|
|
| Kesi
za Mwembechai zaanza kusikilizwa
KESI za watuhumiwa wa kadhia ya Mwembechai pamoja na zile za nyuma za ‘mihadhara ya kashfa’ zimeanza kusikilizwa Jijini Dar es Salaam chini ya mahakimu watano tofauti. Kesi hizo ni kesi ya jinai No. 1345 ya 1997 yenye washitakiwa 6, kesi Na. 1383 ya 1997 yenye washitakiwa sita na kesi Na. 184 ya 1998, yenye washitakiwa 11. Nyingine ni kesi Na. 192 ya 1998 yenye watuhumiwa 12 na Kesi Na. 407 ya 1998 yenye wahitakiwa 10. Kesi Na. 1345 inaanza kusikilizwa Oktoba 23 ambapo watuhumiwa wanashitakiwa kwa kusema maneno yenye kudhuru hisia za kidini (kiimani). Walio katika kesi hii ni Swalehe Rashid, Ramadhani Mwakwangu, Ally Majapa na Uliza Rashid. Wengine ni Ally Athumani na Ramadhani Hamisi. Kesi Na. 1383 (1997) imeanza kusikilizwa Oktoba 2, na itaendelea Novemba 10, katika kesi hii Waislamu sita wanashitakiwa kuharibu kituo kidogo cha Polisi pamoja na vifaa vyake huko Mwananyamala. Walio katika kesi hii ni Uliza Rashid; Ally Athuman, Ramadhani Hamisi na Ally Majapa. Wengine ni Hamisi Swalehe na Magezi Shaaban. Kesi Na. 184 (1998) imeanza kusikilizwa na itaendelea tena Novemba 13. Katika kesi hii watuhumiwa wanashitakiwa kwakufanya ghasia (Mwembechai); kufanya ghasia baada ya onyo la Polisi na kumjeruhi askari (Simon Nyakoro). Walio katika kesi hii ni Hatamu Sudi, Hamidu Mohamed, Hussein Mohamed, Ally Kassim na Kivuele Mawazo Abadallah. Wengine ni Abdallah Juma Bakari, Rashid Mohamed na Kombo Hassan. Aidha, wapo Hemedi Ramadhani, Hamza Amani Ally na Abdurahaman Juma Saidi. Walio katika kesi Na. 192 (1998) ni Mwalimu Ramadhani, Hamad Salum, Yusuf Salum, Hassan Utyani, Gaudence Gervas na Omar Hassan. Wenginen i Kassim Ally, Abdallah Sufian, Richard Kobello, Saidi Rashid na Bernard Augustino. Hawa kwa pamoja wanashitakiwa kwa uharibifu wa mali kwa nia mbaya (gari; bendera); kuvun ja nyumba na kuiba; kufanya ghasia baada ya onyo na kumjeruhi askari. Katika kesi Na. 407 (1998) wapo Rutemba Shabani, Iddi Selemani Makota;
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Wanawake Dodoma wataka mtoto aliyepigwa risasi akatibiwe nje Kesi za Mwembechai zaanza kusikilizwa Dondoo za saikolojia: Tuonavyo mambo Waraka wa Baraza Kuu kuhusu Parole Inawezekana kufanyika mdahalo kati
ya Waislamu na wasio Waislamu?
Teknologia
Serikali ihamie Dodoma kwanza !
Mahafali ya AMSIR Iringa
Bihawana Sekondari wafungua Ijumaa Vijana Shinyanga watakiwa
kuwa mfano mwema
Vyeo visiwasahaulishe majukumu
yenu- Sheikh Abri
Jiandaeni na kifo – Sheikh
Abdallah
Semina zawazindua wanawake
Bukoba
Waislamu wanaomaliza Kidato
cha Nne Tanga waaswa
Ndugu Kamuhabwa ndiye mwenye
chuki na AN-NUUR
'Ukombozi wa mwanamke si kugeuzwa
biashara huria'
Polisi walinda amani katika
muhadhara wa Wakristo
Mazengo wapewa uwanja wa
kujenga Msikiti
'Ajiengua Chuoni Z'bar kwa
kutoruhusiwa kuvaa hijab'
Shairi
|