|
|
| Sherehe za
wiki ya usalama barabarani:
Kauli nzito za waheshimiwa zimekalia kuti kavu Na Said Omar MATAMSHI mbalimbali yaliyotolewa na waheshimiwa wenye nyadhifa mbalimbali katika kuadhimisha "wiki ya usalama barabarani" wiki hii yafaa Watanzania wote tuyaenzi. Lakini Wengine wameasa kuwa sheria za matumizi ya barabara ni lazima na muhimu kuzingatiwa na watembeao kwa miguu hadi waendeshao vipando vikubwa vikubwa. Hili ni muhimu kwani ni mara nyingi sana waendao kwa miguu wamekuwa ni vyanzo vya ajali mbaya sana barabarani. Nasaha zingine zimegusa suala zima la umakini katika utoaji wa leseni, maadili ya udereva, maadili ya uaskari katika kusimamia sheria za barabarani n.k. Yote haya ni mazito kulingana na ufafanuzi uliotolewa na wasemaji wetu wakuu. Katika mazungumzo baada ya habari asubuhi ya Septemba 9, 1998, RTD wanasema kuwa ajali nyingi na mabaya zinazotokea barabarani zinaua au kumaliza watu kama magonjwa ya Ukimwi, malaria n.k. yanavyomaliza watu. Yote haya mimi nasema ni muafaka kabisa. Kama wasemaji walivyoainisha sababu kubwa zinazosababisha ajali ni kule kutozingatia sheria za barabarani kwa watumiaji wote wa barabara, mwendo kasi wa madereva na kubwa zaidi ulevi wa madereva. RTD wanaendelea kusema kuwa "Pamoja na sheria ya kuwa dereva asiendeshe gari hali ya kuwa amelewa, ndio kwanza kabla dereva hajaanza safari, atapata "Safari" zake tisa, zikishakaa kichwani anakali usukani". Pia wanaendelea kusema kuwa amepatikana Musa akaja na fikra ya magari yafungwe gavana. Mimi ninasisitiza kuwa Musa aliyepatikana akataka magari yafungwe vidhibiti mwendo(Gavana) anafaa kupongezwa. Ajabu ni kuwa badala ya kupungua kwa ajali ndio kwanza zimeshamiri. Lakini ni kwa nini? Ni bayana kuwa vishawishi vya kwenda kasi havijadhibitiwa miongoni mwao ikiwa ni ule unaolazimishwa kuwa urithi wa watanzania, "Safari". Tusidhani kuwa tunaweza kuondoa tatizo hili kwa kutamani tu, lazima tuwe tayari kuvitoa muhanga tuvipendavyo ili zoezi la Musa lifanikiwe Tusisahau kuwa wana wa Israil baada ya kuishi jangwani wakifafadhiliwa na Mwenyezi Mungu kwa Manna na Sal'wa , tamaa mbaya iliyosukumwa na matashi ya nafsi zao na kibri walimtaka Musa amuombe Mola wake awatolee vile vinavyooteshwa katika ardhi kama mboga zake, matango, thaumu na adesi zake na vutunguu vyake. Ndipo Allah akawauliza " Mnabadilisha vitu duni kwa vile vilvyobora? Na ikapigwa juu yao chapa ya dhila na umaskini na wakastahiki ghadhabu za (2:6). Hivi leo tunamtamani Musa atakayetanczua tatizo hili wakati huo huo hatuko tayari kuyafuata maelekezo yake kwani yatuondoa katika yale yanayotamaniwa sana na nafsi zetu. Tuna haja gani ya kujisumbua? Suala la kujiuliza ni kuwa; je, maneno yatangazwayo na RTD kila moja linajitegemea au yanategemeana? Ni siku chache zilizopita tulikuwa tukishawishiwa na Radio hii hii kuwa tununue hisa katika kampuni ya kutengeneza Safari . Si hivyo tu bali mara kwa mara tunaambiwa huu ndio urithi wetu. Vile vile tunaambiwa ni namna pekee ya kujipatia nguvu na kuondoa machovu tukitumia Safari au Kilimanjaro bia ya Mtanzania. Tunamlaumu nini anayeipata Safari kabla ya safari? Anatumia urithi, anatumia alichokizalisha, maana na yeye anahisa, anahitaji nguvu na kujiondoshea machovu kabla ya safari, kwanini asipate Safari. Askari wa usalama barabarani anahitaji Safari ili afanye kazi yake. Akizingatia maadili ya kazi yake hatapata Safari . Mtoaji wa leseni za udereva halikadhalika. Aliyepata Safari na akatembea kwa mguu hujiona mfalme na kuyumba barabara nzima. Aliyepata Safari akikaa kwenye usukani mwendokasi KM 120 kwa saa huona kama anacheza. Niambie watakapokutaka wenye Safari za vichwani mmoja juu ya kipando na mwingine akitembea kwa mguu safari zao vipi. Kwa msingi huu, mimi naona kuwa nasaha za waheshimiwa wote zemeketishwa kwenye kuti kavu kwani mzizi wa tatizo hauguswi ila lawama zinatolewa kuwa kwanini majani hayakauki. |
YALIYOMO
TAHARIRI Hakuna Muislamu aliyekufa kutokana na vurugu Mgogoro wa kiwanja Duma: Wakatoliki wasema kuna njama za Waarabu Same Na Mwandishi Wetu Wanawake wakutana Mwanza na kusema: Kunyanyaswa sasa basi Na Mwandishi Wetu, Mwanza Sheikh Omar Bashir ataka Waislamu waimarishe mshikamano Na Said Sharif Ustaadhi Abdallah Mfoyi afariki Na Muhibu Saidi Baraza Kuu halina Katibu Nguruka - Sheikh Kilima Na Abu Adli Viongozi Msikiti wa Ubungo Darajani waitwa polisi Na Kassim Juma Marekani `ilivyosaidia' Mujahidiin Barua ya mtoto wa miaka minne toka Lebanon kwa Bibi Hillary Clinton Ujumbe wa waandishi kwa Bw. Batendi, Wakristo Na Muhibu Saidi Waislamu wanadhalilishwa au wanajidhalilisha Tusiwe Jogoo wa Esopo na Almasi Na MAALIM ALI BASSALEH Sherehe za wiki ya usalama barabarani: Kauli nzito za waheshimiwa zimekalia kuti kavu Na Said Omar Mwanasayansi Avicenna: Tabibu bingwa. Na Dk. A. A. Amur Ujenzi wa Msikiti wa Ijumaa Mriti waanza Na Nasib A. Mziray Kutoweka kwa hazina adimu za kimazingira Na Yassir Salim Mfalme Najashi ni mfano bora wa kuigwa kwa watawala Na Idi Kikong'ona Waislamu Moro wasaidia wagonjwa Na Mwandishi Wetu, Morogoro KUFUATIA KUTISHIA MAGAZETI: Sheikh Ayoub amjibu Askofu Rajab Rajab Na Mussa Ally TAMSA Tanga waahidi kuendeleza mema Na Ibn Mohammed, Tanga Ufugaji, uuzaji nguruwe wakera wananchi Dar Na Mwandishi Wetu Mafundisho ya Quran Kuwepo kwa ufufuo Barua za wasomaji
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org