AN-NUUR 
Na.188 Shawwal 1419, Februari 12 - 18 , 1999 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Historia: Form IV 
 
Upinzani dhidi ya Serikali ya Kiislamu wakati wa Khalifa wa Tatu Uthman bin Affan 
 

Imesemwa kuwa nimewateua vijana wadogo maafisa. nimefanya hivyo kwa kuzingatia mchango katika uislamu. hakuna anaekanusha uaminifu wao na mchango wao katika Uislamu, na Waislamu. Kuteuliwa kwa Usmaha na Mtume (s.a.w.) kuwa kamanda wa jeshi ni ushahidi kuwa ujana sio kipingamizi cha kupewa uafisa. 

Imedaiwa nimempa gavana wa Misri ngawira yote ya Afrika kaskazini kama zawadi. Ni kweli lakini niliposikia jamii haikupendezwa na jambo hili nimezichukuwa fedha zote kutoka kwa gavana na kuziweka kwenye mfuko wa serikali (Baitul Mal)... 

Inadaiwa kuwa nimetenga mbuga za malisho ya serikali kwa ajili ya wanyama wangu. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, sitafanya hivyo. Katika mbuga hizo (mashamba hayo) ni wanyama wa Serikali tu (Baitul Mal) ndio wanaolishwa humo, wote mnafahamu kuwa nilipopewa ukhalifa nilikuwa na wanyama wengi kuliko yoyote Arabia nzima. Leo nina ngamia wawili niliowaacha ili wanisaidie wakati wa Hija. Ingekuwaje, nitenge malisho ya serikali kwa ajili yangu wakati wanyama wenyewe sina. 

Watu wananilaumu kwa kuchoma nakala za Qur’an. Qur’an tukufu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu aliteremshiwa Mtume (s.a.w.). Maswahaba waliokiandika chini ya usimamizi wa Mtume wako hai. Nimepeleka ile nakala ya Qur’an iliyokusanywa na maswahaba. 

Inasemwa kuwa nimemrudisha Hakam Madina ambae alipelekwa uhamishoni na Mtume. ukweli ni kwamba Mtume alimhamisha Hakam kutoka Makka kwenda Taif. Baada ya kumwombea Mtume alimruhusu aishi Madina. Nimetekeleza ruhusa iliyotolewa na Mtume (s.a.w.)...." 

(Mwisho wa Hotuba yake akasema). Niambieni kama kuna kitu kisichokuwa cha kweli kati ya niliyosema... 89 

ingawa Khalifa alijibu shutuma zote kwa ufasaha, ukweli na uwazi wawakilishi wa wapinzani walirudi na kusema uongo kuwa Khalifa amepuuza madai yetu. Ndipo wakaja makundi ya watu elfu, elfu kutoka Misr, Basra na Kufa na kupiga kambi karibu na Madina. Waliotoka Basra walipiga kambi Dhikhashab, waliotoka kufa walikaa A’was na waliotoka Misri walikaa Dhi-Murwah. Makundi ya wahaini hawa walishindwa kuingia Madina moja kwa moja kwa sababu walipokuwa wanakaribia Madina, Khalifa alikusanya wakazi wa Madina na kuwahutubia kuwa; 

wananikusudia mimi, karibuni hivi watakumbuka wakati wa ukhalifa wangu na kuujutia, wataona siku moja ni kama mwaka kwa sababu ya vurugu umwagaji damu na uasi utaoenea nchi nzima.90 

Wananchi walichukua silaha na kuzuia uvamizi wa mji wao. Hali hii ndiyo iliyolazimisha wahaini kukaa nje ya Madina. 

Wahaini hawa walikuwa na agenda moja tu, ya kumwondoa Khalifa madarakanai kwa hiyari au kwa nguvu. ndio maana walipofika tu Madina kila kikundi kilimkabili waliyemtaka awe Khalifa kwani katika hili walitofautiana Ibn Saba na Wamisri walimtaka Ali. Watu wa Kufa walimtaka Zubair na watu wa Basra walimtaka Talha. Maswahaba wote hawa walikataa na kuwaambia kuwa Mtume (s.a.w.) aliwaambia makundi ya Dhikkasha, A’was na Dhi-murwah wamelaaniwa..91 

Khalifa aliwatuma maswahaba maarufu akiwemo Ali kusikiliza malalamiko yao. Wamewakilisha matakwa yao pamoja na kutaka Muhammad Ibn Bakr awe gavana wa Misri badala ya Abu Mussa. Khalifa alikubali bila kuuliza kisha akawaahidi kuwa atatekeleza maombi yao. Ali nae akasisistiza hivyo hivyo. 

Kuzingirwa nyumba ya Khalifa 

Waasi hawa wakidai kama wamekubaliana na ahadi ya Khalifa na wakawa kama wanaondoka. Watu wa Madina kuona hivi wakaacha ulinzi wa mji wao na wakarudia maisha yao ya kawaida. Ghafla wapinzani wakawa wako Madina na kelele ya kulipiza kisasi. Wapinzani walighushi barua kutoka kwa Khalifa na muhuri wa Khalifa aliyomuandikia Gavana wa Misri kuwa wataporudi wapinzani awauwe wote. Wahaini hawa walidai kuwa wamemkamata mtumishi wa Khalifa akipeleka barua hii. Ali alipotaka kujua walivyoweza kuwasiliana yote makundi matatu yanayokwenda njia mbali mbali juu ya barua hii hawakuwa na jibu. Ni wazi barua hii haikutoka kwa Khalifa kama Khalifa mwenyewe alivyoshuhudia. Lakini kwa kuwa huu ulikuwa ni mpango tu, wapinzani hawa hawakumsikiliza mtu na kusema uandike usiandike hufai kuwa kiongozi - na kumtishia kumuua ambapo Khalifa naye aliwajibu siogopi kufa nakataa kumwaga damu ya Waislamu.92 Barua anayosingiziwa Khalifa sio ya kweli kwa sababu kadhaa. 

Kwanza ilikuwa ni upumbavu kufikiria kuwa kwa kuwaua wahaini wa Misri au kuwafunga kungeondoa upinzani. Pili hata kama wapinzani wa Misri wangedhibitiwa kwa njia hii hakuna ambacho kingewazuia wapinzani wa Kufa na Basra kuendeleza upinzani wao na kwa kweli ingewaongezea hoja ya fujo zao. Tatu, kama Uthman angetaka kutumia nguvu watu wa dola nzima walikuwa tayari kuwadhibiti wahaini hawa. Hata kama labda angeona pengine kuandika kungefaa, basi angemuandikia Muawiya ambae alikwisha tamka kuleta jeshi lake kama Khalifa angeonyesha dalili tu ya kukubali. Hivyo barua hii ni ya kughushi tu wala Marwan katibu wa Khalifa hakuhusika pia. 

Kwa kutumia uongo huu wa barua, sasa wakaja na jingine wakataka Khalifa ajiuzulu. Khalifa alikataa na kusema, "Siwezi kuvua mwenyewe joho la heshima alilonivisha Mwenyezi Mungu. 93 

Wahaini hawa sasa wakazingira nyumba ya Khalifa na hawakumruhusu kutoka ila kwa swala tu na baadae pia walimkataza asitoke. Hata hivyo vijana shujaa walilinda mlango wa nyumba ya Khalifa ili wahuni wasiingie na kumuua Khalifa. Mashujaa hawa walikuwa Hassan, Hussein, Muhammad bin Talha na Abdullah bin Zubair. Waliokuwa ndani ya nyumba ni Khalifa na mkewe Nailah na Marwan. Hali ya kuzingirwa ilipozidi kuwa mbaya, baadhi ya maswahaba maarufu kama Mughira bin Subah walimwomba Khalifa awaruhusu watu wa Madina wawarudi wapinzani lakini Khalifa alikataa. 

Juu 
 

YALIYOMO 
  

Tahari 
Tusirudishane nyuma 

Mwaka mmoja wa mauaji ya Mwembechai: Waliouawa ni wanne
Na Mwandishi wetu

Waasisi wa TAA waibuka kupigania haki zilizoporwa

Kuhujumiwa Waislamu kielimu: Mzazi adai mwanafunzi Adam Rashid kafelishwa

Maoni yetu: Tuondoleeni wenye mikono ya damu

MARADHI YA KISAIKOLOJIA: MULTIPARAPHILIASIS

Askari wa Tume ya Jiji wapora mkaa

Kuchangia Radio Kheri Broadcasting Station

Yesu Kristo na Yohana Mbatizaji
Na BERNARD B. MWENDA

Wakereketwa CCM wawakosha wauaji wa Mwembechai
Na Idd Kikong’ona, Morogoro

Ufugaji holela wa nguruwe waikumba Dodoma
Na Abu Zubeir, Dodoma

Watembelea na kusaidia wagonjwa Arusha

Mkuu wa wilaya awatimua Masheikh ofisini kwake
Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Kutoka magazeti ya zamani

Sayansi na Teknolojia 
[Windows: Mambo Mazuri ya Kuyajua] 

Masomo ya Kiislam 

Barua za Wasomaji 

Mashairi

Chakula na Lishe 
[Kauli hii ya serikali itatumaliza Watanzania kwa njaa] 

Kumbukumbu ya mauaji Mwembechai 
[Maazimio ya Maimamu Dar]
 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita