|
|
|
Kuisafisha Documents Menu Kila unapotumia kwa mfano Microsoft Word na kuihifadhi (kui-save) kazi yako kwenye faili fulani, jina la faili hilo linaingizwa kwenye sehemu ya Documents, yaani Documents Menu, inayoonekana baada ya kubonyeza Start. Madhumuni yake hasa ni kukurahisishia kazi ya kuyafungua mafaili hayo mara nyengine unapotaka kuongeza kitu kwenye mafaili hayo au unapotaka kuyachapa kwa kutumia printa. Yaani unachokihitaji ni kiasi cha kubonyeza Start -> Documents na ukichagua faili lako, mara moja linafunguliwa na Microsoft Word au programu yoyote uliyoitumia kutengenezea faili hilo. Lakini tatizo ni kwamba, baada ya muda si mrefu, Documents Menu itakuwa na msururu mrefu sana wa mafaili, kiasi cha kuhitaji kusafishwa kidogo. Unaweza pia kuhitaji kuisafisha Document Menu kama kwa mfano ulikuwa unaandika barua ya siri na umeitunza kwenye faili ambalo hupendi watumiaji wengine wa kompyuta hiyo waweze kuifungua kirahisi. Kwa namna hiyo, ukimaliza tu kuiandika barua yako na kuitunza kwenye faili, utahitaji pia kuisafisha Document Menu kwa njia nitakayoieleza hapa chini ili pasisalie kumbukumbu za jina la faili lenye barua yako ya siri. Kuisafisha Document Menu ni kazi rahisi sana. Bonyeza Start -> Settings -> Taskbar -> Start Menu Programs, kisha bonyeza kifungo cha Clear ikifuatiwa na OK. Baada ya kufanya hivyo, ukiangalia Start -> Documents hutakuta kitu tena.
Unapofuta faili kwa kutumia kifungo cha Delete, faili hilo halifutiki hasa bali huwekwa kwenye Recycle Bin. Madhumuni hasa ni kuweza kulipata tena faili hilo kama umelifuta kimakosa. Lakini kama una uhakika wa unachokifanya, na ungependa hasa kulifuta kabisa faili hilo lisionekana tena kwenye kompyuta yako, basi mbinu ya kutumia ni rahisi sana. Ukihitaji kufuta faili, tumia Windows Explorer, bonyeza mouse kwenye faili unalolitaka kulifuta, kisha bonyeza kifungo cha Delete wakati umeshikilia kifungo cha Shift. Ukifanya hivyo utaulizwa kama una uhakika kuwa faili hilo lifutwe. Ukibonyeza Yes faili litafutwa bila ya kuwekwa kwenye Recycle Bin.
Desktop ni sehemu inayoonekana kwenye kompyuta yako baada ya Windows 95 kumaliza shughuli zake za kujianzisha. Hii ni sehemu ambayo zinakuwepo icons za kukusaidia kuanzisha programu mbali mbali kirahisi zaidi. Mara nyengine, unaweza kuwa umefungua madirisha kadhaa na Desktop haionekani kirahisi. Njia zifuatazo zitakuwezesha kuifikia Desktop au icons zilizo kwenye Desktop kirahisi zaidi. Kama shida yako ni kuzifikia icons zilizo kwenye Desktop, lakini kwa bahati mbaya zimefunikwa na madirisha ya programu nyengine ambayo hupendelei kuyafunga, basi bonyeza Start -> Run na kwenye kisanduku cha Open andika nukta, yaani (.) bila ya kuweka hizo brackets (), kisha bonyeza Enter. Ukifanya hivyo kitatokezea kidirisha chenye icons zilizo kwenye Desktop na utaweza kuanzisha programu nyengine kwa kutumia icons hizo. Njia ya pili na ya uhakika zaidi kuweza kufikia icons zilizo kwenye Desktop ni kuyafunga madirisha yote kwa mpigo. Kufanya hivyo bonyeza kifungo cha kulia cha mouse kwenye sehemu tupu ya Taskbar na uchague Minimize All Windows. (Taskbar ni mstari wenye Start na ambao pia unaandikwa jina la kila programu unayoifungua. Mara nyingi unakuwa chini ya kioo cha monita). Kurudisha madirisha yako, bonyeza tena kifungo cha kulia cha mouse kwenye sehemu tupu ya Taskbar na uchagua Undo Minimize All.
Sijui wewe, lakini mimi mara kadhaa ninapotumia programu mbali mbali kwenye Windows 95, programu hizo hugoma katikati na hukatakaa kabisa kufanywa chochote. Ikitokezea hivyo, huna lazima ya kuianzisha upya Windows 95. Badala yake unaweza kuifunga programu iliyogoma tu kwa kubonyeza vifungo vitatu – Ctrl + Alt + Delete, vyote kwa wakati mmoja. Kubonyeza vifungo hivyo kwa wakati mmoja baadhi ya watu wanaita kuwa ni three-finger salute, yaani saluti ya vidole vitatu. Ukibonyeza saluti ya vidole vitatu, utaiona programu iliyokugomea. Ibonyezee mouse na ubonyeze kifungo cha End Task ili kuifunga programu hiyo iliyogoma na kuweza kupata nafasi ya kuendelea na shughuli nyengine ikiwemo kuianzisha upya programu hiyo iliyogoma – kama utapenda, au kuizima kompyuta yako kistaarabu zaidi kwa kutumia taratibu za kawaida za ku-shutdown.
Kuna namna kadhaa za kuanzisha programu ya kutafuta mafaili kwenye Windows 95. Unaweza kutumia Start -> Find -> Files and Folders; au ukiwa kwenye Windows Explorer, unaweza kuchagua Tools -> Find -> Files and Folders, n.k. Sasa, kama kompyuta yako imejaaliwa kuwa na drives kadhaa, unaweza kutafuta faili unalolitaka kutoka kwenye drives kadhaa kwa wakati mmoja. Picha 1 inaonyesha mfano wa kutafuta faili lenye jina "clip"
kutoka kwenye drives kadhaa. Jina la faili (au sehemu ya jina lake),
inaandikwa kwenye kisanduku cha "Named", na kwenye kisanduku cha
"Look in" zinaandikwa herufi za drives zote zitakazotumiwa
kutafutia faili hilo. Herufi za drives hizo ziandikwe kama inavyoonekana
kwenye Picha 1, yaani kila drive ikitenganishwa na drive
nyengine kwa semicolon yaani (;) na nafasi tupu, yaani space.
Unapobonyeza kifungo cha Find Now faili lako litatafutwa kwenye
drives zote kwa wakati mmoja.
![]() |
YALIYOMO
Tahari
Mwaka mmoja wa mauaji ya Mwembechai:
Waliouawa ni wanne
Waasisi wa TAA waibuka kupigania haki zilizoporwa Kuhujumiwa Waislamu kielimu: Mzazi adai mwanafunzi Adam Rashid kafelishwa Maoni yetu: Tuondoleeni wenye mikono ya damu MARADHI YA KISAIKOLOJIA: MULTIPARAPHILIASIS Askari wa Tume ya Jiji wapora mkaa Kuchangia Radio Kheri Broadcasting Station Yesu Kristo na Yohana Mbatizaji
Wakereketwa CCM wawakosha
wauaji wa Mwembechai
Ufugaji holela wa nguruwe
waikumba Dodoma
Watembelea na kusaidia wagonjwa Arusha Mkuu wa wilaya awatimua Masheikh
ofisini kwake
Sayansi na Teknolojia
Chakula na Lishe
Kumbukumbu ya mauaji Mwembechai
|