AN-NUUR 
Na.169 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 2 - 8, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
‘VAT’ yaingia Bakwata Same

Kusoma Khitma sh. 5000 

Wacheza disko badala ya Maulid 

Na Mwandishi Wetu 

BAKWATA wilayani Same imepandisha gharama za huduma zake inazotoa kwa waumini katika kile kinachoonekana kama juhudi za kukabiliana na hali ngumu ya maisha. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Sheikh wa Wilaya, Sheikh Mustafa Mohammed kwa waumini, gharama za kusomewa Khitma na Maulid zimepanda kutoka shilingi 1000 na kuwa shilingi 5000. 

Aidha, huduma ya kusomewa ‘tatu’ baada ya mazishi itakuwa shilingi 5000 vile vile. 

Sheikh Mustafa akiongea katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa mjini Same, alisema kuwa huduma ya kufungiwa ndoa itakuwa shilingi 5000 (hizi ni mbali na cheti cha ndoa cha serikali). 

Hatua hii ya ofisi ya Bakwata kupandisha gharama ya huduma hizi muhimu kwa jamii zimelalamikiwa na waumini wengi mjini hapa hasa ikizingatiwa hali halisi ya kipato cha wananchi. 

Wengi wamekuwa wakikejeli ongezeko hilo kwa kuliita ‘VAT’ na kusema heri ya ‘VAT’ ya serikali ambayo ni 20% wakati ya Bakwata ni asilimia mia nne (400%). 

Uchunguzi wa gazeti hili umeonyesha kwamba tayari athari zimeshaanzakujitokeza ambapo watu waliokuwa wamepanga kufanya shughuli mbalimbali wamezifuta. 

Mama mmoja, Mwajuma Juma aishie eneo la Majevu jirani na hospitali ya wilaya alishindwa kufanya Maulidi yake baada ya kukosa shilingi 5000 za kulipa ofisi ya Bakwata. 

Mama huyo alikuwa amenuia kusoma Maulidi kumshukuru Mungu baada ya mtoto wake aliyekuwa amepata ajali kupona. 

Kushindwa kupata elfu tano hizo, mama huyo alifanya tafrija ndogo ya chai kwa majirani na ndugu zake. Hata hivyo kwa kukosekana Maulidi vijana hawakuona mantiki ya tafrija hiyo kufanywa kimya kimya, kwahiyo wakaiteka nyara na kupiga disko. 

Baadhi ya majirani Waislamu nao hawakuridhika na hali hiyo ya kuigeuza hafla ya kumshukuru Mungu kuwa ya disko, walimuomba mama muhusika disko lisimamishwe wasome dua, ambapo walisoma. 

Uchunguzi zaidi umebaini kwamba Waislamu mjini Same wanaandaa utaratibu wao wa kuendesha shughuli zao za Khitma, Dua, Maulidi na ndoa kupitia taasisi nyingine za Kiislamu ambazo haziwatozi mapato. 

Kwa ujinga baadhi ya waumini wamekuwa na fikra potofu kwamba ibada zao na mambo kama mazishi, kuozesha, dua, maulidi n.k. hayawezi kuswihi mpaka yafanywe na Sheikh maalum au chombo maalumu cha kidini. 

Hali hiyo imewapelekea wanaokabidhiwa jukumu la kuzifanya shughuli hizo kuweka viwango vya malipo ambavyo vinajenga hisia za kujali chumo zaidi kuliko huduma. 

Malalamiko ya Waislamu yatokanayo na hali hii yataondoka tu pale Waislamu watakapo elimika wajue kwamba wanaweza kumwombea dua maiti wao bila ya kumsubiri Sheikh maalum na kwamba Walii anayeozesha binti ni baba mzazi (au kaka, babu nk) na wala sio Sheikh wa taasisi fulani. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
TAHARIRI 
Majeshi ya nje kupelekwa Lesotho: Je, ni sera za Nguvumali? 

Nyumba ya Wakfu yageuzwa  Baa Dar 
Na Mwandishi Wetu 

‘VAT’ yaingia Bakwata Same 
 Na Mwandishi Wetu 

Mchungaji asema hakuna mihadhara ya kashfa 
 Na Muhibu Saidi 

Maoni yetu: Masheikh tupeni Fatwa 

Safari yangu Ufini 
Ustaadh Ka-Batembo 

Unyanyasaji wa kidini mashuleni, vyuoni ukomeshwe 
Na Abuu Afahah 

Wanaume toeni haki za wanawake 
Na Zabibu Iddi Ng’onda Box 78, Mwadui 

MAONI: Yesu ni yule yule Isa 
Na Saleh Ngoi 

Hatuna uwezo wa kuwapinga manabii 
Na Elia Batendi, S.L.P. 538, DSM 

Ukoloni mwingine unaingizwa nchini? 
Sheikh Thabit H. Mbago,S.L.P. 21486,DSM 

Khatamy ni ‘Gorbacheiv’ mwingine? 
Na Athman Rajab 

Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo kwa maneno 
Mwandishi: Maalim Ali Bassaleh 

AN-NUUR  lina chuki na Wakristo 
Na Charles Kamuhabwa, DSA Mtwara 

Msiiparamie ovyo Biblia 
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa 

Yaliyosemwa na viongozi wa dini juu ya idadi ya watu 1989 
Na Rajab Rajab 

Uislamu ulivyoingia Zanzibar -2 

Waislamu Moro watakiwa kutoyumba 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Wanawake Masasi wawataka Masheikh kutangaza sheria za Allah 
Na Muhibu Saidi, Masasi 

Ugaidi na Uislamu siyo kitu kimoja – Sheikh Jongo 
Na Bakari Musa 

Sheikh Abbas awataka wananchi Dodoma waepuke upuuzi 
Na Abu Zubair, Dodoma 

Vijana watakiwa kujiepusha na ‘vijiwe’ 
Na Badru Kimwaga 

Mafundisho ya Quran 
Kutoa katika njia ya Allah: Al-Baqarah aya   261-263 

Barua za wasomaji 

Mashairi 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Magonjwa yanayoathiri lishe 
  
 

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita