|
|
|
Na Twahir Rashid Upande! Mungu Mkubwa, Mungu Mkubwa, Mungu Mkubwa. Neno "Upande" ni lugha ya Kiswahili ambapo Kiarabu ni "Kibla" (2:177). Nalo neno hili kibla (upande wa kuelekeza nyuso zetu) limebatizwa na huitwa (Capital City) mji mkuu. Kibla! Mungu Mkubwa, Mungu Mkubwa, Mungu Mkubwa. Kauli hii "tunahitaji "UN" ya Waislamu", labda tusema "UN-dhana" ni ya madume matano yenye Turufu (VETO). Bali tunahitaji "UN" ya walimwengu wote. Na hapa tuingize fikra hii. Kwamba Mwenyezi Mungu hakuna kitu alichokiacha bila kukiweka wazi ndani ya kitabu chake (Quran). "UN ya Mataifa yote ilishaundwa na Mwenyezi Mungu na kUtiwa zege na Mtume Muhammad (s.a.w.) pale alipogeuzwa katika kibla akipendacho (2:144) nao ni upande wa msikiti mtakatifu, kwa kuacha upande (kibla) (kiini cha zamani) Baitil -Magdis. Na ni kwa nini alekee Makka? Basi fahamu kuwa "Nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu ni ile iliyoko Makka, yenye baraka na uongozi kwa ajili ya walimwengu wote." (3:96) Basi yule atakayekuwa maongozi yake hutokea mji huu, kwa maana wale wanaoelekea Makka kwa ajili ya maongozi ya maisha ya dunia yao na baraka; hao ndio wafuasi wa Mtume Muhammad (s.a.w.) (2:143).Kwa hiyo shibe na amani (106:3-4) watapata. Ili hali watakaoelekea mji mwingine usiokuwa huu(k.m. New York); njaa na khofu zitawasibu (106:3-4). Ndio Khaswa Mwenyezi Mungu atufanyiza Kampeni (anatuita)katika Nyumba (Ikulu) ya amani (10’25) - lakini watu leo tumefikishwa katika nyumba (Ikulu) ya Maangamizo (14:28) humo tukaagizwa kuwa watoto na moja kwa moja dini kuvurugwa (6:137). Kwa hiyo kuwa na Katibu Mkuu (Khalifa) ndio sawa. Ila Kofi Anan ahame kutoka Ikulu ya Maangamizo (14:28) (New York), ahamie Ikulu Kongwe (22:29) (Makka), kwani Katibu Mkuu (Khalifa) hana lake jambo ila kufuata Buku atakalolikuta katika Nyumba atakayosimama (2:125). Kwa hayo jua basi, Waislamu ni wale ambao mji wao mkuu (mji wanaowatajia watoto wao) ni Makka kwa hiyo Kofi Anan wao makao (ofisi) yake yapo Makka (27:91).Kinyume na hivyo ni kushirikisha (6"148). Ndio hivyo tunapo ambiwa turejee kwa Menyezi Mungu maana yake ni kwamba sasa hivi tupo katika uongozi wa Majumba (Ikulu) ya shetani (UN-New York) (ambavyo Ikulu hii imeshikana Ikulu yote ya kila nchi mpaka ofisi za vijiji). Kwa hiyo tutoke humo turejee katika (Ikulu ) ya Mwenyezi Mungu (UN-Makka). Na tayari UN-Makka ina ofisi zake mpaka Vijijini nayo ndio misikiti (72:18). Misikiti! Mungu Mkubwa, Mungu Mkubwa, Mungu Mkubwa. Ndugu yangu Said Rajab swali lako. Je! Waislamu wa dunia nzima, wakati haujafika tu wa kuwa na "UN’ ya Waislamu.....? Basi fahamu kuwa kizazi cha Israel kilichukuwa ahadi (2:40) (lakini) waliificha haki (2:42, 2:146) nayo ni kuelekea Makka (2:144, 2:147) kwa maongozi ya dunia nzima (3:96). Wao wakaasi na kuruka mipaka pale walipokataa (maongozi)ya Mwenyezi Mungu na kuwaua manabii. Kwa hiyo wakapingwa juu yao chapa ya dhila na umasikini (2:61) mpaka leo hawana nchi. Wamepigwa chapa ya dhila popote wanapokuweka, ila (kwa kushika)kamba (dini) ya Mwenyezi Mungu (uogozi wa UN-Makka) au kamba ya watu (UN-New York) (Amerika Inawasaidia).... (3:112) na imewasimika Palestine. Kwa hiyo juhudi zimefanyika kuficha ukweli huu wa UN ya walimwengu wote (3:96) ambayo ndiyo tengenezo la maisha ya watu (5:97) baada ya kuharibiwa (2:12-11). Hivyo maongozi ya watu (Serikali) Majeshi, Mashule, na Nyumba za Mungu (Makanisa, Misikiti, Mapagoda n.k.)vyote vimehujumiwa (17:64) zimeshikwa na shetani. Na kutumiwa kupotosha ukweli. Wanaostahiki kuamirisha misikiti (ofisi za Mwenyezi Mungu) kwa ajili ya uongozi khaswa (2:120) ni wale 1. Wanaomuamini Mwenyezi Mungu
Eh! Mola wangu, mimi ni mja wako
Na hivi imetimu ishirini na tano
Unyonge umekithiri, umasikini ndio usiseme. Manabii wa leo (Mbwechai) wauawa (2:61) neno la Mwenyezi Mungu kosa. Ilivyokuwa kwa mfalme wa Yemen ndivyo hivi leo. Mfalme wa Marekani kafanya
aliyoshindwa Mfalme wa Yemen na watu wote hata Saudia na Iran wana wajumbe
wa kudumu katika Kibla cha New York Wamegeuzwa bila kujua (40:63). Ni nguvu
ya mkono wako sasa tunayoienzi. Kwa sababu mfalme hupambana na mfalme mwenzake.
Watu wanakutaka sasa uwaongoze uwatoe katika giza uwapeleke katika Nuru
(2:257).
|
YALIYOMO
'White Paper ni ulaghai wa Serikali ya CCM' Na Mwandishi wetu Sheikh Omar Bashir awekwa rumande
Mpango wa 'Kupindua' uongozi
wa Bakwata: Masheikh Dar waitwa polisi kuhojiwa
Zahrau Day yatikisa Tanga
MAKALA: Hatuna haja ya maelekezo ya
yule aliyetufikisha hapa
Huduma za afya Kondoa haziridhishi
Tunahitaji 'UN' ya Waislamu!
Hoja binafsi: Wawekezaji watuondokesha makwetu Jamii inapokuwa soko huria...
Someni kwa ajili ya Allah - Sheikh
Baruti
Madrasa Al-Ii'Tiswamu
Al-Umaahaati Fiisabiililillah - Moro
Madrasat Hidayat Mbagala
Hali ya Uislamu Moro
Vijijini yazidi kuwa mbaya
Sheikh Masoud Mwinyi awaonya
Waislamu kuacha migogoro Babati
Tusikaribishe mfungo wa Ramadhani
kwa Vunja Jungu
'Acheni zinaa muepukane
na ukimwi'
Wavunja jungu watahadharishwa
Hoja/Uchambuzi:
Njia ya uzimani ni nyembamba,
waionao ni wachache
Habari:
Kesi ya Waislamu Mwembechai
yaahirishwa kwa mara nyingine
Kongomano la wanawake wa
Kiislamu Bagamoyo
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|