|
Na.175 Rajab 1419, Novemba 13 - 19, 1998 |
|
KESI za mihadhara zilizofunguliwa mwishoni mwa mwaka wa jana(1997) ambazo Serikali iliahadi kuzifuta mwanzoni mwa mwaka huu zinaendelea kutajwa katika mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam. Washitakiwa katika kesi hizo wanatuhumiwa na Serikali kuwa kupitia muhadhara wao uliofanyika katika Msikiti wa Komakoma (Masjid Subra), Mwananyamala "A", jijini Dar es Salaam, mapema Oktoba Mosi na Septemba 25, mwaka jana (1997), walikashifu BibliaTakatifu, Wakristo, Jeshi la Polisi na viongozi wake wakuu, kutishia usalama wa nchi, kukishambulia kituo kidogo cha polisi cha Msisiri, kilichopo Mwananyamala ‘A’, jijini na kuharibu mali za kituo hicho. Watuhumiwa katika kesi hizo ni pamoja na Uliza Rashidi (37), Swalehe Rashid (30), Ramadhani Makwangu (30), Ally Majapa (42), Ally Athumani (40), Hamisi Swalehe (50), Ramadhani Hamisi (30) na Magezi Shaban. Mapema mwezi Januari mwaka huu, Serikali kupitia Jeshi lake la Polisi, ilitangaza rasmi kufuta kesi zote zinazohusiana na mihadhara kwa kila ilichodai kuanza ukurasa mpya wa namna "nzuri" ya kuendesha mihadhara ya dini nchini. Pamoja na tangaza hilo, lakini kesi hizo ambazo zilifunguliwa na Serikali katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu Jijini, bado ziko mahakamani, ambapo yapata mwaka sasa hazijaanza kusikilizwa, licha ya upelelezi wake kudaiwa kukamilika. Jumanne ya wiki hii mahakama ya Kisutu iliahirisha kesi hiyo yenye namba 1383 inayowakabili Waislamu hadi Novemba 24, mwaka huu, tarehe ambayo inatarajiwa tena kuanza kusikilizwa. Uamuzi huo wa mahakama wa kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe hiyo, umezingatia ombi la mwendesha mashitaka wa Serikali, Inspekta wa Polisi, Bw. Rashidi Ngonyani la kuomba kuahirishwa kesi hiyo kutokana na mashahidi wa upande wa Serikali kutofika mahakamani siku hiyo (ya Jumanne ya Novemba 10, 1998) kama ilivyotarajiwa. Aidha kwa mujibu wa Hati mpya ya mashitaka (charge sheet) iliyosomwa mahakamani hapo hivi karibuni na mwendesha mashtaka huyo wa Serikali, Bw. Rashidi Ngonyani, imedhihirika pia kuwa shitaka hilo (la kushambulia kituo) dhidi ya washitakiwa limebadilishwa. Tofauti na Hati ya awali ya shitaka hilo, sasa inadaiwa katika Hati hiyo mpya kuwa watuhumiwa watano ukimtoa Magezi Shabani kuwa katika muhadhara wao huko Mwananyamala waliwafanyia fujo waumini wa dini nyingine na kuwazuia polisi kufanya kazi yao. Aidha, katika Hati hiyo (mpya) inadaiwa pia kuwa Magezi akishirikiana na watuhumiwa wenzake watano waliwachochea wafuasi wao kukishambulia kwa mawe na matofali kituo hicho kidogo cha Polisi cha Msisiri, Mwananyamala ‘A’ na kuharibu mali za kituo hicho. Katika kesi hiyo, mwendesha mashitaka, Inspekta Msaidizi wa Polisi, mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Bi Cypriane William, alidai kuwa mnamo Septemba 23, mwaka jana (1997) huko Mwananyamala ‘A’, Wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, washitakiwa walitoa maneno yenye lengo la kukashifu imani ya watu wengine. Mwendesha mashitaka huyo aliendelea kudai kuwa washitakiwa hao walisema Biblia siyo kitabu cha kweli na kwamba wangepambana na wanaume ambao wangesogea kwenye jukwaa lao mpaka kufa. Wakati huo huo, baada ya kusota rumande kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu kwa tuhuma ya kutohudhuria mahakamani, hatimaye mahakama ya Kisutu imeamuru kuachiwa kwa dhamana Ustadhi Uliza Rashidi. Ustaadhi Uliza aliachiwa Jumanne ya Novemba 10, mwaka huu, kwa dhamana
ya T.sh. 500,000/- (laki tano) kwa wadhamini wawili
|
YALIYOMO
Maoni Kuvuja kwa mitihani: Tuweni wakweli kwa nchi yetu Katibu
wa Baraza Kuu azikwa Dar
Ubabe
wa madhalimu kuzimwa:
MACHO
YA SHUTUMA
Wazo
mpachiko (Programmed mind)
Ta'azia: Abbas Shaaban Kilima 1938-1998 Mdahalo
kati ya Waislamu na Wakristo- 4
Siri
ya Miujiza
Umuhimu
wa Elimu ya Awali kwa watoto wadogo
Ifahamu
Madrasat Ghazal Muslim - Moro
Pamoja
na sala, tusimamishe zakah
Aina
za maudhi yaliyoharamishwa juu ya Muislamu
Israi
na Miiraji ni miujiza
Pamoja
na ahadi ya Serikali kuzifuta: kesi za mihadhara zaendelea mahakamani
Waislamu Uluguruni Moro wazama kwenye matambiko Imarisheni
miradi ya elimu - Prof. Mikidadi
Teknologia:
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (5)
Mafunzo
ya Qur'an
Chakula
na lishe
|