|
|
|
Na Abeid Poyo Waislamu wametahadharishwa na kufanya mambo maovu unapokaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa hoja ya kuvunja jungu. Hayo yamesemwa na Sheikh Alhad Mussa Imam wa Msikiti wa Majumuatil Islamiya alipokuwa akizungumza na waumini baada ya sala ya Ijumaa Msikiti wa Temeke Mwisho, Jijini. Alinukuu hadithi ya Anas isemayo "walikuwa Waislamu kila ukikaribia kuingia kwa mwezi wa Ramadhani wakisoma Quran na wale wenye uwezo kimali wakitoa mali kuwapa maskini ili kuwapa nguvu (Kujiandaa na mfungo wa Ramadhani). Aliongeza kusema kuwa kama ni kuvunja jungu basini huku kulikokuwa kukifanywa na maswahaba watukufu. Sheikh Alhad aliendelea kuwaasa Waislamu hasa vijana wanaofanya kila aina ya maovu kama uzinzi, unywaji pombe, miziki na mengineyo kwa kisingizio cha kuvunja jungu waache tabia hiyo kwani ni kinyume na Uislamu. Sheikh Alhad alihitimisha mazungumzo ya kwa kuwaambia Waislamu , kuwa huenda akalizungumza tena suala hili la "Vunja Jungu" kwa undani katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi huu wa Shaabani. Na Mussa Salum IMEELEZWA kuwa kama jamii inataka iondokane najanga la kuambukizwa na ukimwi, wananchi hawanabudi kuachana na zinaa tamko ambalo linakwenda sambamba na makatazo yanayotolewa na viongozi mbalimbali wa dini hapa nchini. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Temeke hivi karibuni, Sheikh Ali Mohamed alisema kuwa ugonjwa wa ukimwi hauna dawa hadi sasa na dawa kamili ya ugonjwa huo ni kuachana na vitendo vya zinaa na kuongeza kuwa kondom sio tiba ya ugonjwa huo. Sheikh Ali alisema kuwa mara nyingi viongozi wa dini wamekuwa wakipiga kelele kuhusiana na ugonjwa huo lakini jamii zimekuwa zikipuuzia hali inayofanya ugonjwa huo uzidi kuota mizizi hapa nchini. Alisema endapo zinaa itaachwa mara moja gonjwa hilo ni tishio katika maisha ya watu karibu sehemu mbalimbali za dunia unaweza kupungua kwa kiasi fulani na kuongeza kuwa hakuna budi kwa waumini wa dini mbalimbali kuanza kuwaelimisha wananchi jinsi ya kuachana na zinaa. Alisema Zinaa imekatazwa katika Qur-an na Biblia kama kinavyotumika na waumini wa dini ya Kikristo hivyo waumini wa dini hizo hawanabudi kuzifuata kama wanataka kuepukana na ugonjwa huo hatari ambao hauna tiba wala kinga hadi sasa. "Dawa pekee ya ukimwi ambayo ipo hadi sasa ni kufuata maneno matakatifu kutoka katika vitabu vya dini, Qur-an na Biblia, kuacha zinaa" alisisitiza Sheikh Ali. Aliwaasa waumini wa dini zote kuzungumzia jinsi ya kupigana vita na
ueneaji wa ugonjwa huo ambao umepoteza Watanzania wengi tangu ulipoanza
katika miaka ya mwanzoni mwa 1980 ambapo alisema vitendo vya kujimiiana
vinavyofanywa na watu wa rika mbalimbali vimechangia kuenea kwa ugonjwa
huo.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro Waislamu wametahadharishwa na kutakiwa kujiepusha na tabia ya kumkejeli na kumtania Allah (s.w.) kwa kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kufanya yaliyo maovu na machafu chini ya anwani ya kuvunja jungu. Akiwakumbusha Waumini katika Msikiti wa Mafiga Mjini Morogoro, Ustaadh Mohamed Suleimani aliikemea dhana ya kuvunja jungu na kudai kuwa inapingana na mafundisho ya Qur’an na Sunna ya Mtume (s.a.w.) na kusema kuwa inaondoa "mafuhumu" ya funga. ya Ramadhani. Akiwaelezea Waislamu waliokusanyika kwa ajili ya sala ya Ijumaa Msikitini hapo, Ustaadh Mohammed alisema kuwa ni muhimu kwa Waislamu kufanya maandalizi ya Ramadhani kwa kujielimisha juu ya namna ya kuukabili mwezi mtukufu hasa kuelewa maana na makusudio ya funga, namna ya kufunga kwa kuzingatia masharti, mambo yanayobatilisha pamoja na Sunna zilizokokotezwa na Mtume (s.a.w.). Alisema kuwa Mtume (s.a.w.) ametufundisha namna iliyobora ya kuukaribisha funga ya Ramadhani, hivyo tunapaswa kufunga Sunna za Jumatatu na Al-khamisi pamoja na kuisoma Qur’an kwa wingi kama alivyotuagiza. Aidha, ustaadh huyo aliwanasihi Waislamu wajiepushe kabisa na mambo yote ya laghwi ambayo hupoteza swaumu kama vile kuangalia mpira, kucheza bao, karata, usoro, dhumma, drafti, sinema za kipuuzi n.k. Akisisitiza yaliyozungumzwa Ustaadh Kilewa Saidi akifafanua laghwi kuwa ni jambo lolote la kipuuzi ambalo hupoteza muda na kukasahaulisha kumkumbuka Allah (s.w.).
|
YALIYOMO
'White Paper ni ulaghai wa Serikali ya CCM' Na Mwandishi wetu Sheikh Omar Bashir awekwa rumande
Mpango wa 'Kupindua' uongozi
wa Bakwata: Masheikh Dar waitwa polisi kuhojiwa
Zahrau Day yatikisa Tanga
MAKALA: Hatuna haja ya maelekezo ya
yule aliyetufikisha hapa
Huduma za afya Kondoa haziridhishi
Tunahitaji 'UN' ya Waislamu!
Hoja binafsi: Wawekezaji watuondokesha makwetu Jamii inapokuwa soko huria...
Someni kwa ajili ya Allah - Sheikh
Baruti
Madrasa Al-Ii'Tiswamu
Al-Umaahaati Fiisabiililillah - Moro
Madrasat Hidayat Mbagala
Hali ya Uislamu Moro
Vijijini yazidi kuwa mbaya
Sheikh Masoud Mwinyi awaonya
Waislamu kuacha migogoro Babati
Tusikaribishe mfungo wa Ramadhani
kwa Vunja Jungu
'Acheni zinaa muepukane
na ukimwi'
Wavunja jungu watahadharishwa
Hoja/Uchambuzi:
Njia ya uzimani ni nyembamba,
waionao ni wachache
Habari:
Kesi ya Waislamu Mwembechai
yaahirishwa kwa mara nyingine
Kongomano la wanawake wa
Kiislamu Bagamoyo
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|