|
Na.175 Rajab 1419, Novemba 13 - 19, 1998 |
|
KUNA suala ambalo linaitatiza sana akili yangu ya kitoto. Kama wewe ni mtoto mdogo kama mimi, unaambiwa huwezi kufanya jambo lolote kwa vile ni mdogo, na akili yako haijakomaa. Hiyo ndiyo nadharia iliyokuwepo duniani kote. Lakini kimatendo, naona kwamba binadamu huzaliwa na akili, lakini kila anavyokuwa mkubwa akili hupungua, kuvia na hatimaye kupotea kabisa. Ninazo hoja ambazo nina imani kuwa mtu yeyote asiye mtoto hawezi kuzipinga, hata akiwa na ndevu nyeupe kama mapovu ya sabuni ya unga. Nitatoa mfano mmoja tu. Ukiangalia mitaani utaona watoto ambao wakubwa wanawaita "Watoto wa Mitaani". Hata redioni na kwenye televisheni huitwa hivi hivi. Kwa akili yangu ya kitoto, hakuna mtu yeyote anayeweza kunieleza nikakulibali eti kwamba watoto hawa walitokea tu bila ya mume na mke ambao sio watoto. Lazima tu lilikuwepo dume na jike la binadamu waliowazaa. Lakini midume na mijike hiyo ya binadamu kama yako hai, yamekosa huruma kabisa ya kuwalea na kuwatunza watoto wao. Yani haya yameshindwa hata na kuku, kwani hatelekezi vifaranga hadi vikue. Kha! Haya basi, hata kama kuna wanaume na wanawake wa aina hii, wanawaacha watoto wao wazurure kama mbwa koko wasio na wenyewe, baba na mama waliyobaki mbona wanaona ni kawaida tu kuwa na watoto wanaoitwa wa mitaani? Ndiyo! Mimi huona baba na mama waliovalia vizuri, wengine wakiwa kwenye magari ya thamani, wakiwapita tu hawa watoto, masikini! Hamna hata anayenyanyua ukope! Utawaona watoto hawa wakikimbia uchi au na matambara, kwa vile hawana wa kuwanunulia nguo, au wanaokota makopo, kwa vile hawana wa kuwanunulia matoi, au wanaokota mabaki ya ukoko majalalani, kwa vile hakuna wa kuwanunulia chakula, na utawakuta wamelala upenuni mwa majumba, masokoni, au mitaroni, kwa vile hawana hata paka wa kuwaambia karibu. Akitokea mtu kwa bahati mbaya ambaye si mtoto, lakini bahati nzuri bado akili yake kidogo inafanya kazi, atawatupia shilingi hamsini au mia. Twasikia pia kuna watu walioanzisha vituo vya watoto. Lakini kwa kawaida, kwa jinsi niwajuavyo watu wasio watoto, lazima kuna maslahi yao tu. "Misaada kwa watoto" ni nembo tu ya kuwaombea fedha wale ambao kidogo bado akili zao hazijavia. Twasikia tu majina ya vituo, lakini bado twaona "watoto wa mitaani" na wanazidi kila uchao, na misaada hawapati. Cha kushangaza zaidi, watoaji wa mapesa, nguo na vyakula wapo, lakini wanapotoa, huwapa wenzao wenye akili zilizovia kama wao, hasa pale wanapogombea Urais au Ubunge. Kuna watu wazima wengine wanaitwa Mashehe na Mapadre. Nao pia hili hawalioni. Kampeni wanazozijua wao ni za "toa ndugu, toa ndugu", na zile za "kuwasaidia" wagombea, na sio "watoto wa mitaani". Sasa ikiwa hata shehe na Padre nao akili zao ni hizo hizo, ni nani basi asiyekuwa mtoto kama mimi, mwenye akili? Halafu watu wanatarajia pepo! Tubakie watoto watupu, huenda dunia ikawa na amani!
|
YALIYOMO
Maoni Kuvuja kwa mitihani: Tuweni wakweli kwa nchi yetu Katibu
wa Baraza Kuu azikwa Dar
Ubabe
wa madhalimu kuzimwa:
MACHO
YA SHUTUMA
Wazo
mpachiko (Programmed mind)
Ta'azia: Abbas Shaaban Kilima 1938-1998 Mdahalo
kati ya Waislamu na Wakristo- 4
Siri
ya Miujiza
Umuhimu
wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo
Ifahamu
Madrasat Ghazal Muslim - Moro
Pamoja
na sala, tusimamishe zakah
Aina
za maudhi yaliyoharamishwa juu ya Muislamu
Israi
na Miiraji ni miujiza
Pamoja
na ahadi ya Serikali kuzifuta: kesi za mihadhara zaendelea mahakamani
Waislamu Uluguruni Moro wazama kwenye matambiko Imarisheni
miradi ya elimu - Prof. Mikidadi
Teknologia:
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (5)
Mafunzo
ya Qur'an
Chakula
na lishe
|