|
|
|
MADRASATUL Nnajjary Islamiya ipo nyumbani kwa mlezi wa madrasa hiyo Mzee Abbasi Hamza Masoud, Mwananyamala kwa Kopa Jijini Dar es Salaam. Madrasa hii ni maarufu kwa wakazi wa maeneo hayo kutokana na kazi nzuri inayofanywa na walimu ya kuwafundisha wanafunzi wa Kiislamu dini yao. Madrasa hii ilianzishwa na mlezi huyo wa madrasa Abbasi Hamza Masoud mnamo mwaka 1963 ikiwa na wanafunzi wasiopungua 15, wasichana kwa wavulana. Kwa kipindi hicho Ustaadh Abbas alifanya kazi kubwa sana ambapo wanafunzi walikuwa wakiongezeka siku hadi siku. Mpaka hivi sasa wapo wanafunzi 125 wasichana kwa wavulana, masomo yanayotolewa madrasani hapo ni Fiqh, Tawheed, Sira, Hadithi, Tafsiri ya Qur’an, Hifadhi ya Qur’an na Qur’an kwa njia ya Tajwidi. Kwa sasa madrasa hii ipo chini ya usimamizi wa Ustaadh Ahmad Issa, Zuberi Issa, Khalid Abbas na Zuberi Ramadhani. Upo utaratibu ambao umewekwa na walimu kwa kila mzazi kulipa shilingi 100 kwa kila baada ya mwezi ili kuweza kuwasaidia walimu pesa za matumizi yao binafsi. Hata hivyo walimu hao wamesema wazazi wa wanafunzi wamekuwa wagumu kutoa pesa hizo bila ya kujali kwamba nao wanahitaji kuishi na kujikimu katika mambo mbalimbali. Madrasa Nnajjary inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa vifaa vya kufundishia pamoja na vikalio kama vile mikeka, majamvi na hata magunia na pia hulazimika walimu pamoja na wanafunzi kukaa sehemu ambayo haina mikeka. Madrasa hii ina sehemu yake ya kujitegemea na ipo katika mikakati ya kukifanyia chuo ukarabati wa kutosha kwa sababu hakipo katika hali ya kimadrasa. Hivyo, wito umetolewa kwa Waislamu wote wajitokeze kwa wingi kutoa sadaka zao za hali na mali ili kufanikisha mikakati hiyo. KWA wakazi waishio Unga Limited na Daraja II katika manispaa ya mji wa Arusha, Madrasatul Riyadh sio ngeni kwao. Na kwa wale wasioijua madrasa hiyo ipo mtaa wa Jamhuri kata ya Daraja II wilaya ya Arusha mjini. Madrasa hii ilianzishwa mnamo mwaka 1989 na mwalimu Sulemain bin Yahya wakati huo alkuwa anafundisha madrasa iliyokuwa nyumbani kwa marehemu Sheikh Othumani bin Munga hapo Unga Limited. Sambamba nae alikuwa ni Maalim Issa bin Abubakar kwa pamoja wakatoa fikra ya kufungua darsa katika mtaa wa Jamhuri ili Waislamu wa maeneo hayo wapate kujifunza dini ya Allah (sw) kwa ukaribu zaidi. Ndipo lilipofunguliwa darsa na walipatikana wanafunzi wasiopungua 50 waliokuwa wakisomea katika majengo ya ofisi za CCM mtaaani hapo. Baada ya miezi miwili alipatikana maalim mwingine kwa jina ni Issa bin Ally ambaye pia ni kiongozi wa Waislamu katika mas-ala ya dini mtaani hapo. Uongozi aliopewa na Waislamu hivi karibuni na walishirikiana katika kazi hiyo hadi walipohamia sehemu rasmi mwaka 1993. Ilipotimu mwaka 1995 Allah (sw) alijalia madrasa neema ya kupata waalimu wawili zaidi, ambao ni maalim Suleiman Said Ilungulu na maalim Ayoub Abdallah Mwenda ambaye kwa sasa marehemu pia alikuwa Mudir wa madrasa hiyo. Wakati huo idadi ya wanafunzi iliongezeka hadi kufikia wanafunzi wasiopungua mia mbili, ambao walitenganishwa katika makundi matatu, kundi la kwanza ni kwa wanaoanzia kujifunza Qur’an la pili ni wale walio katika juzuu ama pia wanachanganyiwa masomo mengine kama Fiqhi, Lugha, Siratu-Nabawiyah na Hadithi za Mtume (s.a.w). Na kundi la tatu ni kwa waliomaliza juzuu ama na hufundishwa na masomo kama Ataj-wed, Siratu-Nabawiyah, Nahau, Fiqhi na kuhifadhi Qur’an na Hadithi za Mtume (s.a.w). Mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa madrasa hiyo ni ya kuridhisha, kwani imeweza kutoa wanafunzi wengi waliojiunga na madrasa nyingine hapa mkoani kwa mafunzo ya juu zaidi baada ya kufanya mtihani . Walimu kwa kushirikiana na wazazi wa wanafunzi wameanzisha mashindano yanayofanyika kila mwisho wa mwaka ambayo hujumuisha wazazi kama watathmini kwa yale watoto wao waliyojifunza. Kwa wale watakaofanya vizuri hupewa zawadi maalumu iliyoandaliwa na wazazi kama pongezi. Pia madrasa hiyo imeanzisha darsa maalum kwa ajili ya watu wazima wakina mama ambalo huanza baada ya Salatil Dhuhur na darsa la akina baba linaloanza baada ya Salatil Magharibi na kuisha Isha. Matatizo yanayoikabili madrasa hiyo ni pamoja na upungufu wa vitendea
kazi kwa ujumla. Hivyo wanatoa wito kwa taasisi mbalimbali na watu binafsi
pote nchini kutoa misaada yao kadri ya Allah (sw) atakavyowajaalia.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Wanawake Dodoma wataka mtoto aliyepigwa risasi akatibiwe nje Kesi za Mwembechai zaanza kusikilizwa Dondoo za saikolojia: Tuonavyo mambo Waraka wa Baraza Kuu kuhusu Parole Inawezekana kufanyika mdahalo kati
ya Waislamu na wasio Waislamu?
Teknologia
Serikali ihamie Dodoma kwanza !
Mahafali ya AMSIR Iringa
Bihawana Sekondari wafungua Ijumaa Vijana Shinyanga watakiwa
kuwa mfano mwema
Vyeo visiwasahaulishe majukumu
yenu- Sheikh Abri
Jiandaeni na kifo – Sheikh
Abdallah
Semina zawazindua wanawake
Bukoba
Waislamu wanaomaliza Kidato
cha Nne Tanga waaswa
Ndugu Kamuhabwa ndiye mwenye
chuki na AN-NUUR
'Ukombozi wa mwanamke si kugeuzwa
biashara huria'
Polisi walinda amani katika
muhadhara wa Wakristo
Mazengo wapewa uwanja wa
kujenga Msikiti
'Ajiengua Chuoni Z'bar kwa
kutoruhusiwa kuvaa hijab'
Shairi
|