AN-NUUR 
Na.169 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 2 - 8, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
BARUA

Msiogope nguruwe na mbege, tembeleeni Rombo 

Ndugu Mhariri 

NAOMBA japo nafasi kidogo ili nipate kuwapa Waislamu harakati za hapa Rombo. 

Baada ya kupambana na mlokole aliyejiita Rashidi ambaye alimwaga maneno ya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa muda wa wiki mbili hivi. Punde kidogo wakaja Wasabato wakaweka sumu yao na kuwatosa watu mtoni kama vile kambale, walikaa muda wa wiki tatu. 

Kwa uwezo wake Allah (sw) wakafika vijana wa kikundi cha AL-MALLID kutoka Arusha kujibu shutuma za kutukanwa Mtume (saw). 

Ninachoomba kwenu Waislamu katika kila pembe, muweze kuitembelea sehemu hii ya Rombo ili kuihui kwani Waislamu wake bado imani zao hazijawa na msimamo. 

Mwisho napenda kuwashukuru vijana hawa wa AL-MALLID kwa kueweza kufikisha Da’awah katika sehemu hii ambapo ni mara ya kwanza kabisa Wahadhiri kufika sehemu hii ya Rombo. 

Kudra R. Mwindadi, 

Box 9 Tarakea, 

Rombo, Kilimanjaro. 


Profesa Kaisi ametoa mpya 

Ndugu Mhariri  

KATIKA makala yake ya toleo namba 027 la gazeti la Msema kweli, Profesa Kaisi amechambua hoja za Dokta Juma kwa umahiri mkubwa. Mimi natamani Msema kweli lipate hoja Maprofesa kama Kaisi, maana kwa watu wenye shule yao yanaigia akilini.  

Naomba pia kumshahihisha Profesa Kaisi kwamba tofauti ya Paulo na Muhammad (saw) haipimwi kwa suna za kuwa, mswaki, uturi na haya. Kwanza ametaja kuwa hizo ni suna, wanavitu vilivofardhishwa kwao na hizo sunna zao. Unabii ni wa kulazimishwa. Wafasili wa Bibilia walifanya kosa la makusudi kwa kuwaita wajumbe wa Yesu Mitume. 

Kuna tofauti kubwa kati ya wajumbe wa Yesu na wajumbe wa Mungu. Kwa Kiingereza wale waliotumwa na Yesu waliitwa Apostles na wale waliotumwa na Mungu huitwa Phophets. 

Wabangaizaji walipokosa maneno wakawaita wote Mitume. Profesa na wengine wote waisome Bibilia yote hawatakuta Paulo ameitwa Prophet. Kwa hali yoyote ilivyo hawezi kumlinganisha Prophet – Mtume wa Mungu na Apostle – sahaba wa Mtume wa Mungu. Katika Bibilia wamo mitume wa Mungu (Manabii) kama Muhammad (saw) hao ni kama vile Musa, Isaya,Yona, n.k. 

Waislamu pia wanao Apostles yaani wajumbe au masahaba wa mitume, hao ni kama vile Abubakari, Omari, Uthmani, Aliy, n.k. La msingi ni kujua kuwa alietumwa na Nabii huitwa Apostle na aliyetumwa na Mungu huitwa Prophet. Muhammad (saw) ni Prophet wa Mungu na Paulo ni Apostle wa Yesu. 

Yesu ni Mtume wa Mungu "Wakujuwe wewe Mungu wa pekee na wa kweli na Yesu uliyemtuma". (Yoh. 17:3 Asema Yesu: "Huyu ametumwa na Mungu wa pekee na wa kewli". 

Mungu Mwenyeenzi anamwambia Muhammad (saw) "Innaka Laminal’Mursalina ala Siraat Limustaqiyma" (Yaasini). Hakika wewe u-miongoni mwa Mitume walio katika njia ilionyooka. 

Kwa sababu hiyo Yesu tunamkubali kama Mtume lakini tunasema hana jipya. Maana yeye mwenyewe anasema: 

"Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au Manabii la, sikuja kuitangua bali kuitimiliza, kwa maana, amin nawaambieni mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka Yodi moja wala nukta moja ya Torati haita ondoka hata yote yatimie. Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni (Mat. 5:17). 

Waislamu wanazo sheria kama zile za Torati na wanazifuata. Paulo aliondoa hizo na Wakristo wamemuunga mkono wanadai Torati na sheria zake haina maana tena, wakati Yesu anasema wasifundishane kinyume na Torati. 

Kwa msingi huo Paulo hawezi kutambuliwa na Waislamu maana amemkataa Mtume Yesu, Torati yasema: "Na alaaniwe asieyaweka imara maneno ya Torati hii kwa kuyatenda. (Kumb. 27:26). 

Paulo yeye anafundisha kuwa wale wote walio na matendo ya sheria ( ya Torati) wako chini ya laana. (Wagalatia 3:10) Yaani waikatae Torati. Kama kweli Bibilia ni neno la Mungu wa milele isingewezekana Mungu aseme amelaaniwa asiyefuata Torati na Paulo anasema msifuate sheria za Torati mtalaaniwa. Halafu watu waache ya Mungu wafuate ya Paulo. Hapo kila mwenye akili timamu anaelewa hivyo. 

Kama Wakristo wanamwamini Mungu wa milele basi wanaamini pia kuwa maagizo yake ni ya milele na kwa watu wote. Kujifanya mtu wa Paulo bado si njia ya kuepuka hukumu kwa kutofuata Torati. 

Waislamu wana hakika na yakini ya mambo maana hiyo Qur’an yao imeweka wazi kuwa Yeyote atakaye mtii Mungu kwa imani ya moyo, kwa maneno ya kinywa na kwa matendo amefaulu. Pepo ni yake. 

Kimangale H.  

S.L.P. 605, 

Tanga. 


Duma msitishwe  

Ndugu Mhariri  

SINA tabia ya kuandika katika magazeti, ingawaje mimi ni msomaji mzuri sana wa gazeti lako. 

Kuna hii tabia iliyojengeka miongoni mwa watu ambao si Waislamu kuwalaumu Waarabu kwa chochote watakachofanya imma iwe kizuri au kibaya, Muarabu siku zote ataonekana mbaya tu. 

Kwa nini nimeamua kuandika barua hii kwenu. Ni kuwa naomba muwatanabaishe hao wanaowaona Waarabu kuwa ni wabaya, waelewe kuwa wana dhana mbaya. 

Hapa nchini kwetu, utakwenda mashariki na magharibi, kusini na kaskazini ya nchi hii, hutaweza kuona Waarabu wanafanya shughuli yoyote ya kueneza dini, na kama wapo basi ni wa kuhesabika. 

Lakini hebu tembea hivyo hivyo kama hapo juu na utaniambia utakutakana na Wamissionari wangapi. Jibu ni wengi sana, wengine unaweza kukutana nao mahali ambapo hata hungeamini kama kuna Mzungu angeweza kufika huko. 

Lakini kuonekana huko kwa Wazungu wanaoendesha dini mpaka vijijini, hakuna mtu anayesema chochote. Lakini kuonekana Waarabu huko Duma, Same tayari Wakatoliki wanapiga kelele oh tumewaona Wairan, Wairaq, Wasomalia na Wazanzibari, hivyo kwao huko tayari Wakatoliki wanapiga kelele. 

Mimi nawaomba Mhariri wa gazeti hili la Kiislamu nchini lipige kelele sana kuhusu tabia hizi za kuonekana kwa Waarabu watu wabaya sana na Ilhali Wamissionari walio tapakaa mpaka vijijini hili halionekani na hakuna anaelilalamikia hilo. 

Mwisho kabisa nawaombea Mungu Ndugu Waislamu wa Duma – Same waendelee kwa jitihada zote kwa Mungu mpaka wahakikishe kuwa eneo lao walipate lote na wasitishike kabisa kuomba misaada ya ndugu zao popote pale walipo bila ya kujali huyu ni Mpare, Mwarabu au Muhindi, nia na madhumuni yetu ni kusimamisha kamba ya Mwenyezi Mungu na kwa hilo hatutamuogopa yeyote yule. 
 

Wabilahi Taufiq 
Alhaj M.M. Mattaka, 

Dar es Salaam. 

  


Hongera kina mama wa Kiislamu 

Ndugu Mhariri 

NAOMBA nafasi japo kidogo katika gazeti lako hili la AN-NUUR ili niweze kuwapongeza akina mama wa Kiislamu nchini. 

Hali ya sasa hivi imekuwa ni mbaya sana katika jamii yetu kwa sababu ya kukiukwa maadili aliyotuwekea Allah (sw) ndio mana jamii yetu inaenda tenge. 

Hapoo hapo tunaona katika gazeti lako hili kurasa zimepambwa kwa picha nzuri za makongamano ya wanawake wa Kiislamu sehemu mbalimbali zikiwa zinavutia sana. 

Kutokana na hai hiyo, nawapongeza sana akinamama wa Kiislamu kuweza kufahamu wajibu wao katika jamii, Isha’allah Allah (sw) awajalie afya njema ili waweze kufikisha ujumbe wao barabara. 

Akina mama hawa nawaombeni waweze kufikisha ujumbe sehemu zote mijini na vijijini pamoja na matatizo ya usafiri na mengineyo yanayowapata. 

Akina mama wengine huku sehemu za vijijini tunakataliwa kutoka kwenda katika sehemu ambazo kuna kongamano mfano sehemu za mikoa ya Mara na Kagera hivyo jaribuni kutafuta njia ya kuweza kutusaidia angalau tufahamu haki zetu. 

Na sisi akina mama tukishapewa huo ujumbe tuupokee na kuutekeleza kwa vitendo sio tunabakia kuhesabu tu ni makongamano mangapi umeishahudhuria wakati huo kichwani hamna hata moja uliloambulia. 

Litakuwa ni jambo la kushangaza sana kongamano tunazihudhuria sana lakini jamii inabakia vile vile bila kuwa na mabadiliko yoyote. 

Hivyo nawaombeni sana akina mama tushikamane na hao wahadhiri wetu kwa pamoja kutekeleza yale yasemwayo katika hayo makongamano ili kutafuta radhi za Allah (sw). 

Aula Tinda, 

Karagwe. 


Elimu kwa wanafunzi wa Kiislamu Tanzania 

Ndugu Mhariri 

NATOA pongezi na shukrani nyingi za dhati kwa kazi yenu nzuri kwa kutuelimisha na kuufahamisha umma kuhusu mengi yatendekayo ulimwenguni pia hapa nchini, katika nyanja tofauti. 

Kwa leo maoni yangu ni kuhusu elimu kwa Waislamu. Ni zaidi ya miaka mitatu sasa kupitia gazeti lako hili la AN-NUUR tumekuwa tukitaarifiwa kuhusu wanafunzi wa Kiislamu waendao kupata elimu nje ya Tanzania, zikiwa ni nchi mbalimbali: Uchina, Uarabuni n.k. 

Swali langu ni je, elimu katika Uislamu imefaradhishiwa kina kaka tuu wa Kiislamu? Na pengine kina dada wanafahamu lakini wakanyimwa fursa hiyo? 

Ikiwa haki zao upande wa elimu yaani wake kwa waume, basi tutalisherehekea jambo hilo pindi tangazo la nafasi ya kwenda kusoma nje ya nchi kwa kina dada Waislamu litachapishwa katika gazeti letu la AN-NUUR. 

Ni matumaini yangu labda na wengine hasa kina dada wa Kiislamu watafurahia na kupongeza wazo hili. 

Sifa Hilali, 

C/o Mama Omari, 

S.L.P. 821 Kahama. 


Kwa nini iwe ‘Boy friend’ na isiwe ‘Husband?’

Ndugu Mhariri 

SIKU hizi kumekuwa na mijadala mbalimbali katika mashule ya sekondari na hata kwenye vipindi vya televisheni kama vile Sema kweli.n.k. 

Mijadala hii imekuwa ikizungumzia hasa msichana ambaye amefikia umri wa miaka 15 na kuendelea na kwamba bila ya kuwa na "Boy friend" msichana huyu ataathirika kisaikolojia na vile vile mpaka atakapofikia umri wa miaka 18 bila ya kufanya tendo la ndoa (sexual Interrose) She can’t survive. 

Katika mijadala hii huwa wanatoa sababu zao za kisayansi ambazo hazina hata nguvu. 

Inasikitisha kwamba mijadala hii inaungwa mkono na walimu na hata baadhi ya wazazi wetu. 

Sasa ndipo ninapojiuliza kama kweli wanafahamu kuwa kuna athari fulani sicologically kwa nini iwe ‘Boy friends’ na isiwe "Husband?" 

Kwa mtazamo wangu ninaona kwamba hapa kuna kitu fulani kimefichwa hasa kwa upande wa mabinti wa Kiislamu ambao ni wenye kujitahidi katika kufuata sheria za Uislamu ili wazipuuze na kuingia katika mifumo ya Kitwaghuti. 

Kwa mtazamo huo ninaweza kusema wamefanikiwa kwa kiasi fulani kwani baadhi ya mabinti wenye majina makubwa makubwa ya Kiislamu wamekubaliana na hayo na wameamua kujitafutia wazinifu wenzao ili waweze kuishi kama wanavyodai. 

Mwisho ninapenda kuwausia mabinti wa Kiislamu ikiwa ni pamoja na kuisia nafsi yangu ya kwamba tusijiingize kwenye mambo yasiyotuhusu na tuwe ni wenye kufuata maamrisho ya Allah (sw) na tujitahidi kuepukana na makatazo yake kwani mijadala yote hii inaanzishwa kwa sababu yetu. 

Maadui zetu wanatafuta kila njia ya kutupiga vita, wanashindwa kwa hiyo wanaamua kutupiga vita vya kifikra kwani hijjab tuvaazo zinawatisha. 

Na pia mbona wazazi wetu mpaka leo wanaendelea kuishi na wala hawakuwa na ‘Boy friend’ basi wangeanza kufa wao au kuathirika kisaikolojia. 

Rahma Salum, 

Dar es Salaam. 
 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 TAHARIRI 
Majeshi ya nje kupelekwa Lesotho: Je, ni sera za Nguvumali? 

Nyumba ya Wakfu yageuzwa  Baa Dar 
Na Mwandishi Wetu 

‘VAT’ yaingia Bakwata Same 
 Na Mwandishi Wetu 

Mchungaji asema hakuna mihadhara ya kashfa 
 Na Muhibu Saidi 

Maoni yetu: Masheikh tupeni Fatwa 

Safari yangu Ufini 
Ustaadh Ka-Batembo 

Unyanyasaji wa kidini mashuleni, vyuoni ukomeshwe 
Na Abuu Afahah 

Wanaume toeni haki za wanawake 
Na Zabibu Iddi Ng’onda Box 78, Mwadui 

MAONI: Yesu ni yule yule Isa 
Na Saleh Ngoi 

Hatuna uwezo wa kuwapinga manabii 
Na Elia Batendi, S.L.P. 538, DSM 

Ukoloni mwingine unaingizwa nchini? 
Sheikh Thabit H. Mbago,S.L.P. 21486,DSM 

Khatamy ni ‘Gorbacheiv’ mwingine? 
Na Athman Rajab 

Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo kwa maneno 
Mwandishi: Maalim Ali Bassaleh 

AN-NUUR  lina chuki na Wakristo 
Na Charles Kamuhabwa, DSA Mtwara 

Msiiparamie ovyo Biblia 
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa 

Yaliyosemwa na viongozi wa dini juu ya idadi ya watu 1989 
Na Rajab Rajab 

Uislamu ulivyoingia Zanzibar -2 

Waislamu Moro watakiwa kutoyumba 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Wanawake Masasi wawataka Masheikh kutangaza sheria za Allah 
Na Muhibu Saidi, Masasi 

Ugaidi na Uislamu siyo kitu kimoja – Sheikh Jongo 
Na Bakari Musa 

Sheikh Abbas awataka wananchi Dodoma waepuke upuuzi 
Na Abu Zubair, Dodoma 

Vijana watakiwa kujiepusha na ‘vijiwe’ 
Na Badru Kimwaga 

Mafundisho ya Quran 
Kutoa katika njia ya Allah: Al-Baqarah aya   261-263 

Barua za wasomaji 

Mashairi 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Magonjwa yanayoathiri lishe 
  

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita