AN-NUUR 
Na.175 Rajab 1419, Novemba 13 - 19, 1998 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Kansa ya tumbo
 

Na Mujahid Mwinyimvua 

TANGU wiki kadhaa zilizopita, makala zetu za chakula na lishe zinazungumzia ugonjwa wa kansa na namna ya kuukabili kwa silaha ya chakula. Katika kuendeleza kusudio hilo, makala hii inatoa ujumbe juu ya lishe na kansa ya tumbo. 

Kansa ya tumbo ni tatizo linalotishia maisha ya watu kama zilivyo aina nyingine za kansa. Wataalamu wanasema kwamba katika nchi ambayo vyakula vya kila siku vya watu ni vile vilivyohifadhiwa kwa madawa (preservatives), vyenye chumvi (nyingi) na vilivyosindikwa (Pickled foods), idadi ya watu wenye ugongwa wa kansa (salatani) ya tumbo huwa ni kubwa. 

Ukweli wa jambo hilo uko wazi zaidi katika nchi ya Japan, ambayo wananchi wake wanatumia zaidi vyakula vya aina niliyoitaja hapo juu. Kwa mujibu wa taarifa za mwaka 1984, kansa ya tumbo ndiyo iliyokuwa inaongoza kwa kuua watu wengi zaidi ikilinganishwa na aina nyingine za kansa. 

Hata hivyo, wataalamu hao wanasema kuwa, katika miaka 25 iliyopita, ugonjwa wa kansa ya tumbo duniani umepungua kwa asilimia sitini (60%). Hii ni kwa sababu ya teknolojia ya kuhifadhi vyakula kwenye majokofu (refrigeration). 

Vyakula vikihifadhiwa kwenye majokofu (ubaridi) huweza kukaa siku nyingi bila ya kuharibika. Kwa hiyo, mahitaji ya kuhifadhi vyakula kwa kutumia njia zenye kusababisha kansa (kama njia ya kuweka madawa, chumvi, moshi, n.k.) yanapungua. 

Ili kupunguza uwezekano wa kupata kansa ya tumbo hasa inayosababishwa na vyakula tunavyokula, watu lazima wazingatie ushauri wa lishe ufuatao: 

Kwanza, watu waache kula vyakula vilivyohifadhiwa kwa kutumia madawa hasa ‘nitrites’ na ‘nitrates’. Katika utumbo wa mwanaadamu, madawa hayo yanapambana na vitu vingine vijulikanavyo kama ‘aminesi’. Kutokana na mapambano hayo vitu vyenye kusababisha kansa hutokea. Vitu hivyo vinaitwa ‘nitrosamines’. 

Siku hizi ni jambo jepesi kununua vyakula visivyokuwa na ‘nitrites’, ‘nitrates’ na madawa mengine ya hatari. Jambo la kufanya ni kusoma ‘lebo’ kabla ya kununua chakula chochote kilichotengenezwa (kiwandani). 

Pili, epuka vyakula vyote vilivyohidhiwa kwa kutumia chumvi na kukaushwa kwa moshi. Vile vile epuka kula mara kwa mara aina ya vyakula vijulikanavyo kama ‘pickled foods’. 

Tatu, watu waepuke kula kila siku vyakula vilivyokaangwa kwa mafuta au vile vilivyookwa kwa kutumia oven (grilled foods). Hii ni kwa sababu njia hizo za kutayarisha vyakula zinasababisha nyama na samaki kutoa vitu vinavyosababisha kansa ya tumbo. 

Hivyo basi, ni vema watu wakapendelea vyakula vya asili na vile vilivyopikwa au kuokwa kwa njia ambazo si za hatari. 

Nne, watu wajitahidi kula vyakula vyenye vitamini A, B na C na pia vyenye madini ya ‘selenium’. Kwa ushahidi wa utafiti, vitu hivyo (vitamini na madini) vinasaidia kuzuia kutokea kwa kansa. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Maoni  
Kuvuja kwa mitihani: Tuweni wakweli kwa nchi yetu  

Katibu wa Baraza Kuu  azikwa Dar  
Na Mwandishi Wetu  

Ubabe wa madhalimu kuzimwa:  
Na Mwandishi Wetu  

MACHO YA SHUTUMA  
Na Abu Halima Sa Changwa  

Wazo mpachiko (Programmed mind)  
Na Abu Halima Sa Changwa  

Ta'azia: Abbas Shaaban Kilima 1938-1998  

Wasemavyo Wanaharakati  

Mdahalo kati ya Waislamu na Wakristo- 4  
Na Nandenga wa Mkomidachi  

Siri ya Miujiza  
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa  

Umuhimu wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo  
Na Ustaadh Kupa Pazi Said  

Ifahamu Madrasat Ghazal Muslim - Moro  
Na Mussa Ally, Morogoro  

Pamoja na sala, tusimamishe zakah  
Na Abubakari S. Marwillo  

Aina za maudhi yaliyoharamishwa juu ya Muislamu  
Na. Ramla  

Israi na Miiraji ni miujiza  
Mwandishi: Maalim Bassaleh  

Pamoja na ahadi ya Serikali kuzifuta: kesi za mihadhara zaendelea mahakamani  
Na Muhibu Said  

Waislamu Uluguruni  Moro wazama kwenye matambiko  

Imarisheni miradi ya elimu -  Prof.  Mikidadi  
Na Mwandishi Wetu, Dodoma  

Teknologia: Jifunze Kuunganisha Kompyuta (5)  
Na Hassan Omar  

Mafunzo ya Qur'an  
Shetani anawaogopesha wenye mali kutoa  

Chakula na lishe  
[Kansa ya tumbo]  

Matangazo  
 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita