AN-NUUR 
Na.178 Shaaban  1419, Desemba 4 - 10, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Chalula na Lishe:
 
Madini ya Zinc
 

Na Mujahid Mwinyimvua 

Ili mwili wa mwanadamu uweze kukaa na kunawili vizuri lazima upate virutubisho vinavyoitwa madini. Katika makala iliyopita tulianza kuzungumzia dhana hii ya madini kwa kutazama madini ya chuma. Makala yetu ya wiki hii inatazama madini ijulikanayo kwa kimombo kama madini ya zinc (Zinki). 

Madini ya zinc ni moja ya madini inayohitajika mwilini kwa kiasi kidogo lakini ina umuhimu mkubwa, kwa wastani mtu mzima ana madini ya zinc kiasi cha gramu 2.5 (mbili na nusu) sawa na nusu ya kijiko cha chai. Utafiti wa miaka ya hivi karibuni umedhihirisha umuhimu wa madini hii kwa afya ya binadamu. Hivyo basi, watu wasiidharau kwa hoja tu kuwa inahitajika kwa kiasi kidogo mwilini. 

Madini ya zinc ina kazi nyingi mwilini, baadhi yake ni kuuwezesha mwili kukua na kunawili vizuri, kulinda mwili usipate magonjwa, kufanya vidonda kupona haraka, kusaidia macho kuweza kuona vizuri, inapunguza harufu mbaya kutoka mwilini, inasaidia milango ya fahamu ya kunusa na kuonja kufanya kazi vizuri, n.k. 

Ukosefu au upungufu wa madini ya zinc nao unasababisha madhara kadhaa kwa mfano, ukuaji kwa watoto unakwenda kwa kasi ndogo, mtu anakosa hamu ya kula chakula, ubongo (akili) unaweza kuathirika, vidonda haviponi kwa haraka, viungo vya uzazi kwa wavulana havikui kwa haraka, uzito wa mtu unapungua, milango ya fahamu (kunusa na kuonja) haifanyi kazi vizuri, macho hayao ni vizuri hasa usiku, na ngozi haiwi katika hali nzuri. 

Kila binadamu anahitaji madini ya zinc lakini watoto, kina mama wajawazito na wale wanaonyonyesha wanahitaji zaidi madini hayo. Yaani mahitaji yao ni makubwa kuliko watu wengine. 

Vyakula vingi vya Kiafrika vina madini ya zinc. Hata hivyo, mtu anaweza kuwa na upungufu wa madini ya zinc kama hatakula mlo kamili. Vile vile ikumbukwe kuwa, kama ilivyo madiniya chuma, uwezowa mwili kuweza kunyonya madini ya zinc kutoka katika vyakula tunavyokula unategemea sana aina ya vyakula mtu anavyokula, wakati huo anapokula vyakula vyenye madini ya zinc. Kwa mfano, vyakula vya nyuzi nyuzi na nafaka zisizokobolewa hupunguza uwezo wa mwili kunyonya madini ya zinc kutoka katika vyakula tunavyokula. 

Vyakula vyenye madini ya zinc kwa wingi ni kama vile nyama, samaki, nafaka, mboga, jamii ya kunde (maharage, njegele, kunde, n.k.) na maziwa ya mama. 

Jambo la kuzingatia ni kwamba kila mlo (wa asubuhi, mchana au usiku) lazima uwe mlo kamili. Yaani uwe na makundi yote sita ya virutubisho kama tulivyoona katika makala za nyuma. 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
'White Paper  ni ulaghai wa  Serikali ya CCM' 
Na Mwandishi wetu 

Sheikh Omar Bashir awekwa rumande 
Na Mwandishi Wetu 

Mpango wa 'Kupindua' uongozi wa  Bakwata: Masheikh Dar waitwa polisi kuhojiwa 
Na Mwandishi Wetu 

Zahrau Day yatikisa Tanga 
Na Mwandishi Wetu 

MAKALA: Hatuna haja ya maelekezo ya yule aliyetufikisha hapa  
Na Alhaj Yusuf Kalala, Washington DC USA 

Huduma za afya Kondoa haziridhishi 
Na Abu Zubeir 

Wasemavyo wanaharakati 

Tunahitaji 'UN' ya Waislamu! 
Na Twahir Rashid 

Hoja binafsi: Wawekezaji watuondokesha makwetu 

Jamii inapokuwa soko huria...  
Na Said Rajab 

Someni kwa ajili ya Allah - Sheikh Baruti  
Na Muhibu Said 

Madrasa Al-Ii'Tiswamu Al-Umaahaati Fiisabiililillah - Moro 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Madrasat Hidayat Mbagala 
Na Mussa Salum  

Hali ya Uislamu Moro Vijijini yazidi kuwa mbaya  
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Sheikh Masoud Mwinyi awaonya Waislamu kuacha migogoro Babati  
Na Abu Zuberi - Babati 

Tusikaribishe mfungo wa Ramadhani kwa Vunja Jungu  
Na Abeid Poyo 

'Acheni zinaa muepukane na ukimwi'  
Na Mussa Salum 

Wavunja jungu watahadharishwa 
Na Mwandishi Wetu, Morogoro 

Hoja/Uchambuzi: 
Je, hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? 
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu 

Njia ya uzimani ni nyembamba,  waionao ni wachache 
Na Yasin Valerian Massawe 

Habari: 
Semina ya Maimamu Tanga yadai: Maimamu wanapuuzwa  
Na Mwandishi Wetu 

Kesi ya Waislamu Mwembechai yaahirishwa kwa mara nyingine  
Na Muhibu Saidi 

Kongomano la wanawake wa Kiislamu Bagamoyo 
Na Mwandishi Wetu 

Sayansi na Teknolojia 
[Kuongeza RAM kwenye Kompyuta] 
 
Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Madini ya Zinc] 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita