|
|
|
• Moto utalipuka wananchi waking’amua • Rais asiwe muweza
wa yote
Na Mwandishi Wetu MWANASIASA mkongwe nchini Bw. Christopher Kassanga Tumbo amesema kwamba utaratibu wa kuifanyia marekebisho Katiba kupitia White Paper huku wananchi wakitakiwa watoe maoni yao ni kuleta ulaghai. Akifafanua kauli yake hiyo, Balozi Kassanga Tumbo alisema kwamba ni kuwaghilibu wananchi kuwataka watoe maoni katika jambo ambalo hawatakuwa na kauli ya uamuzi. Alisisitiza kwamba maoni ya wananchi yangekuwa na maana kama hatimae pangekuwepo na kura ya maoni. Balozi Kassanga Tumbo ambaye alikuwa akizungumza katika kipindi cha Kiti Moto kama kilivyorushwa na ITV usiku wa Jumatano Desemba 3, mwaka huu, amesema kwamba White Paper kama utaratibu wa kuibadili Katiba una dosari kubwa mbili: Kwanza umevitenga vyama vingine vya siasa na pili wananchi wanaoulizwa hawana kauli ya uamuzi. Amesema utaratibu huu wa White Paper ni namna nyingine ya kuwaghilibu wananchi na akatahadharisha kwamba moto utakuja kulipuka pindi wananchi watakapotambua kwamba wamekuwa wakighilibiwa. Amezitaja ghilba nyingine ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali kwamba ni pamoja na kuwaundia wafanyakazi vyama ambavyo haviwakilishi matakwa yao wala kutetea maslahi yao. Ametaja majina ya NUTA, JUWATA, OTTU na TFTU kwamba ni majina tofauti lakini yanayowakilisha vyama vilivyodhibitiwa na CCM na serikali yake na hivyo kukosa nguvu ya kutetea maslahi ya wafanyakazi. Amehoji inakuwaje chama cha wafanyakazi kiongozwe na kada wa CCM. Bw. Kassanga Tumbo ambaye ni miongoni mwa waasisi na wapigania mfumo wa siasa wa vyama vingi nchini, amesema kwamba nao hivi sasa kama kambi ya upinzani wanawaelimisha wananchi na wana mapendekezo yao ya Katiba. Amesema yeye binafsi anapendekeza mfumo wa Shirikisho kwani ndio mfumo pekee unaozuia madikteta. Amesema kama wakuu wa mikoa na wilaya watachaguliwa na wananchi basi watawajibika kwao zaidi kisiasa kuliko hivi sasa. Aidha, alisema kwamba haifai Rais wa nchi kuwa na mamlaka makubwa na
kumfanya kuwa muweza wa yote. Hali hiyo amesema kwamba huzaa udikteta.
|
YALIYOMO
'White Paper ni ulaghai wa Serikali ya CCM' Na Mwandishi wetu Sheikh Omar Bashir awekwa rumande
Mpango wa 'Kupindua' uongozi
wa Bakwata: Masheikh Dar waitwa polisi kuhojiwa
Zahrau Day yatikisa Tanga
MAKALA: Hatuna haja ya maelekezo ya
yule aliyetufikisha hapa
Huduma za afya Kondoa haziridhishi
Tunahitaji 'UN' ya Waislamu!
Hoja binafsi: Wawekezaji watuondokesha makwetu Jamii inapokuwa soko huria...
Someni kwa ajili ya Allah - Sheikh
Baruti
Madrasa Al-Ii'Tiswamu
Al-Umaahaati Fiisabiililillah - Moro
Madrasat Hidayat Mbagala
Hali ya Uislamu Moro
Vijijini yazidi kuwa mbaya
Sheikh Masoud Mwinyi awaonya
Waislamu kuacha migogoro Babati
Tusikaribishe mfungo wa Ramadhani
kwa Vunja Jungu
'Acheni zinaa muepukane
na ukimwi'
Wavunja jungu watahadharishwa
Hoja/Uchambuzi:
Njia ya uzimani ni nyembamba,
waionao ni wachache
Habari:
Kesi ya Waislamu Mwembechai
yaahirishwa kwa mara nyingine
Kongomano la wanawake wa
Kiislamu Bagamoyo
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|