AN-NUUR
Na.167 Jamadul Awal 1419, Septembe 17 - 24, 1998

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita

 

Waislamu wanadhalilishwa au wanajidhalilisha

NI muda mrefu sasa mada zenye kuonyesha udhalilishaji wa Waislamu zimekuwa zikijitokeza. Hasa zaidi 1998 baada ya mauaji ya Waislamu Msikiti wa Mwembechai na kukamatwa na kudhalilishwa kwa Maimamu wa Msikiti wa Mtambani na mengineyo wakiwemo Waislamu wanaume na wanawake. Maswali mengi yanaendelea kuwepo hasa kwa watu wanaopenda suluhisho la kudumu kwa masuala yanayowagusa Waislamu. Hivyo tatizo hasa ni nini. Ni nia ya makala hii kutazama kwa undani na kugusia ufumbuzi wake. Tujiulize hasa Waislamu wanadhalilishwa au wanajidhalilisha wenyewe? Mwandishi Ibn Ismail wa Arusha anaendelea zaidi...

KWA mtazamo wa haraka haraka Waislamu wanahisi wanadhalilishwa na serikali yao (ambayo wao vile vile wamehusika katika kuileta kwenye madaraka) hasa kwa mifano ya:

Ufanyaji wa propaganda zisizo sahihi kwenye masuala ya Waislamu. Mfano ni Msikiti wa Mwembechai, masuala ya nguruwe n.k.

Upendeleo ambao unawanyima haki Waislamu kwa upande wa uchaguzi wa viongozi wa kitaifa, mikoa, wilaya katika nyanja za serikali, mashirika ya umma n.k.

Kwenye upangaji wa sikukuu za kitaifa, mfano mzuri ni pale panapokuwa na dini kuu mbili katika nchi ilitegemewa kuwa siku ya Jumapili na Ijumaa zingekuwa ni siku za mapumziko kitaifa. Siku ya Ijumaa imenyimwa haki hii. Hii husababisha wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na baadhi ya wafanyakazi kukosa nafasi ya kuhudhuria ibada zao kwa wakati na matayarisho yanayostahili.

Mipango ya muda mrefu ya dira ya taifa inalenga katika kulipeleka taifa kuwa nchi ya dini moja na kuiondosha nyingine. Hii ina mifano hai kiutamaduni, elimu, sheria n.k.

Nchi imeongozwa muda mrefu sana na viongozi wa juu wa dini moja tu.

Wasio Waislamu wanaonekana kuchangia kwa udhalilishaji wa Waislamu kwa sababu kuu zifuatazo:

Kwamba wanapata misaada mingi kutoka kwenye nchi za Kikristo kwa ajili ya maendeleo yao, lakini vile vile katika kudhibiti kukua kwa Waislamu na kubadilisha desturi na mifumo ya Kiislamu.

Wamejipenyeza sana kwenye serikali na vyama kiasi ambacho wakati mwingine baadhi ya Waislamu wameshindwa kutofautisha kati ya serikali na dini fulani pale ambako kiongozi wa juu anapokuwa sio Muislamu. Nembo za dini zimetumika katika maswala haya.

Kwa sababu baadhi ya Makanisa yanaendeshwa kwa amri ya moja kwa moja kutoka Ulaya mfano wa Kanisa Katoliki na Papa wa Vatican. Hivyo baadhi ya Waislamu wanahisi kuwa wanadhalilishwa sio tu na wasio Waislamu wa ndani bali hata kutoka nje ya nchi.

Waislamu wenyewe wanaonekana kujidhalilisha wenyewe katika nyanja zifuatazo:

Wanapopata madaraka na hasa wanapohisi wamefadhiliwa na viongozi Wakristo, wanachukua nafasi hizo kulipa fadhila badala ya kuleta maendeleo yanayokusudiwa kwa nchi nzima bila kujali dini zao.

Wanapopata madaraka wanajikuta wamewekewa vizingiti vingi kiasi ambacho anapokaribia kuvuka vizingiti hivyo muda wa kuwepo madarakani unakuwa umekwisha.

Viongozi Waislamu wanapokuwa madarakani wanakuwa wao wenyewe sio waumini wa aina wanayotegemewa kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na Waislamu wenzao.

Vyombo vya Kiislamu nchini ama kwa ujinga, au kubanwa na serikali au kwa sababu za kibinafsi, vimekuwa havifanyi kazi zinazotarajiwa na Waislamu, hivyo kuonekana kama vibaraka wa vyombo vingine ambavyo sio vya Kiislamu.

Waislamu wenyewe katika hali ya mtu mmoja mmoja, vikundi na hata jumuiya zimeshindwa kutatua masuala madogo madogo yaliyopo kwenye uwezo wao. Mifano hai ni sawa na ile ya familia tatu zilizo na uwezo sawa, nafasi ya ardhi sawa, upatikanaji wa maji sawa. Lakini familia moja ikalima bustani ya mchicha na nyingine isifanye hivyo halafu familia hiyo ikaenda kuomba familia nyingine msaada wa mboga ya mchicha.

Baadhi ya Waislamu wamepandikiziwa hisia kuwa kujadili masuala ya Uislamu yanapoingiliana na serikali au dini nyingine ni kama kosa kubwa na nyeti sana. Wengine hupata hofu hata kutaka kukimbia. Na mara nyingi hawa ndio wanaopewa au wanatakiwa kuwa viongozi wa Waislamu

Juu 
 

YALIYOMO  
 
TAHARIRI 
Hakuna Muislamu aliyekufa kutokana na vurugu

Mgogoro wa kiwanja Duma: Wakatoliki wasema kuna njama za Waarabu Same Na Mwandishi Wetu

Wanawake wakutana Mwanza na kusema: Kunyanyaswa sasa basi
Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Sheikh Omar Bashir ataka Waislamu waimarishe mshikamano
Na Said Sharif

Ustaadhi Abdallah Mfoyi afariki
Na Muhibu Saidi

Baraza Kuu halina Katibu Nguruka - Sheikh Kilima
Na Abu Adli

Viongozi Msikiti wa Ubungo Darajani waitwa polisi
Na Kassim Juma

Marekani `ilivyosaidia' Mujahidiin

Barua ya mtoto wa miaka minne toka Lebanon kwa Bibi Hillary Clinton

Ujumbe wa waandishi kwa Bw. Batendi, Wakristo
Na Muhibu Saidi

Waislamu wanadhalilishwa au wanajidhalilisha

Tusiwe Jogoo wa Esopo na Almasi
Na MAALIM ALI BASSALEH

Sherehe za wiki ya usalama barabarani: Kauli nzito za waheshimiwa zimekalia kuti kavu
Na Said Omar

Mwanasayansi Avicenna: Tabibu bingwa.
Na Dk. A. A. Amur

Ujenzi wa Msikiti wa Ijumaa Mriti waanza
Na Nasib A. Mziray

Kutoweka kwa hazina adimu za kimazingira
Na Yassir Salim

Mfalme Najashi ni mfano bora wa kuigwa kwa watawala
Na Idi Kikong'ona

Waislamu Moro wasaidia wagonjwa
Na Mwandishi Wetu, Morogoro

KUFUATIA KUTISHIA MAGAZETI: Sheikh Ayoub amjibu Askofu Rajab Rajab
Na Mussa Ally

TAMSA Tanga waahidi kuendeleza mema
Na Ibn Mohammed, Tanga

Ufugaji, uuzaji nguruwe wakera wananchi Dar
Na Mwandishi Wetu

Mafundisho ya Quran 
Kuwepo kwa ufufuo

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Haja ya maji ya kunywa

 

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org  

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita