|
|
| Upimaji
huu mpya ni wa nini
Na Mwandishi Wetu ZOEZI la kuchoma nyumba za wananchi huko Nzasa limekuwa likienda sambamba na upimaji wa eneo hilo na kuweka mpaka mpya. Upimaji huo unajumuisha kuchimba mashimo makubwa, kupaka rangi miti na kuweka maboya (beacon) mapya. Baadhi ya maboya mapya yaliyoyashuhudiwa Mwandishi wa Habari hizi yamepewa Namba. FD KZ 76 na FD KZ 77. Nyingine ni FD KZ 68, FD KZ 120, FD KZ 121 na FD KZ 122. Ambacho wanauliza wananchi ni je; upimaji huu mpya ni wa nini? Je, ni upanuzi wa mipaka ya Msitu, uandaaji wa eneo la amani au kinga (buffer zone) au ni kitu gani hasa. Kutaka kujua zaidi AN-NUUR iliwasiliana na Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki (Wizarani), Prof. Idd Saidi. Hata hivyo Prof. Idd alikataa kabisa kuzungumzia suala hilo la upimaji na kumtaka Mwandishi awasiliane na Mkuu wa Mkoa wa Pwani au Waziri. Baada ya kuelezwa kwamba Mhe. Waziri Zakia Meghji kaenda Sumbawanga AN-NUUR iliwasiliana na Katibu Mkuu, Bw. Luhanjo ambaye naye hakuweza kufafanua upimaji huo mpya ni wa nini. Ila Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Maliasili na Utalii alisisitiza kwamba upimaji huo mpya hauwezi kuwa ni upanuzi wa mipaka (extension) ya msitu kwani itakuwa ni kinyume cha sheria. Alisema kwamb a upanuzi ni lazima ufuate sheria ya misitu inayoagiza kutangazwa upanuzi huo katika gazeti la Serikali na kufuatwa taratibu nyingine zote zinazohitajika kisheria. Baadhi ya wafanyakazi wa Idara hiyo walioongea na Mwandishi wa Habari hizi kwa "sharti" la kutowataja japo kwa ishara tu, wamesema kwamba zoezi linalofanyika sasa hivi ni kupima kuweka mipaka na wakati huo huo, kuchora ramani. Lakini na wao hawajui endapo ramani hiyo mpya itakuwa ndiyo ramani ya Kazimzumbwe au ni eneo jipya linalotengwa nje ya mipaka ya msitu wa Kazimzumbwe. Haikuweza kufahamika mara moja ni kwa vipi Mkurugenzi wa Idara ya Misitu katika Wizara; ambaye pia ni Profesa wa Misitu akatae kuzungumzia upimaji huu na aagize aulizwe Mkuu wa Mkoa. Hata hivyo, alisema Profesa Iddi ilikuwa kwamba chanzo cha habari ni lazima kiwe kimoja ama Waziri au Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Kwa kuwa wananchi wanadai kwamba zilikochomwa nyumba zao ni nje ya mipaka ya msitu na upimaji na uwekaji mipaka mipya unaendelea kwa kasi, Serikali ieleze upimaji huu na mipaka hii ni ya nini? |
YALIYOMO
TAHARIRI Serikali iwahurumie wananchi wake KUCHOMWA MOTO NYUMBA ZA WANANCHI:
Nzasa wamtaka Mkapa awaonyeshe pa kwenda
Mishikaki ya nguruwe Moshi yachomwa
mbele ya Msikiti
MAONI YETU:
Upimaji huu mpya ni wa nini
TANGAZO LA HIFADHI YA MSITU WA KAZIMZUMBWI Ndoa si lengo, ni wasila wa kufikia
lengo
Makala:
Goda Muslim School, Manzese
Utabiri sahihi wa kuibuka kwa Uislamu
Historia ya mgogoro wa Nzasa
DUMT watoa msaada kwa walioathirika
Nzasa
UCHOMAJI NYUMBA NZASA: Wafadhili
wana mchango gani?
Mafundisho ya Quran
|