|
|
|
NDUGU Waislamu na wananchi kwa ujumla, mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 3 Juni, 1998, BARAZA KUU LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU TANZANIA (BARAZA KUU) lililalamikia Serikali juu ya uundaji wa BODI ZA PAROLE ambazo zote zilikuwa zikiongozwa na Wakristo watupu na hasa Wakatoliki, hakukuwa na uwiano wa uwakilishi wa Waislamu na Wakristo. ALHAMDULILLAH, Rais alisikia kilio chetu na ilipofika tarehe 6 Juni, 1998 alizivunja Bodi hizo, na akamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani aunde Bodi mpya akizingatia uwiano wa Dini. Mpaka sasa ni miezi minne BODI hizi hazijaundwa bado. Hivi karibuni katika Gazeti la RAI toleo Na. 258 la Alhamisi Oktoba 1 – Oktoba 10, 1998 lilitufahamisha kuwa kuna ugumu katika uundaji wa BODI ZA PAROLE kwa misingi ya uwiano wa kidini; kwa sababu muundo wake unafuata sheria ya mwaka 1994, na wajumbe wake asilimia 50 ni watu wanaoingia kwa nyadhifa zao; ambapo wote, wenye nyadhifa hizo ni Wakristo. BARAZA KUU LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU TANZANIA (BARAZA KUU) lilipo ilalamikia serikali nia yake ilikuwa kuondosha udini ambao tayari umejitokeza katika uundaji wa Bodi hizo, kwanini kuwepo wawakilishi wa dini moja tu, ya Wakristo tena Wakatoliki tu. Je, Waislamu hawapo ? Kama Bodi hizi wangekuwa Waislamu pekee – je, Wakristo wangeridhika. Ikiwa wajumbe wanaingia katika Bodi hizo kwa mujibu wa nyadhifa zao sawa tunakubali na wala hatutaki hiyo sheria ibadilishwe; lakini suala la kujiuliza ni kwamba imekuwaje nyadhifa hizo zote zishikwe na Wakristo watupu tena Wakatoliki. Ina maana Waislamu hakuna wenye sifa ya kushika nyadhifa hizo ? BARAZA KUU linakataa kata kata si kweli kwamba hakuna Waislamu wenye sifa za kushika nyadhifa hizo ; baada ya miaka 37, ya UHURU na miaka 27 ya ELIMU YA UPE haiwezekani hata kidogo. Waislamu wapo wenye sifa za kushika nyadhifa hizo. Lakini hili limeandaliwa maksudi ili kuwazuia na kuwanyima Waislamu haki yao ya kikatiba kushiriki katika maongozi ya nchi hii (Soma kitabu cha Sivalon utaelewa zaidi). Gazeti linatufahamisha kuwa kuna ugumu katika uundaji wa BODI hizi, BARAZA KUUlinaitaka serikali itamke wazi wazi kama kuna ugumu na ugumu uko namna gani ? Isikae kimya ili tuweze kuisaidia, kuikwamua. Pia itueleze sifa zinazotakiwa kuingia katika ujumbe wa hizi PAROLE kisha tuangalie je, Waislamu hawana sifa hizo kweli. Kama sababu ya nyadhifa – wajumbe wanaoingia kwa nyadhifa zao; ni Wakristo Basi serikali ichukue hatua za kuwaondoa katika nyadhifa hizo ili zishikwe na Waislamu wanaostahili na waweze kuingia hizo BODI ZA PAROLE. Je, Maaskofu nao waliingia vipi katika ujumbe wa PAROLE ukiachilia mbali wale waliongia kwa nyadhifa zao. Gazeti linamkosoa Rais kwa kusema kuwa amefanya haraka kuvunja PAROLE zilizojaa Wakristo, eti angefanya uchunguzi kwanza. Na wanasheria nao wanatia maoni kuwa kutakuwa na utata kuunda Bodi hizo kwa Uwiano wa kidini – BARAZA KUU lina wauliza – Gazeti la RAI pamoja na hao wanasheria, mlikatae Rais, achunguze nini – Wakati jambo liko wazi kuwa Bodi hizo wamejaa Wakristo. Badala wao wanasheria pamoja na hili gazeti la RAI- wangekuwa wa kweli wangeihoji serikali imekuwaje vyeo vyote hivyo kushikwa na Wakristo ? Badala ya kutoa lawama kwa hatua aliyoichukua Rais. Sisi BARAZA KUU tunampongeza Rais kwa hatua aliyoichunguza. Tuna jua kuwa hili gazeti la RAI pamoja na hao wanasheria wako katika njama na kampeni ya kumzuia Rais asichukue hatua kama hizi za kufuta ubaguzi wa kidini uliopo katika Taasisi mbalimbali serikalini na katika mashirika ya umma. Njama za kuwazuia Waislamu wasishike nyadhifa mbalimbali – kuna kamati kadhaa zimetawaliwa na udini kwa mfano UTUMISHI (Central Establishment) Wakurugenzi wake wote ni Wakristo watupu; Tume ya Jiji, Tume ya Uchaguzi kwa kutaja chache tu. BARAZA KUU litaendelea kufichua huu udini uliopo serikalini kutoka katika kila sekta ili kuhakikisha unapatikana uwiano ulio sawa. Muislamu akidai haki yake anaambiwa ana udini. Kwa hiyo BARAZA KUUlinaitaka Serikali ichukue hatua za haraka kuunda Bodi hizi za PAROLE ili wananchi wafaidike na huduma hii muhimu kwa jamii. Maana ni miezi minne sasa tangu kuvunjwa, na kama kuna ugumu serikali itangaze na kueleza wazi wazi, wapi walikokwamia. Katibu Mkuu wa BARAZA KUU alizungumza na Mheshmiwa Ali Ameir Mohamed Waziri wa Mambo ya Ndani kuhusu kuundwa kwa Bodi hizo siku ya Jumatatu tarehe 12/10/1998 kwa njia ya simu. Waziri alijibu bado wako katika hatua ya kuunda Bodi hizo. BARAZA KUU liko tayari kuisaidia serikali katika uundaji wa Bodi hizo kwa kutoa majina ya wajumbe wa Kiislamu wanaostahiki kuingia kila mkoa mpaka ngazi ya Taifa tupewe idhini na tutaifanya kazi hiyo kwa kipindi kifupi tu. |
YALIYOMO
Wanawake Dodoma wataka mtoto aliyepigwa risasi akatibiwe nje Kesi za Mwembechai zaanza kusikilizwa Dondoo za saikolojia: Tuonavyo mambo Waraka wa Baraza Kuu kuhusu Parole Inawezekana kufanyika mdahalo kati
ya Waislamu na wasio Waislamu?
Teknologia
Serikali ihamie Dodoma kwanza !
Mahafali ya AMSIR Iringa
Bihawana Sekondari wafungua Ijumaa Vijana Shinyanga watakiwa
kuwa mfano mwema
Vyeo visiwasahaulishe majukumu
yenu- Sheikh Abri
Jiandaeni na kifo – Sheikh
Abdallah
Semina zawazindua wanawake
Bukoba
Waislamu wanaomaliza Kidato
cha Nne Tanga waaswa
Ndugu Kamuhabwa ndiye mwenye
chuki na AN-NUUR
'Ukombozi wa mwanamke si kugeuzwa
biashara huria'
Polisi walinda amani katika
muhadhara wa Wakristo
Mazengo wapewa uwanja wa
kujenga Msikiti
'Ajiengua Chuoni Z'bar kwa
kutoruhusiwa kuvaa hijab'
Shairi
|