AN-NUUR 
Na.176 Shaaban  1419, Novemba 20 - 26, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Maoni
Kuwa na mawazo ya kufugwa tunajidharaulisha
 

Yatupasa tujishangae nini kimetusibu Walimwengu wa leo. Iweje pamoja na akili zetu tuaminizo kuwa timamu tudhanie kwamba mtu akiwa hana mali au maguvu hana akili. Kwamba yeye hathubutu japo kusimama na kusema jambo fulani halifai, maadhali mkubwa kasema! 

Inashangaza na kusikitisha bali na kutia huzuni kwamba watu wote kuanzia viongozi wa nchi, vyombo vya habari na taasisi mbali mbali duniani wamesita kufikiri kwa akili zao ila hunena na kufikiri kwa akili za wengine. Wamegeuka kuwa vipaza sauti na wacheza ngoma inayopigiwa kwingine. 

Ulimwengu mzima hivi sasa unacheza zumari inayopigwa na Marekani kwamba Saddam Hussein lazima ashirikiane na wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa la sivyo ataadhibiwa kijeshi. 

Hakuna hata mmoja anayehoji kwamba je hilo linaloitwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lina uhalali gani? Pili je ni Iraq pekee iliyo na silaha zinazohitaji ukaguzi na kuangamizwa? Tatu Marekani ina uso gani kimaadili na uwajibikaji wa kusimamia, utengamano na amani ya mataifa mbalimbali duniani. 

Kinachojitokeza hapa ni kwamba Marekani kwa ubabe wake sio tu kwamba inaziburuza nchi nyingine pamoja na vyombo vinavyoitwa vya kimataifa, lakini hufanya itakavyo kwa kujua hakuna yeyote wa kuidhibiti. Maguvu yamefanywa ndio haki na hivyo kuifanya dunia itawaliwe na ubabe wa Marekani. 

Zipo nchi kama Uingereza ambazo huitwa Marafiki wa Marekani ambazo kila lisemwalo huko Washington wao ni hewala bwana. Hakika ya mambo hawa si marafiki wala washirika wa Marekani bali ni wanyonge wa Marekani. Uingereza haina inaloweza kupinga dhidi ya Marekani. 

Katika suala la Iraq Marekani inakuruza kila nchi na chombo cha Umoja wa Mataifa. Lakini Marekani nayo inakuruzwa na sera za Israel. Israel yenyewe ambayo, ina silaha za "Nuklia’ na imekataa kutia saini mkataba wa kuzuia silaha kali za maangamizi na pia ipo Mashariki ya Kati kama Iraq inayoshutumiwa kutishia nchi nyingine za eneo hilo. 

Marekani imeweka utaratibu ambao kwa vyovyote Iraq itakavyofanya haiwezi kutosheleza madai ya kinachoitwa maazimio ya Baraza la Usalama. Na ndio maana tunasema Iraq ina haki ya kulalamika kwamba haitendewi haki. 

Marekani yenyewe ina silaha za kila aina pamoja na zile za maangamizi. Hizo zinazoitwa silaha za kemikali (chemical weapons). Mwanzilishi si Iraq. Iraq imenunua kwa hao leo wanaowashutumu. 

Ipo hoja kwamba tahadhari inachukuliwa ati silaha za hatari zisiangukie mikono ya mtu asiye faa. Je, zikiwa mikononi mwa Marekani ndio zipo kwenye nchi inayofaa? Marekani ambayo imezivamia nchi nyingi na kuleta fujo iliyoleta hasara kubwa ya roho za watu na mali? Na juzi hapa ikaipiga Sudan kwa dhulma na kuzuia Umoja wa Mataifa usifanye uchunguzi! 

Sasa iweje pamoja na kwamba watu wana akili zao na nchi zinadai huru na zenye demokrasia lakini zinashindwa japo kusema. 

Zamani wakati wa TANU kulikuwa na msemo "Mawazo ya kufugwa". Sasa leo kama mtu hushindwa kuyapima mambo na kuamua kwa akili yake si ni utumwa ule ule. 

Yawezekana Serikali na nchi mbalimbali tukiwemo Tanzania, zimenyamaza kwasababu ni kaa la moto mguuni mwa wenzako. Ni Iraq itakayopigwa. Lakini kesho waweza kutushinikiza na masera yao bila kujali wananchi wetu wataathirika vipi na itatubidi tusalimu amri. Hapo ile dhana ya Taifa huru itakuwa imepoteza maana yake. 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
Maoni 
Kuwa na mawazo ya kufugwa tunajidharaulisha 

Sakata la mabucha  ya Nguruwe kuibuka upya 
Na Mwandishi Wetu  

Kondom sio kinga ya Ukimwi 

Bakwata yairushia polisi makombora Ngaramtoni 

MACHO YA SHUTUMA 
Na Abu Halima Sa Changwa 

Serikali yatakiwa iwachukulie hatua wauaji 
Na Mwandishi Wetu 

Historia ya Msikiti wa Ngaramtoni 

Silaha yetu ni kura ya pamoja 
Na Alhaj Yusuf Kalala, Washington DC  U.S.A 

Anuani ya fikra 
Na Abu Halima Sa Changwa 

Kuukaribisha mwezi mtukufu 

Tunahitaji "UN' ya Waislamu! 
Na Said  Rajab 

Kongamano la wanawake wa Kiislamu Newala lafana 

Umuhimu wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo - 2 
Na Ustaadh Kupa Pazi Said 

Kesi mojawapo ya mihadhara yafutwa 

Wasaidieni watoto wenye vipaji - Prof. Kilonzo 

Mahafali ya kidato cha nne Thaqafa: Wazazi wakumbushwa wajibu wao 

Wanafunzi Mwanza wadai haki za kuabudu mashuleni kwa usawa 
Na Iddi M. Katiba, Mwanza 

Saidianeni katika shida - Sheikh Abdallah 

Waislamu, Wakristo Rufiji watakiwa kuunda umoja 

Someni  muiokoe jamii kimaadili 

Acheni Shirki 

Kesi nyingine ya Waislamu Mwembechai yaahirishwa 
Na Muhibu Said 

Kusilimu kwa Wakristo kwaleta kero Mwanza 

Nzasa waomba msaada wa chakula, madawa 

Katibu wa Bakwata Moro ang'olewa Msikitini 

Masomo ya Dini ya Kiislamu  

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Umuhimu wa chakula katika shule za awali]  

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita