AN-NUUR
Na.157 Rabi' Awal 1419, Julai 10 - 16, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Makala

Elimu ya ngono yapenyezwa tena Zanzibar 

Na Saidi Mzee 

Somo la elimu ya ngono limepenyezwa tena Zanzibar baada ya mpango huo kusita kwa muda kutokana na mshikamano wa wananchi wa visiwa hivi kupinga kusomeshwa kwa somo hilo maskulini. 

Kwa mujibu wa muhutasari mpya wa somo la viumbe uliotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa la Tanzania, somo la ngono limejumuishwa kama ni mada ndogo ambapo wanafunzi wa kidato cha pili watakiwa wakisomeshwa mambo mbalimbali yanayohusiana na ngono. 

Mpango huu wa elimu ya ngono uliwahi kuletwa Zanzibar mnamo mwaka 1992 ambapo pamoja na juhudi kubwa iliyofanywa na Wizara ya Elimu wakati huo, zikiwemo za kuwashawishi masheikh waukubali mpango huo, ulishindikana baada ya wananchi wa Zanzibar kwa umoja wao kuipinga elimu hiyo hatua ambayo ilipelekea viongozi wa serikali kukiri kwamba elimu ya ngono ni jambo la hatari ambapo lisipoangaliwa kwa makini linaweza kusababisha madhara kwa jamii. 

Mheshimiwa Mapuri kusema kwamba Zanzibar haitokubali kuwa maabara ya majaribio. Haikudhaniwa kwamba Mheshimiwa Mapuri aliyasema hayo kwa lengo la kukipigia chama chake wakati ule kikijiandaa kwa uchaguzi bali iliaminika alikuwa akikusudia kulinda maadili na utamaduni wa Mzanzibar. 

Pamoja na Zanzibar kuwa sio nchi ya kidini lakini imekuwa ikilinda utamaduni wake kwa lengo la kuhakikisha kwamba kizazi pamoja na wageni wanaufahamu utamaduni halisi wa visiwa hivi hivyo kuleta mambo ambayo ni kinyume na utamaduni wake ni kutaka kusababisha ghasia zisizo za lazima. 

Pengine kabla ya kuelezea kwa undani wa athari ya elimu hiyo ni vyema kama tungeelezea ni kwa vipi mpango huo wa elimu ya ngono ulifikiwa kuwekwa katika muhutasri wa masomo ya baraza la mitihani Tanzania. 

Mpango huu ulianza kuingizwa Zanzibar mapema mnamo miaka ya themanini kwa kupewa majina mbali mbali kama vile family life education, environmental education n.k. 

Lengo kuu la mradi huu ikiwa ni kuwafundisha wanafunzi jinsiya kufanya "ngono salama. 

Ujanja mwingine uliotumika ni kupitisha masomo hayo katika mpango wa kudhibiti uzazi ulio chini ya UNFPA. 

Kulingana na jarida la DEV NEWS Namba 3 la Aprili 1990, Uk. 8 Tanzania ni nchi iliyopewa kipaumbele na shirika hilo la UNFPA na limekuwa likiipatia misaada tokea mapema katika miaka ya sabini. 

Mnamo Desemba, 1989 shirika hilo liliipatia Tanzania msaada wa dola milioni 3.7 kwa njia ya ufundi, ushauri, mafunzo, vifaa vya kuzuia mimbari n.k. Kutokana na misaada hiyo Tanzania ilitangaza rasmi mnamo Februari, 1990 mjini Dar es Salaam kuwa imeanza mpango wa kudhibiti kizazi kwa jina la Natural Family Planning Programme kwa msaada wa dola milioni 7.23 kutokashirika hilo. 

Ni kipindi hiki hiki Zanzibar kwa upande wake iliwasiliana na UNFPA ikilalamikia kuhusu wanafunzi wengi wanaopata mimba nje ya ndoa wakiwa masomoni na hatimaye kushindwa kuendelea na masomo UNFPA ilitumia fursa hii kwa kuishauri Zanzinbar kuanzisha elimu ya ngono kwa upande mmoja na kutawanywa kwa nyenzo za kuzuia mimba (kondomu) kwa upande mwengine. 

Mabingwa wa shughuli hii walioko Marekani kupitia kituo chao cha Margaret Sanger walihusishwa na UNFPA katika mpango huu mpya. 

Wawakilishi wa mashirika haya mawili walifika Zanzibar na kuanza kushawishi Wizara ya Elimu ya hapa ianze haraka kufundisha somo hilo katika maskuli yake. 

Vitabu vya mihutasri na vya rejea vilianza kuchapishwa na semina mbali mbali ambazo washiriki wake walikuwa wakilipiwa marupurupu makubwa ziliendeshwa katika sehemu mbali mbali. 

Miongoni mwa watu walioshirikishwa katika hatua za mwisho za mradi huo ni Masheikh ambao lau wangekubali Wizara ingetangaza kwamba hata viongozi wa dini wameupitisha mradi huo hivyo hawaoni kwa nini somo hilo lisifundishwe maskulini. 

Bahati ya mambo masheikh hao baada ya kuipitia mihutasari ya somo hilo walikataa katakata kusomeshwa kwa somo hilo maskulini. 

Masheikh hao walidai wapatiwe mifano ya nchi ambazo zimesaidiwa kuondosha tatizo lao kwa kutumie njia ya elimu hiyo ya ngono. 

Kutokana na kukataa huko kwa masheikh kusomeshwa kwa somo hilo Serikali ilitahadharisha Wizara husika kuhusu kupokea mawazo kutoka nje yanayohusu utekelezaji wa mradi huo. 

Pengine baada ya kitengo hicho cha Magareth Sanger kushindwa kuanzishwa elimu hiyo Zanzibar pamoja na kutumia mamilioni ya shilingi na dola kutokana na mshikamano wa wananchi wa Visiwa hivyo, ndiyo kitengo hicho kikaanzisha harakati zake kupitia serikali ya Tanzania ambapo wameweza kuishawishi hadi kukubali kuijumuisha elimu hiyo katika masomo ambayo yatalazimika kufanywa mitihani na wanafunzi wote wa Tanzania, wakiwemo pia wale wa Zanzibar ambao wazee wao na masheikh walipinga vikali juu ya watoto wao kusomeshwa elimu hiyo. Kwa vile watakaoendesha mradi huu wa elimu ya ngono ni wale wale walioondoka Zanzibar baada ya kushindwa kutekeleza mradiwao ni rahisi kuamini kwamba mihutasari itakayotumika ni katika kiongozi kilichotayarishwa kwa ajili ya Wizara ya Elimu ya Zanzibar ambacho naamini kabisa ndicho hicho hicho kinachotumika Tanzania, ambayo yanasema: 

"This manual is the product of many people experience. It’s author is a specialist in family life/sex education curriculum development, a certified conselor and educator in human sexuality, a doctoral candidate in public administration, trained in cultural anthropology……" 

April 1992 Shirley Oliver 

Director, Domestic and International Operation, Parent Education Program Project Consultant/Trainer Margaret Sanger Centre. 

Nukta muhimu ambayo mwana mama huyo aliizungumza ni kwamba Zanzibar ni miongoni mwa nchi ambazo zimeingizwa mkumboni kusomesha elimu hii ya ngono. Nchi ambazo tayari zinasomesha elimu hii ukiwacha Tanzania ni zile zenye Wakristo wengi tu. Hakuna nchi hata moja duniani ya Kiislamu japo kwa jina tu ambayo imekubali kusomesha elimu hii. Pia ikumbukwe kwamba hakuna sehemu yoyote ya dunia ambapo elimu hii imesaidia japo kwa asilimia moja tu (1%) maelekezo ni katika hali ile ile ya kuingiza Zanzibar katika mkumbo wa elimu hii ndiyo Baraza la Mitihani la Taifa ambalo kisheria ni la Muungano limeweza kuingiza elimu hiyo ya ngono katika mihutasari yake. Mama Shirley kwa kauli yake anapinga kwamba elimu ya ngono ni tofauti na elimu ya maadili pale anaposema kwamba elimu ya familia (maadili) ni jina jingine tu la elimu ya ngono. "It’s author is a specialist in family life/sex education…" 

Kwa upande wa Zanzibar mazingira yaliyopelekea kukataliwa kwa elimu hiyo ya ngono tunaamini kwamba bado yapo na yataendelea kuwepo hivyo tunaiomba Wizara ya Elimu itumie nguvu zake zote kuhakikisha kwamba elimu hiyo haifundishwi ndani ya Visiwa hivi. 

  
Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Maoni yetu: Prof. Juma Kapuya, vipi Muislamu usijue agenda za Waislamu? 

Hatimaye Mzee Katambo, Chata waachiwa
Na Mwandishi wetu

Polisi Newala wajenga Msikiti 

Sheikh Bafadhil aitaka Bakwata iwe mtetezi wa Waislamu
Na mwandishi wetu

Makala: Uinjilisti wa Mbuni haufai
Na Rajabu Mbambwa, Kigoma

Mussa Katambo: Mzee aliyewekwa rumande kwa kuandaa mihadhara

Ukweli usiachwe 

Makala: Elimu ya ngono yapenyezwa tena Zanzibar 
Na Saidi Mzee 

Arusha wasema: Hongera Mhe. KK kwa kuwa mfano mwema 
Na Hussein M.,  Arusha 

Wanawake Songea kuandaa maonesho 
Na. Jumah Mbwana, Songea 

Kesi ya mgogoro wa Ardhi
Na. Mustafa Adam 

AN-NUUR marufuku gerezani? 
Na Mwandishi Wetu 

Waislamu Karagwe wadai kusalishwa na imamu asiyejua kutawadha 
Na. Abu Abdallah 

Ofisi mpya za Rabita 
Na Mwandishi Wetu

Barua za wasomaji

Habari za Madrasa

Masomo 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita