|
|
|
NILIBAHATIKA kukutana na miongoni mwa waandishi wa ANNUUR pindi nilipokuwa Dar es Salaam baada ya maongezi mafupi niliharakishia kutaka kujua juu ya tangazo linalowataka Waislamu kuchangia Radio ya Kiislamu (Radio Kheri), swali lilikuwa, jinsi gani Waislamu walivyoitikia wito wa kuchangia Radio Kheri? Jibu, hali si nzuri kabisa. Jibu hili lilininyongesha na kupata fikra na kushika kalamu kutoa hoja binafsi juu ya Waislamu wa Tanzania kufanikisha azma hii, mwandishi KAWELA SAID toka Dodoma anaanza makala yake hivi... Kabla sijatoa pendekezo binafsi naanza makala hii kwa maswali matatu: Je, Waislamu wa Tanzania tumeshindwa kupata milioni 34, kwa zaidi ya mwaka sasa toka kupatikana kwa kibali serikalini cha kuanzisha Radio? Je, Waislamu tumekuwa maskini wa kiwango hiki? Je, hatuelewi umuhimu wa kuwa na Radio yetu hususan katika kipindi hiki cha mmomonyoko wa maadili ya jamii? Bahati ambayo Waislamu wa Tanzania tumepata ni ya kumshukuru Allah (s.w.) ambaye amejalia kwa upandewa BARAZA KUU kufikia hatua ya kupatikana kwa kibali cha kuanzisha Radio ya Kiislamu, wasiishie hapo tu, bali tunahitaji pia tupate Televisheni yetu na Benki za Kiislamu. Kila Muisamu aje na shilingi 200 kila wiki na kila mwezi kwa miezi minne. Misikiti 20 x 600 Waislamu x 200/= kwa wiki x 4x4 = yaani 20x600 = 12000 x 200 = 2,400,00 x 4 = 9,000,000 x 4 = 38,400,000. Hesabu hizi zinaonyesha kuwa Waislamu 12000 ambao wanasali sala ya Ijumaa kwa Tanzania nzima iwapo watadhamiria kwenda na shilingi 200 kila Ijumaa kwa wiki zipatikana shilingi 2,400,000 kwa mwezi 9,600,000 na kwa miezi minne shilingi 38,400,000 kwa utaratibu huu hatujapata Radio Kheri kwa ulaini bila ya hata kuwa na wafadhili? Je suala hili Masheikh wa Mikoa hawawezi kuwahamasisha waumini wao kusaidia suala hili muhimu? La kuzingatia hapa ni kuwa idadi hii ni ndogo sana, kwani Dar es Salaam, Tanga, Mwanza n.k. Idadi ya Waislamu wanaokutana katika sala ya Ijumaa ni zaidi ya mara mbili na nusu. Hivyo natoa wito kwa Waislamu wenzangu tuazimie jambo
hili, na Radio hii ni ya Waislamu si ya BARAZA KUU kama vile lilivyo gazeti
la ANNUUR, ni gazeti la Waislamu na siyo gazeti la I.P.C (Islamic
Propagation Centre) iwapo tunataka tuingie katika karne ya sayansi na teknolojia
basi tuelewe BARAZA KUU wamepania kuwaingiza Waislamu wa Tanzania katika
karne hiyo. Tafadhali tusijiweke katika miaka ya 47.
|
YALIYOMO
Tahari
Mwaka mmoja wa mauaji ya Mwembechai:
Waliouawa ni wanne
Waasisi wa TAA waibuka kupigania haki zilizoporwa Kuhujumiwa Waislamu kielimu: Mzazi adai mwanafunzi Adam Rashid kafelishwa Maoni yetu: Tuondoleeni wenye mikono ya damu MARADHI YA KISAIKOLOJIA: MULTIPARAPHILIASIS Askari wa Tume ya Jiji wapora mkaa Kuchangia Radio Kheri Broadcasting Station Yesu Kristo na Yohana Mbatizaji
Wakereketwa CCM wawakosha
wauaji wa Mwembechai
Ufugaji holela wa nguruwe
waikumba Dodoma
Watembelea na kusaidia wagonjwa Arusha Mkuu wa wilaya awatimua Masheikh
ofisini kwake
Sayansi na Teknolojia
Chakula na Lishe
Kumbukumbu ya mauaji Mwembechai
|