda Jumuia ya akinamama wa Kanda ya Kusini. 4. Kulaani mauaji ya Mwembechai, kuitaka Serikali iwafikishe mahakamani wahusika. 5. Kuanzisha darsa za akinamama kila msikiti. 6. Kufanya mikutano ya Kiwilaya na Kimkoa kila mwezi. 7. Kila msikiti/madrasa uanzishe chekechea. 8.. Waislamu wafanye sensa kila msikiti wajuane. Baada ya kongamano kumalizika, Ustadh Yusuf Kayungilo alizungumza kwa
niaba ya wazee na Waislamu wa Newala, na wakaahidi kuwaunga mkono akinamama
kwa hali na mali.
|
YALIYOMO
Maoni Kuwa na mawazo ya kufugwa tunajidharaulisha Sakata la
mabucha ya Nguruwe kuibuka upya
Bakwata yairushia polisi makombora Ngaramtoni MACHO YA
SHUTUMA
Serikali
yatakiwa iwachukulie hatua wauaji
Historia ya Msikiti wa Ngaramtoni Silaha yetu
ni kura ya pamoja
Anuani
ya fikra
Tunahitaji
"UN' ya Waislamu!
Kongamano la wanawake wa Kiislamu Newala lafana Umuhimu
wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo - 2
Kesi mojawapo ya mihadhara yafutwa Wasaidieni watoto wenye vipaji - Prof. Kilonzo Mahafali ya kidato cha nne Thaqafa: Wazazi wakumbushwa wajibu wao Wanafunzi
Mwanza wadai haki za kuabudu mashuleni kwa usawa
Saidianeni katika shida - Sheikh Abdallah Waislamu, Wakristo Rufiji watakiwa kuunda umoja Someni muiokoe jamii kimaadili Kesi
nyingine ya Waislamu Mwembechai yaahirishwa
Kusilimu kwa Wakristo kwaleta kero Mwanza Nzasa waomba msaada wa chakula, madawa Katibu wa Bakwata Moro ang'olewa Msikitini Chakula
na lishe
|