AN-NUUR
Na.167 Jamadul Awal 1419, Septembe 17 - 24, 1998

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita

 

Sheikh Omar Bashir ataka Waislamu waimarishe mshikamano

Na Said Sharif

SHEIKH maarufu Jijini, Sheikh Omar Bashir amewataka Waislamu wote nchini kuimarisha mshikamano kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (sw) na matukio ya kuuawa Waislamu na kuteswa ndani ya magereza yasiwe chanzo cha kurudi nyuma na kupoteza msimamo katika dini, kwa sababu hayo si mambo mageni katika historia ya Uislamu.

Amesema matukio hayo yanapotokea huwa ni uthibitisho wa kuuelekea Uislamu.

Sheikh Omar Bashir ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waislamu Septemba 11, mwaka huu baada ya swala ya Ijumaa katika Masjid Mujahiduun.

Amesisitiza kwamba Waislamu wana wajibu wa kuutangaza Uislamu na kumtakasa Mwenyezi Mungu (sw) na kazi hiyo itakuwa ni yenye mafanikio mshikamano utakapo kuwa imara.

Katika hotuba hiyo fupi, Sheikh Omar Bashir amesema kwa kufahamu hatari ya migongano katika jamii, Uislamu umeweka adhabu kali kwa yule anayebainika kuleta migongano na kufarakanisha jamii ya Kiislamu. 

Juu 
 

YALIYOMO  
 
TAHARIRI 
Hakuna Muislamu aliyekufa kutokana na vurugu

Mgogoro wa kiwanja Duma: Wakatoliki wasema kuna njama za Waarabu Same Na Mwandishi Wetu

Wanawake wakutana Mwanza na kusema: Kunyanyaswa sasa basi
Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Sheikh Omar Bashir ataka Waislamu waimarishe mshikamano
Na Said Sharif

Ustaadhi Abdallah Mfoyi afariki
Na Muhibu Saidi

Baraza Kuu halina Katibu Nguruka - Sheikh Kilima
Na Abu Adli

Viongozi Msikiti wa Ubungo Darajani waitwa polisi
Na Kassim Juma

Marekani `ilivyosaidia' Mujahidiin

Barua ya mtoto wa miaka minne toka Lebanon kwa Bibi Hillary Clinton

Ujumbe wa waandishi kwa Bw. Batendi, Wakristo
Na Muhibu Saidi

Waislamu wanadhalilishwa au wanajidhalilisha

Tusiwe Jogoo wa Esopo na Almasi
Na MAALIM ALI BASSALEH

Sherehe za wiki ya usalama barabarani: Kauli nzito za waheshimiwa zimekalia kuti kavu
Na Said Omar

Mwanasayansi Avicenna: Tabibu bingwa.
Na Dk. A. A. Amur

Ujenzi wa Msikiti wa Ijumaa Mriti waanza
Na Nasib A. Mziray

Kutoweka kwa hazina adimu za kimazingira
Na Yassir Salim

Mfalme Najashi ni mfano bora wa kuigwa kwa watawala
Na Idi Kikong'ona

Waislamu Moro wasaidia wagonjwa
Na Mwandishi Wetu, Morogoro

KUFUATIA KUTISHIA MAGAZETI: Sheikh Ayoub amjibu Askofu Rajab Rajab
Na Mussa Ally

TAMSA Tanga waahidi kuendeleza mema
Na Ibn Mohammed, Tanga

Ufugaji, uuzaji nguruwe wakera wananchi Dar
Na Mwandishi Wetu

Mafundisho ya Quran 
Kuwepo kwa ufufuo

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Haja ya maji ya kunywa

 

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org  

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita