AN-NUUR
Na.167 Jamadul Awal 1419, Septembe 17 - 24, 1998

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita

 

Chakula na lishe

Haja ya maji ya kunywa

Na Mujahiid Mwinyimvua

MAJI ni moja ya virutubisho muhimu sana kwa ukuaji na maendeleo ya mwili wa mwanadamu. Katika mwili wa mwanadamu maji yana kazi nyingi, baadhi yake ni: Maji ni sehemu ya mwili wa mwanadamu na pia kazi nyingi mwilini zinafanyika katika mazingira ya umajimaji.

Mwili wa mwanadamu hupoteza maji kila siku kwa njia mbalimbali. Miongoni mwa njia hizo ni kutokwa na jasho, kupumua, kutokwa na damu, na kwenda haja ndogo na haja kubwa.

Ukizingatia umuhimu wa maji mwilini na kiasi cha maji kinachopotea kila siku katika mwili, itakubainikia wazi haja ya kunywa maji mara kwa mara.

Wataalamu wa tiba na wale wa lishe wanatuambia kuwa wasichana, wavulana na watu wazima wanywe angalau glasi nne za maji kila siku.

Kiasi hicho cha maji kisipungue, lakini kinaweza kuongezeka kwa kutegemea hali ya hewa (mfano wakati wa majira ya joto) au aina ya kazi anayofanya mtu.

Mtu mwenye kufanya kazi ngumu hupoteza maji mengi, hivyo lazima anywe maji mengi ili kuziba pengo.

Baadhi ya watu hunywa maji pale tu wanapojihisi kuwa wana kiu. Kiu ni njia ya asili inayomwezesha binadamu kunywa maji.

Hata hivyo, njia hiyo haifanyi kazi vizuri katika mazingira ya baridi. Kwa hiyo, jambo la kuzingatia ni kiwango kinachotakiwa mtu kunywa maji kila siku. Hasa katika kila mlo, mtu lazima anywe maji.

Hii ni kwa sababu kazi ya usagaji wa chakula inahitaji mazingira ya umaji maji.

Mwili wa binadamu pia hupata maji kwa njia ya chakula au vinywaji vingine zaidi ya maji. Kwa mfano matunda kama vile matikiti (Watermelon), mananasi na machungwa ni viongezo vizuri vya maji mwilini.

Vile vile maziwa, chai, uji, togwa, soda, n.k. vinaupa mwili kiasi kikubwa cha maji. Zaidi ya vyanzo hivyo, baadhi ya kazi mwilini pia huupa mwili maji.

Haja ya kunywa maji au vinywaji vingine lazima iambatane na kanuni za afya. Yaani lazima watu wanywe maji (au kinywaji kingine) yaliyo safi na salama.

Katika baadhi ya miji ya Tanzania (likiwemo Jiji la Dar es Salaam) kuna vijana wanaouza maji ya kunywa barabarani ambayo usafi na usalama una mashaka. Kwa hiyo, mwananchi ajihadhari na maji hayo.

Na kwa upande wa serikali na vyombo vyake, viheshimu Katiba ambayo inasisitiza utunzaji wa uhai wa raia

Juu 
 

YALIYOMO  
 
TAHARIRI 
Hakuna Muislamu aliyekufa kutokana na vurugu

Mgogoro wa kiwanja Duma: Wakatoliki wasema kuna njama za Waarabu Same Na Mwandishi Wetu

Wanawake wakutana Mwanza na kusema: Kunyanyaswa sasa basi
Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Sheikh Omar Bashir ataka Waislamu waimarishe mshikamano
Na Said Sharif

Ustaadhi Abdallah Mfoyi afariki
Na Muhibu Saidi

Baraza Kuu halina Katibu Nguruka - Sheikh Kilima
Na Abu Adli

Viongozi Msikiti wa Ubungo Darajani waitwa polisi
Na Kassim Juma

Marekani `ilivyosaidia' Mujahidiin

Barua ya mtoto wa miaka minne toka Lebanon kwa Bibi Hillary Clinton

Ujumbe wa waandishi kwa Bw. Batendi, Wakristo
Na Muhibu Saidi

Waislamu wanadhalilishwa au wanajidhalilisha

Tusiwe Jogoo wa Esopo na Almasi
Na MAALIM ALI BASSALEH

Sherehe za wiki ya usalama barabarani: Kauli nzito za waheshimiwa zimekalia kuti kavu
Na Said Omar

Mwanasayansi Avicenna: Tabibu bingwa.
Na Dk. A. A. Amur

Ujenzi wa Msikiti wa Ijumaa Mriti waanza
Na Nasib A. Mziray

Kutoweka kwa hazina adimu za kimazingira
Na Yassir Salim

Mfalme Najashi ni mfano bora wa kuigwa kwa watawala
Na Idi Kikong'ona

Waislamu Moro wasaidia wagonjwa
Na Mwandishi Wetu, Morogoro

KUFUATIA KUTISHIA MAGAZETI: Sheikh Ayoub amjibu Askofu Rajab Rajab
Na Mussa Ally

TAMSA Tanga waahidi kuendeleza mema
Na Ibn Mohammed, Tanga

Ufugaji, uuzaji nguruwe wakera wananchi Dar
Na Mwandishi Wetu

Mafundisho ya Quran 
Kuwepo kwa ufufuo

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Haja ya maji ya kunywa

 

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org  

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita