AN-NUUR
Na.157 Rabi' Awal 1419, Julai 10 - 16, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
. AN-NUUR marufuku gerezani? 

Na Mwandishi Wetu 

MAGEREZA ya Keko na Segerea yamedaiwa kuzuia gazet la ANU-NUUR kuingia gerezani kwa sababu zisizofahamika. 

Watuhumiwa walioachiwa hivi karibuni wamesema kwamba walipokuwa mahabusu katika magereza hayo waliruhusiwa kupokea magazeti yote kutoka kwa jamaa zao ispokuwa AN-NUUR

"Hata magazeti ya Kiongozi na Msema Kweli yanaruhusiwa gerezani lakini AN-NUUR haliruhuisiwi", wamedai watuhumiwa hao. 

Haikuelezwa sababu hasa za kuzuiliwa gazeti hili gerezani lakini habari ambazo hazikuweza kuthibitishwa zimefahamisha kwamba baadhi ya maaskari wamesikika wakisema kuwa AN-NUUR gazeti la uchochezi na kwamba linapigwa marufuku. 

Jitihada za kuwaona wahusika wakuu wa magereza hayo kuhusiana na suala hili, hazikuweza kufanikiwa. 

  

Waislamu Karagwe wadai kusalishwa na imamu asiyejua kutawadha 

Na. Abu Abdallah 

WAISLAMU wa Kata ya Kituntu, Wilaya ya Karagwe, Mkoani Kagera wameilalamikia ofisi ya BAKWATA Mkoa wa Kagera kufuatia kitendo cha ofisi hiyo ikishirikiana na ofisi ya Wilaya kuwachagulia viongozi wanaodai hawajui hata kutawadha na kusoma suratul fatiha. 

Alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi uchaguzi huo ulizingatia vigezo gani. Mmoja wa viongozi wa BAKWATA ajilibu kuwa waliochaguliwa ni BAKWATA damu. 

Waumini wa Karagwe wamedai wapo katika hatua za mwisho kuwakilisha malalamiko yao kwa Mufti wa BAKWATA Sheikh Hemed Bin Jumaa bin Hemed Jumaa. 

  
Ofisi mpya za Rabita 

Na Mwandishi Wetu 

OFISI za Rabita - Muslim World League (Tanzania) zimehamia katika ofisi za International Islamic Releaf Organization (IIRO) MTAA WA Uhuru na Congo. 

Hatua hii inafuatia kuteuliwa kwa Alhaj Hassan Mnjeja kuwa mkurugenzi mpya wa Ratiba (T). 

Sheikh Muhammad Rukara Khalfan, mkurugenzi wa zamani amehamishiwa Gabon. 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Maoni yetu: Prof. Juma Kapuya, vipi Muislamu usijue agenda za Waislamu? 

Hatimaye Mzee Katambo, Chata waachiwa
Na Mwandishi wetu

Polisi Newala wajenga Msikiti 

Sheikh Bafadhil aitaka Bakwata iwe mtetezi wa Waislamu
Na mwandishi wetu

Makala: Uinjilisti wa Mbuni haufai
Na Rajabu Mbambwa, Kigoma

Mussa Katambo: Mzee aliyewekwa rumande kwa kuandaa mihadhara

Ukweli usiachwe 

Makala: Elimu ya ngono yapenyezwa tena Zanzibar 
Na Saidi Mzee 

Arusha wasema: Hongera Mhe. KK kwa kuwa mfano mwema 
Na Hussein M.,  Arusha 

Wanawake Songea kuandaa maonesho 
Na. Jumah Mbwana, Songea 

Kesi ya mgogoro wa Ardhi
Na. Mustafa Adam 

AN-NUUR marufuku gerezani? 
Na Mwandishi Wetu 

Waislamu Karagwe wadai kusalishwa na imamu asiyejua kutawadha 
Na. Abu Abdallah 

Ofisi mpya za Rabita 
Na Mwandishi Wetu

Barua za wasomaji

Habari za Madrasa

Masomo
 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita