AN-NUUR 
Na.175 Rajab 1419, Novemba 13 - 19, 1998 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Ubabe wa madhalimu kuzimwa:
‘Wamarekani walikiona cha moto Iran’

Na Mwandishi Wetu

IMAMU na Khatib wa Msikiti wa Ma’mur Sheikh Talib amesema kwamba ucha Mungu na kumtegemea Mwenyezi Mungu ni silaha na kinga kubwa kwa muumini. 

Akifafanua nukta hii, Sheikh Talib alitoa mfano wa tukio la Mtume (s.a.w.) kutoka salama akielekea Madina wakati nyumba yake ilikuwa imezungukwa na wauaji. 

Alisema Mtume (s.a.w.) alisoma Surat Yaasin huku akiwatupia mchanga wauaji hao na wakalala usingizi huku Mtume (s.a.w.) akiwapita hawana habari. 

Sheikh Talib akihutubia siku ya Ijumaa iliyopita alisema kwamba tukio kama hilo limejirudia katika miaka ya hivi karibuni ambapo ndege za Wamarekani zilipongana wenyewe kwa wenyewe zikiwa angani zilipokuwa zinajaribu kuivamia Iran ili kuwaokoa Wamarekani waliokuwa wanashikiliwa mateka. Kama alivyofanya Mtume (s.a.w.) Sheikh Talib alisema kwamba Wairan walisoma Surat Yaasin na nguvu za Wamerakani zikayeyuka angani. 

Kwa mifano hiyo Sheikh Talib alisisitiza kwamba mafanikio na ulinzi kwa waumini unatoka kwa Mwenyezi Mungu na kuwaonya wale wanaokimbilia kwenye mizimu. 

Hata hivyo, Sheikh Talib aliwakumbusha waumini kwamba wasitarajie kupata mafanikio pekee katika mambo yao halikadhalika kupata ushindi tu kila wakati. 

Alisema kwamba ni katika utaratibu wa Mwenyezi Mungu kuwajaribu waumini ili wapate kujulikana wale waumini wa kweli na wale waongo. 

Katika kujaribiwa huko Sheikh Talib alisema kwamba matatizo mbalimbali yatawakuta waumini na watakaofuzu na kufanikiwa ni wale watakao subiri na kumtegemea Mwenyezi Mungu. 

Awali katika khutba yake Sheikh Talib alieleza falsafa ya miraj na Israh ambayo ni katika matukio muhimu katika historia ya Uislamu. 

Miraj ni safari ya Mtume (s.a.w.) kutoka Makka hadi Baitil Muqadas wakati Israh ni safari ya Mtume (s.a.w.) kutoka Baitil Muqadas hadi wingu wa saba na kurejea. 

 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 

 Maoni  
Kuvuja kwa mitihani: Tuweni wakweli kwa nchi yetu  

Katibu wa Baraza Kuu  azikwa Dar  
Na Mwandishi Wetu  

Ubabe wa madhalimu kuzimwa:  
Na Mwandishi Wetu  

MACHO YA SHUTUMA  
Na Abu Halima Sa Changwa  

Wazo mpachiko (Programmed mind)  
Na Abu Halima Sa Changwa  

Ta'azia: Abbas Shaaban Kilima 1938-1998  

Wasemavyo Wanaharakati  

Mdahalo kati ya Waislamu na Wakristo- 4  
Na Nandenga wa Mkomidachi  

Siri ya Miujiza  
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa  

Umuhimu wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo  
Na Ustaadh Kupa Pazi Said  

Ifahamu Madrasat Ghazal Muslim - Moro  
Na Mussa Ally, Morogoro  

Pamoja na sala, tusimamishe zakah  
Na Abubakari S. Marwillo  

Aina za maudhi yaliyoharamishwa juu ya Muislamu  
Na. Ramla  

Israi na Miiraji ni miujiza  
Mwandishi: Maalim Bassaleh  

Pamoja na ahadi ya Serikali kuzifuta: kesi za mihadhara zaendelea mahakamani  
Na Muhibu Said  

Waislamu Uluguruni  Moro wazama kwenye matambiko  

Imarisheni miradi ya elimu -  Prof.  Mikidadi  
Na Mwandishi Wetu, Dodoma  

Teknologia: Jifunze Kuunganisha Kompyuta (5)  
Na Hassan Omar  

Mafunzo ya Qur'an  
Shetani anawaogopesha wenye mali kutoa  

Chakula na lishe  
[Kansa ya tumbo]  

Matangazo  
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita