AN-NUUR
Na.167 Jamadul Awal 1419, Septembe 17 - 24, 1998

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita

 

KUFUATIA KUTISHIA MAGAZETI:

Sheikh Ayoub amjibu Askofu

Rajab Rajab na Mussa Ally,

MWENYEKITI wa Baraza Kuu Mkoa wa Morogoro, Sheikh Ayoub Muwinge amemjibu Askofu Telesphor Mkude kufuatia kitisho alichokitoa hivi karibuni katika gazeti la moja binafsi la Septemba 4, 1998 na kukaririwa na Radio Tanzania.

Akiongea na gazeti hili ofisini kwake mapema wiki hii, Sheikh Ayoub amesema inawezekana Askofu Mkude hakujua wanacholalamika Waislamu, aliposema mwalimu ni jukumu lake kujua idadi ya wanafunzi wake na kuwapima.

"Hili jambo halipingiki na Waislamu, lakini jukumu hilo linapobebeshwa serikali hapo ndipo mshangao unapopatikana wakati serikali ina jukumu lake tofauti na hilo", alisema Sheikh huyo maarufu mkoani Morogoro.

Akifafanua zaidi, Sheikh Muwinge amesema utata wa barua ya muelekezaji Idara ya Katekesi Jimbo la Morogoro upo sehemu mbili kama inatoa ombi na pili inatoa amri kwa Afisa Elimu wa Manispaa, jambo ambalo alisema ni kinyume na madaraka aliyonayo Afesa Elimu.

Ameendelea kusema Sheikh Muwinge kwamba si wajibu wa Kanisa au Mkurugenzi kumchagulia mtu Afisa Elimu na kufanya naye kazi ambapo barua ilimwagiza ashirikiane na Mratibu Kata.

"Kwa mpango huu inaonyesha watu waliotakiwa kushirikishwa ni watu walioandaliwa", alisema Sheikh Muinge.

"Inashangaza kuona suala hili linapewa kipaumbele kwa Waratibu kuliko walimu wakuu ambao ndio walezi wa wanafunzi wote pale shuleni. Mfano inatia wasiwasi pale Mratibu mmoja wa Elimu alipowakemea walimu wa shule ya msingi Chamwino kupeleka suala la kuuzwa nyama ya nguruwe shuleni kwa Sheikh na kuita hiyo ni siasa kali", aliongeza Sheikh huyo.

Aidha, amesema kuwa kufuatia barua iliyomwagiza Afisa Elimu kufanya mambo ya Kanisa, inaonyesha wazi ni jinsi gani Kanisa hilo lilivyokuwa na uhusiano wa karibu sana na Wizara hiyo hali ambayo inatishia hujuma kwa Uislamu.

"Hali hii inaonyesha walimu wakuu waliitwa na kuelezwa mpango mzima wa Roman Katoliki, lakini agizo hilo la mdomo likaonekana halitoshi na kuwaandikia barua huku ikizingatiwa kuwa shule ni ya watu wa madhehebu yote", alituhumu Sheikh Muwinge.

Ameendelea kusema kuwa katika kutekeleza agizo hilo limechukua nafasi isiyo halali kwa kutumia muda, mahali na nafasi ya serikali katika jamii jambo ambalo ni hujuma.

Pia Sheikh Muinge amelitaka Kanisa kuacha kuwaandama Waislamu na vyombo vyao, kama kulishutumu gazeti la AN-NUUR kuwa linaandika habari za uchochezi.

"Mshtuko na wasi wasi unapatikana kwa sababu uzoefu unaonyesha Kanisa linaposema jambo lazima serikali ishughulike.

Akatoa mfano mwingine kwamba 1994 Kanisa lilikaa katika Ukumbi mmoja wa CCT na maamuzi yake yalipelekea Waislamu kupigwa mabomu katika Msikiti wa Uwanja wa Ndege mjini Morogoro.

Pia alisema Paroko Luambano alitao shinikizo la kukomeshwa mihadhara ya Waislamu na hatimaye serikali ikaelekeza nguvu zake na kuwadhuru Waislamu katika Msikiti wa Mwembechai.

Vile vile Sheikh Muwinge amepinga vikali dai kwamba Tanzania kuna watu wa siasa kali, bali amesema kuwa kuna watu wenye uchungu kutokana na maonezi makali na ndiyo maana serika hii inawashitaki watu wanaosema Yesu si Mungu na kuwaachia wanaosema Yesu ni Mungu.


TAMSA Tanga waahidi kuendeleza mema

Na Ibn Mohammed, Tanga

KWA mara nyingine uongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu Tanzania tawi la Tanga imeahidi usimamizi wa maadili mashuleni mwao.

Hayo yalikuwa maazimio yaliyosomwa na Mwenyekiti wa TAMSA Mkoa, Ustadh Sudi Ahmed mwishoni mwa semina ya siku moja iliyofanyika Al-Noor Centre, Pongwe Septemba 6, mwaka huu.

Kwa niaba ya uongozi wake, alisema wanaahidi kutokufanya sherehe yoyote isiyoendana na maadili ya Kiislamu. Pamoja na hivyo, pia watasimamia uvaaji wa mavazi ya heshima wawapo shuleni na nje ya shule.

Majukumu mengine yaliyoahidiwa ni kuondosha dhana potofu juu ya asili ya binadamu na wakati huo huo kushirikiana na taasisi zote za Kiislamu.

Akifunga semina hiyo, mlezi wa TAMSA, "dai" wa AMA na Imamu wa Msikiti wa Al-Noor, Juma Mfaki aliwataka wanafunzi wapatao mia mbili waliohudhuria semina hiyo kutokutosheka na semina moja, aliwahimiza kuhudhuria semina nyingine zote zitakazoandaliwa, kwani elimu haipatikani siku moja.

Wanasemina hao mapema walipata fursa ya kutembelea mabweni ya watoto mayatima na kuzungumza nao.

Kila mmoja alitoka na hadithi za kusisimua kutokana na uzuri wa mazingira na nidhamu za mayatima hao.


Ufugaji, uuzaji nguruwe wakera wananchi Dar

Na Mwandishi Wetu

UFUGAJI, uuzaji na uchomaji wa nyama ya nguruwe umeelezwa kuwakera wananchi wengi Jijini, ANNUUR imefahamishwa.

Kumekuwa na malalamiko kutoka sehemu mbalimbali za Jiji kuhusiana na kuzagaa nguruwe na jinsi wahusika, Tume ya Jiji, wasivyoyapa uzito malalamiko hayo ya wananchi hao.

Taarifa kutoka maeneo ya Ubungo Kibangu, Tabata, Segerea, Kisukuru na Kibamba zinaonyesha kwamba ufugaji na uuzaji wa nyama ya nguruwe huenda ukazua mtafaruku iwapo wahusika wataendelea na tabia ya kutia pamba masikioni.

Baadhi ya wananchi wa maeneo hayo walioongea na gazeti hili mapema wiki hii wamedai kuwa licha ya kufikisha malalamiko yao katika vyombo vinavyohusika, ufugaji na uuzaji wa nyama ya nguruwe umeendelea kushika kasi na hakuna hatua zozote zilizokwisha chukuliwa kudhibiti hali hiyo.

"Kwetu sasa nyama ya nguruwe inachomwa mishikaki na kuuzwa kwa wapita njia, tumewaandikia wahusika mpaka sasa hawajachukua hatua zozote", ameeleza mwananchi mmoja wa Tabata ambaye ni Mwalimu katika shule moja ya sekondari Jijini.

Mwananchi mwingine wa Ubungo Kibangu aliyejitambulisha kwa jina la Abu Malik, amedai kuwa katika eneo analotoka (Ubungo) nyama ya nguruwe inauzwa katika magenge pembezoni mwa nyumba.

Bwana Abu ameongeza kudai kuwa biashara hiyo "haramu" ya nyama ya nguruwe sambamba na ufugaji vimekuwa kero kutokana na harufu inayotoka katika mazizi.

"Wahusika wanafanya nini wakati mazingira na afya za wananchi ziko hatarini kiasi hiki", alihoji Bwana huyo.

Aidha, alisema kuwa wao katika eneo lao waliwaandikia barua "wafanyabiashara" hao kuwaomba waache kuendesha biashara hiyo na nakala ya barua hiyo wakapeleka kitengo cha afya Jiji, hata hivyo amedai bwana huyo malalamiko yao yamepuuzwa na pande zote.

"Nyama ya nguruwe inaendelea kuuzwa, Tume ya Jiji haijachukua hatua zozote", alisema kwa masikitiko Bwana Malik.

Mwandishi wa habari hizi alipotembelea moja ya maeneo hayo alishuhudia kuwepo kwa hali hiyo ambapo miguno ya nguruwe ilikuwa ikisikika katika mazizi yasiyo rasmi.

Juu 
 

YALIYOMO  
 
TAHARIRI 
Hakuna Muislamu aliyekufa kutokana na vurugu

Mgogoro wa kiwanja Duma: Wakatoliki wasema kuna njama za Waarabu Same Na Mwandishi Wetu

Wanawake wakutana Mwanza na kusema: Kunyanyaswa sasa basi
Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Sheikh Omar Bashir ataka Waislamu waimarishe mshikamano
Na Said Sharif

Ustaadhi Abdallah Mfoyi afariki
Na Muhibu Saidi

Baraza Kuu halina Katibu Nguruka - Sheikh Kilima
Na Abu Adli

Viongozi Msikiti wa Ubungo Darajani waitwa polisi
Na Kassim Juma

Marekani `ilivyosaidia' Mujahidiin

Barua ya mtoto wa miaka minne toka Lebanon kwa Bibi Hillary Clinton

Ujumbe wa waandishi kwa Bw. Batendi, Wakristo
Na Muhibu Saidi

Waislamu wanadhalilishwa au wanajidhalilisha

Tusiwe Jogoo wa Esopo na Almasi
Na MAALIM ALI BASSALEH

Sherehe za wiki ya usalama barabarani: Kauli nzito za waheshimiwa zimekalia kuti kavu
Na Said Omar

Mwanasayansi Avicenna: Tabibu bingwa.
Na Dk. A. A. Amur

Ujenzi wa Msikiti wa Ijumaa Mriti waanza
Na Nasib A. Mziray

Kutoweka kwa hazina adimu za kimazingira
Na Yassir Salim

Mfalme Najashi ni mfano bora wa kuigwa kwa watawala
Na Idi Kikong'ona

Waislamu Moro wasaidia wagonjwa
Na Mwandishi Wetu, Morogoro

KUFUATIA KUTISHIA MAGAZETI: Sheikh Ayoub amjibu Askofu Rajab Rajab
Na Mussa Ally

TAMSA Tanga waahidi kuendeleza mema
Na Ibn Mohammed, Tanga

Ufugaji, uuzaji nguruwe wakera wananchi Dar
Na Mwandishi Wetu

Mafundisho ya Quran 
Kuwepo kwa ufufuo

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Haja ya maji ya kunywa

 

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org  

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita