|
|
| Hatuna
uwezo wa kuwapinga manabii
Na Elia Batendi, S.L.P. 538, DSM KWANZA nakupongeza kwa kutokuwa na ubaguzi kwa wasomaji wako, hivyo naomba nafasi niwasiliane na mtu ambaye yeye ameniita kuwa ni rafiki yake kwa majadiliano ya kidini Bwana Muhibu Said. Bwana Muhibu Said kuniita ‘rafiki’ sijui ametumia kigezo gani kwani Qur’an yake inamwambia asinifanye kuwa rafiki (Al Maidah 51) ila mimi ndiyo ninayo haki ya kumwita rafiki kwani Injili yangu inaniamuru nimwite hivyo yeye na wenzake (Mathayo 5:43-48). Pamoja na hayo, katika barua yangu katika gazeti hili toleo la Agosti 23, 1998, nilimpinga Bw. Muhibu na mwenzake kwa kuwazulia Wakristo uongo kuwa wao ndio walioanza kumwita Yesu Mungu au Mwana wa Mungu. Pia nilimpinga aliposema Mtume Paulo ndiye aliyezua kuwa Yesu kafa halafu kafufuka na kwamba Yesu haujui Ukristo kwa kuwa alikuwa Muislamu. Mimi nilimjibu kuwa Yesu aliitwa MUNGU na Manabii na siyo Wakristo, sisi hatuna uwezo wa kuwapinga hao Manabii. Nilitoa ushahidi wa maandiko kama ifuatavyo: Isaya 9:6 Ataitwa Mshauri wa ajabu, Mfalme wa amani, MUNGU mwenye nguvu. Isaya 40:3 Yohana atayarishe njia ya Bwana Mungu wetu, Isaya 7:14 Ataitwa Imanuel – Mungu pamoja na sisi, Ezekiel 44:1-2 Mlango huu wa mashariki atapita Bwana Mungu – Yesu alipita lango hilo la Yerusalemu akiwa amepanda mwana punda (Mathayo 21:10). Anauwezo wa kusamehe dhambi – Anayesamehe dhambi ni nani? (Luka 5:24) Ni Alfa na Omega – ((Ufunuo 22:12) Alfa na Omega ni nani? Haya yote hayakusemwa na Wakristo. Kuhusu kufa na kufufuka kwa Yesu, Manabii ndio waliosema na ikatokea kweli soma Zakaria 12:10, Isaya 58:10, Zaburi 34:20, Zaburi 16:10, Daniel 9:26 n.k. ya nini kumsingizia Mtume Paulo uongo? Kuhusu Yesu kuwa niMuislamu na haujui Ukristo nayo pia ni uzushi. Ingawa Qur’an inasema Manabii wote walikuwa Waislamu lakini inatatanisha inaposema kuwa Mtume Muhammad (saw) ndiye Muislamu wa kwanza (Al An-am 14) Nabii Mussa naye tunaambiwa ni muumni wa kwanza (Al Aaraf 143) sasa kama ni hivyo Nabii Adamu ni Muislamu wa ngapi? Yesu hakuwa Muislamu ndiyo maana aliagiza lianzishwe Kanisa tubatizwe, ndoa mke mmoja mme mmoja, yeye ni chanzo cha uhai (Yoh. 5:26) Yeye ataabudiwa sawa na Baba (Yoh. 5:23) n.k. Mafundisho haya siyo ya Kiislamu. Rafiki yangu Muhibu baada ya kushindwa hoja akarukia hoja nyingine kuwa yeye anafuata Injili ya waliotahiriwa siyo ya wasiotahiriwa (Gal. 2:6-8), lakini yampasa ajue kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mfanya sheria, hatuna uwezo wa kumuuliza kama udongo usivyokuwa na uwezo wa kumuuliza anayefinyanga wafanya nini? (Isaya 45:9). Lakini Mwenyezi Mungu ametutaka tukayajue majira ya sheria zake zinapobadilika kama ndege wanavyojua majira yao (Yeremia 8:7 au Luka 12:54-56). Tangu kuumbwa kwa dunia, Mwenyezi Mungu ameweka, kuziondoa au kuzirudisha sheria mara kadhaa, kwa mfano, vyakula, hapo zamani kuleni vyote (Mwanzo 9:1-4). Baadaye msile vyakula fulani (Walawi sura ya 11) sasa kuleni vyote (Luka 10:8). Kuchinja sadaka: Zamani chinjeni wanyama kwa toba (Wal. 5:6-13) sasa hakuna kuchinja, Yesu amechinjwa inatosha (Mathayo 26:28, Ebr. 10:4-9). Kutawadha: Zamani kutawadha (Kutoka 30:17-21) sasa hakuna haja (Ebr. 9:10). Kutahiri: Zamani hakuna kutahiri, baadaye kutahiri (Mw. 17:11-4) Sasa hakuna haja (Rumi 2:30). Kwa bahati mbaya, Mayahudi na Waislamu hawajui kusoma majira ya Mwenyezi Mungu. Mayahudi walishindwa kusoma ujio wa Masihi hadi leo wanangoja na kushika Sabato ambayo imekomeshwa (Hosea 2:11). Waislamu nao bado wanashika sheria za zamani za mwandamo wa mwezi ambao Mungu amezikomesha. (Hosea 2:11) |
YALIYOMO
TAHARIRI Majeshi ya nje kupelekwa Lesotho: Je, ni sera za Nguvumali? Nyumba ya Wakfu yageuzwa Baa
Dar
‘VAT’ yaingia Bakwata Same
Mchungaji asema hakuna mihadhara ya
kashfa
Maoni yetu: Masheikh tupeni Fatwa Safari yangu Ufini
Unyanyasaji wa kidini mashuleni, vyuoni
ukomeshwe
Wanaume toeni haki za wanawake
MAONI: Yesu ni yule yule Isa
Hatuna uwezo wa kuwapinga manabii
Ukoloni mwingine unaingizwa
nchini?
Khatamy ni ‘Gorbacheiv’ mwingine?
Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo
kwa maneno
AN-NUUR lina chuki na
Wakristo
Msiiparamie ovyo Biblia
Yaliyosemwa na viongozi wa dini juu
ya idadi ya watu 1989
Uislamu ulivyoingia Zanzibar -2 Waislamu Moro watakiwa kutoyumba
Wanawake Masasi wawataka Masheikh
kutangaza sheria za Allah
Ugaidi na Uislamu siyo kitu
kimoja – Sheikh Jongo
Sheikh Abbas awataka wananchi
Dodoma waepuke upuuzi
Vijana watakiwa kujiepusha
na ‘vijiwe’
Mafundisho ya Quran
Chakula na Lishe
|