|
|
|
JUMUIYA ya Wanafunzi, Waalimu na Wafanyakazi wa shule ya Sekondari Bihawana wameanza kuswali Ijumaa shuleni hapo Oktoba 16, mwaka huu. Akiongea na mwandishi wa habari hizi, Mwalimu Mlezi wa Wanafunzi Waislamu Mwalimu Mwinjuma alisema kwamba kufunguliwa kwa Ijumaa hiyo kutawapunguzia wanafunzi safari ndefu kufuata Msikiti wa Ijumaa. Aidha, kutawaokoa kutokana na kupoteza vipindi zaidi ya vitatu kila wiki. Akisoma Khutba katika Ijumaa hiyo ya kwanza, Ustaadh Ramadhani ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo amewausia wanafunzi washikamane na tabia njema kama zinavyofafanuliwa na Uislamu. Aidha. aliwataka wasome kwa bidii ili waweze kutekeleza vyema wajibu wao wa Ukhalifa. Wakati huo huo, wanafujzi wa Bihawana wamehimizwa kushikamana na mafunzo ya Qur’an na Sunnah kwani ndio njia pekee ya kufaulu hapa duniani na akhera. Aidha, amewahimiza wanafunzi kufanya juhudi katika elimu kwani ndio amri ya kwanza na njia pekee ya kujipatia maendeleo. Akitoa nasaha zake katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne, Sheikh Abdallah aliwatahadharisha vijana kutokana na tabia za Kimagharibi zinazokwenda kinyume na Uislamu. Aidha aliwaonya wasiige tabia za kihuni kama vile kuvaa hereni, mikufu kwa wanamume, mambo ambayo yamelaaniwa katika Uislamu. Naye Sheikh Abdallah Ali wa Masjid Quba ameahidi kutuma wanafunzi wake kuendesha ibada hiyo. Pamoja ahadi hiyo, Sheikh Abdallah ameahidi kutoa vitabu vya dini pamoja na miswala kwa ajili ya msikiti huo. VIJANA wametakiwa kuwa mfano mwema kimaadili, kujielimisha zaidi, kujitolea mhanga kupigania dini yao na kuishi Kiislamu. Ujumbe huo ulitolewa hivi karibuni na Amiri Mkuu wa Bodi ya maendeleo ya Waislamu Shinyanga, Ustaadh Mohammed Issa katika hafla ya kuwaaga vijana Waislamu wa shule ya sekondari Uhuru iliyofanyika shuleni hapo. Katika ujumbe wake huo, Ustaadh Mohammed aliwakumbusha vijana hao kuwa wao ni wawakilishi wa vijana wenzao ambao hawakubahatika kupata elimu waliyoipata wao hivyo wana deni kubwa la kuonyesha shukrani zao kwa Allah (sw) kwa kutumia vyema elimu waliyoipata kwa ajili ya manufaa ya wenzao na kwa dini yao kwa ujumla. Vijana hao walikumbushwa pia kuwa mwisho wa jambo moja ndiyo mwanzo wa jingine, hivyo katu wasiridhike na kiwango cha elimu walichopata bali wajiendeleze zaidi katika viwango vya juu ili waweze kunufaika wao na kuunufaisha Uislamu kwa ujumla. Kuhusu suala la uvaaji Hijaab, Ustaadh Mohammed aliwasisitiza mabinti wa Kiislamu kuvaa vazi hilo, kulipenda na kujifakharisha nalo. Alisema ni aibu na jambo la kushangaza sana kuona hadi leo hii bado mabinti wa Kiislamu hawataki kutekeleza amri hiyo ya Mola wao aliyewaumba pamoja na kuondolewa khofu kwa wizara husika kuruhusu uvaaji vazi hilo. Kilichosisimua zaidi katika suala la hijaab ni pale aliposimama Mwalimu Masanja kutoa nasaha zake kwa vijana hao. Mwalimu Masanja ni mwalimu wa shule hiyo na katika nasaha zake hizo Mwalimu aliwasisitiza wanafunzi wake kuvaa vazi hilo kwa kuliita la heshima, linapendeza, na ngao ya mambo maovu. "Qur’an yenu na Hadith za Mtume (s.a.w) vinawaamrisha hivyo, Wizara ya Elimu ilisharuhusu vazi hili, sasa basi kwa nini hamtaki kuvaa ? Mna tatizo gani ?", aliuliza Mwalimu huyo na ambaye si Muislamu kwa mshangao na masikitiko makubwa. Kwa kauli hiyo ya Mwalimu Masanja walisikika baadhi ya wageni waalikwa wakisema, ikiwa hata wasio Waislamu wamechukua dhamana ya kutufikishia ujumbe wa kutekeleza dini yetu basi hatutokuwa tena na udhuru wowote mbele ya Allah (sw). Hadi sasa ni mabinti wanne tu shuleni hapo ambao wamekuwa wakivaa hijaab na watatu kati yao wanatarajia kumaliza shule mwaka huu. Umetolewa wito kumpa moyo na kumwombea dua binti pekee anayebakia akivaa hijaab shuleni hapo ili asikate tamaa kwa kuona kabaki yeye peke yake avaaye vazi hilo, na hasa ukizingatia mazingira yetu yalivyo sasa hivi. Vijana wa Kiislamu wanaotarajia kumaliza masomo yao mwaka huu shuleni hapo ni kumi na wawili (12) kati ya jumla ya wanafunzi themanini na wanne (84). |
YALIYOMO
TAHARIRI
Wanawake Dodoma wataka mtoto aliyepigwa risasi akatibiwe nje Kesi za Mwembechai zaanza kusikilizwa Dondoo za saikolojia: Tuonavyo mambo Waraka wa Baraza Kuu kuhusu Parole Inawezekana kufanyika mdahalo kati
ya Waislamu na wasio Waislamu?
Teknologia
Serikali ihamie Dodoma kwanza !
Mahafali ya AMSIR Iringa
Bihawana Sekondari wafungua Ijumaa Vijana Shinyanga watakiwa
kuwa mfano mwema
Vyeo visiwasahaulishe majukumu
yenu- Sheikh Abri
Jiandaeni na kifo – Sheikh
Abdallah
Semina zawazindua wanawake
Bukoba
Waislamu wanaomaliza Kidato
cha Nne Tanga waaswa
Ndugu Kamuhabwa ndiye mwenye
chuki na AN-NUUR
'Ukombozi wa mwanamke si kugeuzwa
biashara huria'
Polisi walinda amani katika
muhadhara wa Wakristo
Mazengo wapewa uwanja wa
kujenga Msikiti
'Ajiengua Chuoni Z'bar kwa
kutoruhusiwa kuvaa hijab'
Shairi
|