AN-NUUR 
Na.171 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 16 - 22, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
Madrasa: 

Goda Muslim School, Manzese 

  
Na Mwandishi Wetu 

  
GODA Muslim School, ni madrasa iliyoanzishwa mwaka 1994 ikiwa na wanafunzi 11 na mpaka sasa ina jumla ya wanafunzi 100. Kati yao wakiwa ni wasichana na wavulana. Pia madrasa hii ina walimu 5, wanaume 4 na mwanamke mmoja. 

Jengo la madrasa hii lipo ubavuni mwa nyumba ya Bw. Ally Salum. Kabla ya kuhamia katika jengo hilo, madrasa ilikuwa ndani ya nyumba ya mdogo wa Bw. Ally anayeitwa Bw. Omar Salum kwa muda wa miaka miwili.  

Baadaye ilihamia hapa ilipo sasa hivi kutokana na ufinyu wa chumba cha mwanzo na idadi kubwa ya wahitaji waliokua wanajitokeza kila siku. 

Uanzishwaji wa madrasa hii ulikuja baada ya Ustaadh Khamisi Omary kumaliza masomo yake Chuo cha Kiislamu cha Alharamain na kujiona kwamba anao wajibu wa kutoa elimu yake kwa jamii ya Kiislamu, ndipo akamuona Bw. Omar Salum kumuomba ampatie kijisehemu nyumbani kwake aanzishe darasa la vijana, kwa kuanzia na watoto wa Bw. Omar na vijana wa Kiislamu wa nyumba za jirani. 

Kwa bahati nzuri, darasa lilianza na kuendelea kwa mafanikio makubwa mpaka leo, na tayari Waislamu wa jirani wamejitolea uwanja ijengwe madrasa kubwa itakayochukua watoto wengi zaidi kutokana na kuridhishwa na maendeleo ya madrasa hiyo. 

Madrasa hii ina malengo ya jumla ya kuwaelimisha na kuwalea vijana wa Kiislamu kuanzia chekechea mpaka sekondari. Aidha, madrasa inalenga kuwaandaa vijana kuwa viongozi wa kutegemewa na jamii ya Kiislamu na taifa kwa ujumla. 

Ili kufikia malengo hayo, madrasa hii inatoa mafunzo yafuatayo: 

Qur’an, maarifa ya Uislamu, Lugha ya Kiarabu, Kiingereza, Kiswahili, Hesabati, Sayansi, Uraia, Tafsiri ya Qur’an, Tawhiid, Fiqh, Sira, Tajwid, Hifadhi, Historia, Jiografia pamoja na ufundi wa Typing, umeme na kilimo. 

Madrasa hii imepata mafanikio mengi tangu kuanzishwa kwake kutokana na mpangilio mzuri wa utoaji elimu pamoja na ujuzi wa kutosha wa walimu wake, vijana wingi wamehitimu Qur’an na Tafsiri wakiwa na umri mdogo. 

Vijana wanapata masomo ya pande zote, hivyo kuwafanya wanapokuwa mashuleni wanakosomea iwe ni marudio kwao na hivyo kuwepo katika nafasi 10 muhimu darasani. 

Kwa upande wa maadili, madrasa hii imefanikiwa kuwa na vijana wanaosimamisha swala 5, kudumu na vazi la stara popote walipo (wanawake) pia wanafunzi wawapo nyumbani na shuleni hutoa da’awa kwa wenzao wasiosoma chuo na wasioswali. 

Japo ni madrasa, imefanikiwa kuendesha madrasa kwa kufuata taratibu zote za kishule, ukiachilia mbali udogo wa eneo lao, kudhibiti nidhamu, mahudhurio na kuwahi, sare, ratiba za vipindi na mihula pamoja na utaratibu wa ada ya mwezi na michango. 

Kwa upande wa matatizo, madrasa hii kama zilivyo madrasa nyingine ina msururu wa matatizo ambayo yanahitaji misaada ya wafadhili na sadaka kutoka kwa Waislamu. 

Hakuna ushirikiano unaohitajika kwa wazazi, wengi wao wanaona haya ni mambo yanayotaka mashule, kwa hiyo baadhi yao huwahimiza watoto wao kuwahi, hawawanunulii sare, madaftari yakiisha wanawazungusha na maswali ya kuwahimiza stara na swala wanaona ni kazi ya walimu. 

Ada inayotozwa ya shilingi 1500 haitoshelezi posho za walimu 5, uendeshaji wa shule na shughuli za maendeleo ya shule. 

Lipo eneo la kujenga shule kubwa muda mrefu, lakini bado mpaka leo hajapatikana mfadhili wa kujenga wala msaada wowote kutoka kwa Waislamu. 

Mawasiliano na Madrasa ni kupitia Simu Nam. 126896, 128418 au 492993 kwa Katibu Zahra S. Saidi ambaye ni Katibu au Mwalimu Khamisi. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 

 TAHARIRI 
Serikali iwahurumie wananchi wake 

KUCHOMWA MOTO NYUMBA ZA WANANCHI: Nzasa wamtaka Mkapa awaonyeshe pa kwenda 
Na Mwandishi Wetu, Nzasa 

Mishikaki ya nguruwe Moshi yachomwa mbele ya Msikiti 
Na Mwandishi Wetu 

MAONI YETU: 
Je; ni halali kuchoma Kidungu cha mtu? 

Upimaji huu mpya ni wa nini 
Na Mwandishi Wetu 

TANGAZO LA HIFADHI YA MSITU WA KAZIMZUMBWI 

Ndoa si lengo, ni wasila wa kufikia lengo 
Na Bi. Zuhura Tajiri, Shinyanga 
 
Teknologia:
Jifunze kuunganisha Kompyuta
Na Hassan Omar

Makala:
Nani atakayewahoji Waheshimiwa hawa

Goda Muslim School, Manzese
Na Mwandishi Wetu

Utabiri sahihi wa kuibuka kwa Uislamu
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa

Historia ya mgogoro wa Nzasa
Na Mwandishi Wetu

DUMT watoa msaada kwa walioathirika Nzasa
Na Mwandishi Wetu

UCHOMAJI NYUMBA NZASA: Wafadhili wana mchango gani?
Na Mwandishi Wetu

Mafundisho ya Quran 
Kutoa pasipo masimango 

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe  

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita