AN-NUUR 
Na.178 Shaaban  1419, Desemba 4 - 10, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Huduma za afya Kondoa haziridhishi 
 

• Barabara nazo zitaabani 
 

Na Abu Zubeir 

Wakati nchi ikijiandaa kuingia karne ya 20 ambayo hutajwa kuwa ni ya Sayari na teknolojia, hali ya huduma za afya kijiji cha Berera tarafa ya Bereko Wilayani Kondoa ni mbaya. 

Uchunguzi unaonyesha kwamba wananchi wa kijiji hicho wamekuwa wakipata usumbufu wa kusafiri kwa miguu kwa umbali wa kilometa tisa hadi kijijicha Kikiri kwa ajili ya kupata matibabu. 

Wanakijiji wa Bereko walimfahamisha mwandishi wa habari adha wanayoipata pale mgonjwa anapkuwa katika hali mbaya. 

Wamesema hulazimika kumpeleka Kondoa mjini ambako ni umbali mkubwa kutoka kijijini hapo. 

Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Idrisa ambaye ni mfanyabiashara alimweleza mwandishi kuwa wanawake waja wazito hulazimika kusafiri hadi Kondoa mjini kwa tahadhari ya matatizo yanayoweza kutokea wakati wa kujifungua. 

Wakati huo huo, hali ya barabara Wilayani Kondoa ni mbaya sana kiasi cha kutishia kusimama shughuli mbali mbali za wakazi wa wilaya hiyo katika kipindi cha mvua. 

Maeneo ambayo huenda yakaathirika zaidi katika kipindi hicho ni Bakulu na Nasawi Kichangani (Kisangani). 

Wakazi wa sehemu hizo wamemweleza mwandishi kuwa ingawa hivi sasa yamemwagwa malori saba ya changarawe kwa ajili ya ukarabati, wana wasi wasi wa kudumu kwa mawe hayo wakati wa mvua. 

Akiongea na mwandishi, mkazi mmoja wa vijiji hivyo Bwana Ilovya alisema wafanya kazi wa idara ya ujenzi hufika mara kadhaa sehemu hizo lakini hakuna matengenezo yoyote waliyofanya katika barabara hizo. 

"Tunaiomba Serikali itupie jicho barabara hizi hivi sasa kwani mvua zikianza hakutakuwa na mawasiliano kabisa hasa pale yanapotokea magonjwa ya milipuko", alisisitiza Bwana Ilovya. 

Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 1995 aliyekuwa mgombea wa chama tawala (Rais Benjamin Mkapa) aliahidi kuimarishwa kwa miundo mbinu ili kuchochea maendeleo ya wananchi katika sehemu mbalimbali za nchi. Tangu wakati huo imeelezwa kuwa hapajafanyika lolote lenye kuashiria kutekelezwa ahadi hiyo. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
'White Paper  ni ulaghai wa  Serikali ya CCM' 
Na Mwandishi wetu 

Sheikh Omar Bashir awekwa rumande 
Na Mwandishi Wetu 

Mpango wa 'Kupindua' uongozi wa  Bakwata: Masheikh Dar waitwa polisi kuhojiwa 
Na Mwandishi Wetu 

Zahrau Day yatikisa Tanga 
Na Mwandishi Wetu 

MAKALA: Hatuna haja ya maelekezo ya yule aliyetufikisha hapa  
Na Alhaj Yusuf Kalala, Washington DC USA 

Huduma za afya Kondoa haziridhishi 
Na Abu Zubeir 

Wasemavyo wanaharakati 

Tunahitaji 'UN' ya Waislamu! 
Na Twahir Rashid 

Hoja binafsi: Wawekezaji watuondokesha makwetu 

Jamii inapokuwa soko huria...  
Na Said Rajab 

Someni kwa ajili ya Allah - Sheikh Baruti  
Na Muhibu Said 

Madrasa Al-Ii'Tiswamu Al-Umaahaati Fiisabiililillah - Moro 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Madrasat Hidayat Mbagala 
Na Mussa Salum  

Hali ya Uislamu Moro Vijijini yazidi kuwa mbaya  
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Sheikh Masoud Mwinyi awaonya Waislamu kuacha migogoro Babati  
Na Abu Zuberi - Babati 

Tusikaribishe mfungo wa Ramadhani kwa Vunja Jungu  
Na Abeid Poyo 

'Acheni zinaa muepukane na ukimwi'  
Na Mussa Salum 

Wavunja jungu watahadharishwa 
Na Mwandishi Wetu, Morogoro 

Hoja/Uchambuzi: 
Je, hivi tuendelee kushika amri za Mungu tena? 
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu 

Njia ya uzimani ni nyembamba,  waionao ni wachache 
Na Yasin Valerian Massawe 

Habari: 
Semina ya Maimamu Tanga yadai: Maimamu wanapuuzwa  
Na Mwandishi Wetu 

Kesi ya Waislamu Mwembechai yaahirishwa kwa mara nyingine  
Na Muhibu Saidi 

Kongomano la wanawake wa Kiislamu Bagamoyo 
Na Mwandishi Wetu 

Sayansi na Teknolojia 
[Kuongeza RAM kwenye Kompyuta] 
 
Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Madini ya Zinc] 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita