AN-NUUR 
Na.172 Rajab 1419, Oktoba 23 - 29, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
Mazengo wapewa uwanja wa kujenga Msikiti
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

UONGOZI wa shule ya sekondari ya Mazengo umetoa uwanja kwa vijana (wanafunzi) wa Kiislamu kujenga Msikiti katika eneo la shule. 

Akithibitisha taarifa hii, mwalimu mlezi wa vijana wa Kiislamu Bw. Lwamo alisema ni muda mrefu sana tangu uongozi kuwapatia uwanja huu kilichokwamisha ni uwezo mdogo na ubadilishaji wa uongozi kila mwaka. Hata hivyo akasema kwamba kwa sasa ramani ya jengo la Msikiti inachorwa. 

Katibu wa Vijana wa Kiislamu tawi la Mazengo, Ustaadh Kamana alisema amepatikana mfadhili wa kuchora ramani hiyo na wakati huu umewekwa utaratibu wa kupata fedha kwa kuchangishana. 

Awali shule ya Mazengo ilitoa jengo moja lililopo kando ya uwanja wa mpira ambalo ni jukwaa la michezo chini ya jengo hilo vipo vyumba viwili, hivyo uongozi ulitoa chumba kimoja iwe sehemu ya kusalia, chumba hicho kinaweza kusaliwa na watu wasiozidi arobaini. 

Ustaadh Kamana amewaomba wazazi, walezi na Waislamu kwa ujumla waelekeze sadaka zao katika ujenzi wa Msikiti huo. 


‘Ajiengua Chuoni Z’bar kwa kutoruhusiwa kuvaa hijab’
Na Seif Hamad Suleiman, Zanzibar

MWANAFUNZI mmoja wa Chuo cha Afya Bweni ameamua kabisa kutojiunga katika chuo cha Afya kwa madai ya kwamba hawezi kabisa kutembea kichwa wazi bila ya kuvaa hijabu wakati anapokuwa masomoni. 

Mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa) alichukua hatua hiyo baada ya kutolewa tangazo rasmi na uongozi wa chuo hicho cha Afya Bweni. 

"Hii ni sheria ya Chuo, na vile vile ni alama ya kuwatambua madaktari kwa hivyo hairuhusiwi kwa mwanafunzi yoyote kuvaa hijaabu wakati akiwepo chuoni na hususani akiwemo darasani; isipokuwa kuvaa kijialama kidogo kwenye kichwa ambacho kitakuwa ni kama utambulisho kwa wanafunzi wanaosomea udaktari na sio kuvaa hijabu kichwa kizima, sheria hiyo ipo zamani chuoni na sio kwamba imeanza leo au jana". 

Mwandishi wa habari hizi alipojaribu kuzungumza na mwanamke huyo alimwambia ya kwamba Hijabu ni miongoni mwa sheria muhimu katika dini ya Kiislamu na ni vazi ambalo humpatia heshima kubwa mwanamke wakati anapovaa. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 

 
TAHARIRI 
Kuangukia makaa hakuna nafuu kwa aliye kikaangoni 

Wanawake Dodoma wataka mtoto aliyepigwa risasi akatibiwe nje 

Kesi za Mwembechai zaanza kusikilizwa 

Fitna ya Bakwata 

Dondoo za saikolojia: Tuonavyo mambo 

Waraka wa Baraza Kuu kuhusu Parole 

Inawezekana kufanyika mdahalo kati ya Waislamu na wasio Waislamu? 
Na Nandenga wa Mkomidachi 

Teknologia 
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (2) 
Na Hassan Omar 

Serikali ihamie Dodoma kwanza ! 
Na. Said Rajab 

Mahafali ya AMSIR Iringa 
Na Mwandishi Wetu 

Madrasatul Nnajjary Islamiya 

Ijue Madrasatul Riyaadh 

Bihawana Sekondari wafungua Ijumaa 

Vijana Shinyanga watakiwa kuwa mfano mwema 
Na Jihad R. Saballa, Shinyanga 

Vyeo visiwasahaulishe majukumu yenu- Sheikh Abri 
Na Mwandishi Wetu, Iringa 

Jiandaeni na kifo – Sheikh Abdallah 
Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

Semina zawazindua wanawake Bukoba 
Na Nadhiru Ishengoma 

Waislamu wanaomaliza Kidato cha Nne Tanga waaswa 
Na Ibn Mohamed 

Ndugu Kamuhabwa ndiye mwenye chuki na AN-NUUR 
Mwandishi: Maalim Bassalah 

'Ukombozi wa mwanamke si kugeuzwa biashara huria' 
Na Japhary Lemah, Arusha 

Polisi walinda amani katika muhadhara wa Wakristo 
Na Badru Kimwaga 

Mazengo wapewa uwanja wa kujenga Msikiti 
Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

'Ajiengua Chuoni Z'bar kwa kutoruhusiwa kuvaa hijab' 
Na Seif Hamad Suleiman, Zanzibar 

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Shairi 
Simlazimishe Yesu ukombozi wa ulimwengu (jibu) 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita