AN-NUUR 
Na.188 Shawwal 1419, Februari 12 - 18 , 1999 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
MARADHI YA KISAIKOLOJIA:
 
MULTIPARAPHILIASIS
 

Kwa wale waliokuwa wakifuatilia makala hizi, nadhani wameelewa kiasi kikubwa maana ya mtu kuwa na maradhi ya kisaikolojia, hususan yale yanayoambatana na kukithiri kwa zinaa katika jamii. Napenda kusisitizia kuwa kuenea kwa maradhi haya kunatokana na kukithiri kwa gonjwa kubwa la zinaa. Gonjwa hili baya linapoachiwa, na kupewa uhuru, kama ilivyo katika jamii zetu za "kisasa", basi haya maradhi mengine yote huja kama ziada. Qur’an inawataja watu wenye maradhi haya: "Ndani ya nyoyo zao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu akawazidishia maradhi". (Qur’an 2:10) 

Kwa hiyo kwa vile gonjwa kuu limeingia ndani ya mioyo ya watu, basi ziada ya gonjwa hilo ni haya maradhi tuliyokuwa tukiyachambua ya Paraphilia za aina mbalimbali. 

Leo napenda kuongelea uwezekano wa mtu mmoja kuwa na mchanganyiko wa maradhi ya kisaikolojia zaidi ya moja. Mtu anapokuwa na Paraphilia nyingi, basi tunasema mtu huyu anaugua gonjwa kubwa la kisaikolojia linaloitwa Multiparaphiliasis. 

Huyu kichwa chake kinakuwa na vurugu zote za kimawazo tulizozidhambua huko nyuma. Kwa mfano, Mwendawazi (mtu anayependa kwenda wazi kwa viguo vifupi) mara nyingi huwa na Voyeur (kozimeni), anayependa kukodolea macho watu walio wazi. Mtu huyu pia kwa asilimia kubwa anaweza kuwa mminyaji (Fratter), anayependa miminyano na watu wa jinsia tofauti na yeye. 

Vilevile, mwanaume yeyote aliyekubuhu katika uchafu wa zinaa ana hatari ya kuwa na maradhi haya ya Multiparaphiliasis. Utamkuta kote. Voyeur yeye, kwenye Sexual sadism yumo, Fratteurism yumo, kwenye Fetishism utakumta na wengi wao wanaweza wasiwe na maradhi ya Transexualism ( kutamani kuwa wanawake), lakini wengi wao utawakuta kwenye Transvestims (kupenda kujipamba kike) hasa kuvaa mikufu ya dhahabu na kubadili nywele ziwe laini na kujipulizia mafuta uzuri yenye harufu kali ili wanukie. 

Pia utawakuta wanafuga kucha ndefu mithili ya wale wanawake wanaopenda kujipaka marangi kama nyumba, au gari ya mashindoni. 

Sasa jamii ikishafikia kuwa na watu wenye msetu wa maradhi ya kisaikolojia, basi huwa inasubiri gharika. Na gharika sio lazima iwe kama ya wakati wa Nabii Nuhu, bali hata gonjwa linaloua kama ukimwi pia ni gharika. 

Labda tu leo nisiseme mengi. Maradhi haya huwapata watu wenye UKIMO (ukosefu wa Kinga Moyoni). Hii ina maana kwamba moyoni mwao hamna chembe ya hofu ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, mtu akiwa hana chembe ya ucha Mungu, amri za Mungu zinazoweza kumsaidia, haziingii katika moyo wake, kwa mfano ile amri ya: 

"Wala msikaribie zinaa, Hakika hiyo ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa)". (Qur’an 17:32) 

Hakuna daktari wa kutibu maradhi haya, bali tiba inapatikana kwa mtu kuwa Muislamu mtimilifu, ambaye hana UKIMO. 

Juu 
 

YALIYOMO 
  

Tahari 
Tusirudishane nyuma 

Mwaka mmoja wa mauaji ya Mwembechai: Waliouawa ni wanne
Na Mwandishi wetu

Waasisi wa TAA waibuka kupigania haki zilizoporwa

Kuhujumiwa Waislamu kielimu: Mzazi adai mwanafunzi Adam Rashid kafelishwa

Maoni yetu: Tuondoleeni wenye mikono ya damu

MARADHI YA KISAIKOLOJIA: MULTIPARAPHILIASIS

Askari wa Tume ya Jiji wapora mkaa

Kuchangia Radio Kheri Broadcasting Station

Yesu Kristo na Yohana Mbatizaji
Na BERNARD B. MWENDA

Wakereketwa CCM wawakosha wauaji wa Mwembechai
Na Idd Kikong’ona, Morogoro

Ufugaji holela wa nguruwe waikumba Dodoma
Na Abu Zubeir, Dodoma

Watembelea na kusaidia wagonjwa Arusha

Mkuu wa wilaya awatimua Masheikh ofisini kwake
Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Kutoka magazeti ya zamani

Sayansi na Teknolojia 
[Windows: Mambo Mazuri ya Kuyajua] 

Masomo ya Kiislam 

Barua za Wasomaji 

Mashairi

Chakula na Lishe 
[Kauli hii ya serikali itatumaliza Watanzania kwa njaa] 

Kumbukumbu ya mauaji Mwembechai 
[Maazimio ya Maimamu Dar]
 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita