AN-NUUR 
Na.176 Shaaban  1419, Novemba 20 - 26, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Bakwata yairushia polisi makombora Ngaramtoni
 
  • Yadaiwa kuwalinda wahujumu mapato ya Msikiti
  • Wengine wadai wanawalinda wapenda sihri
UONGOZI wa Bakwata mkoani Arusha wamemtuhumu mkuu wa polisi Ngaramtoni Juu wilayani Arumeru kwa utendaji kazi uliojengeka katika mazingira ya kutia wasiwasi wa upendeleo na kukuika sheria. 

Aidha, uongozi huo wa Bakwata umetaka Mkuu wa Kituo cha Polisi Ngaramtoni Juu aache kuingilia masuala ya Waislamu kwani Waislamu wenyewe wana taratibu zao za kuendesha mambo yao. 

Katika barua yake ya Novemba 3, kwa mkuu huyo wa kituo, Katibu wa Bakwata mkoani Arusha, Alhaj Major Mohammed S. Mollel amedai kwamba Bakwata ina habari kwamba waumini wa Ngaramtoni wamekuwa wakiwekwa ndani bila ya dhamana kwa shinikizo la mkuu huyo wa kituo. 

Barua hiyo Na. BKT/AR/ARM/98/66 ambayo imenakiliwa kwa OCD Arusha na Usalama wa Taifa Arumeru, imeeleza kwamba kwa shinikizo la Wasomali na Waarabu wanaodai Msikiti ni mali yao amewafungulia mashitaka baadhi ya Waislamu kwa "kosa la kubughudhi waumini Msikitini". 

Aidha, barua hiyo imedai kwamba hao wanaomshinikiza kamanda huyo wa polisi ndio wachochezi wakubwa. Hivyo ikamtaka afanye kazi zake kwa uadilifu na kufanya uchunguzi kabla ya kukurupukia mambo vinginevyo hao wanaomshinikiza watamuacha pabaya. 

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba Sheikh Shaaban Juma aliwekwa ndani kwa muda wa siku tatu kwa tuhuma kwamba anawabughudhi waumini. 

Hata hivyo uchunguzi zaidi umeonyesha kwamba Sheikh huyo amekuwa akichukiwa na baadhi ya watu ambao hawataki taarifa ya mapato na matumizi ya Msikiti yawasilishwe kwa waumini. 

Aidha, imeelezwa kwamba Sheikh Shaaban Juma amekuwa mstari wa mbele kuwaelimisha Waislamu juu ya shirki ya sihiri. 

Imedaiwa kwamba wanaozuia waumini wasijue mapato ya Msikiti wao pamoja na wasiopendezwa na makemeo ya Qur’an dhidi ya sihiri ndio wanaomtilia fitna Sheikh Shaaban. 

Juhudi za gazeti hilo kuwasiliana na uongozi wa polisi mkoani Arusha dhidi ya tuhuma hizi hazikuweza kufanikiwa. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
Maoni 
Kuwa na mawazo ya kufugwa tunajidharaulisha 

Sakata la mabucha  ya Nguruwe kuibuka upya 
Na Mwandishi Wetu  

Kondom sio kinga ya Ukimwi 

Bakwata yairushia polisi makombora Ngaramtoni 

MACHO YA SHUTUMA 
Na Abu Halima Sa Changwa 

Serikali yatakiwa iwachukulie hatua wauaji 
Na Mwandishi Wetu 

Historia ya Msikiti wa Ngaramtoni 

Silaha yetu ni kura ya pamoja 
Na Alhaj Yusuf Kalala, Washington DC  U.S.A 

Anuani ya fikra 
Na Abu Halima Sa Changwa 

Kuukaribisha mwezi mtukufu 

Tunahitaji "UN' ya Waislamu! 
Na Said  Rajab 

Kongamano la wanawake wa Kiislamu Newala lafana 

Umuhimu wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo - 2 
Na Ustaadh Kupa Pazi Said 

Kesi mojawapo ya mihadhara yafutwa 

Wasaidieni watoto wenye vipaji - Prof. Kilonzo 

Mahafali ya kidato cha nne Thaqafa: Wazazi wakumbushwa wajibu wao 

Wanafunzi Mwanza wadai haki za kuabudu mashuleni kwa usawa 
Na Iddi M. Katiba, Mwanza 

Saidianeni katika shida - Sheikh Abdallah 

Waislamu, Wakristo Rufiji watakiwa kuunda umoja 

Someni  muiokoe jamii kimaadili 

Acheni Shirki 

Kesi nyingine ya Waislamu Mwembechai yaahirishwa 
Na Muhibu Said 

Kusilimu kwa Wakristo kwaleta kero Mwanza 

Nzasa waomba msaada wa chakula, madawa 

Katibu wa Bakwata Moro ang'olewa Msikitini 

Masomo ya Dini ya Kiislamu  

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Umuhimu wa chakula katika shule za awali]  

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita