AN-NUUR
Na.157 Rabi' Awal 1419, Julai 10 - 16, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Wanawake Songea kuandaa maonesho 

Na. Jumah Mbwana, Songea 

VUGUVUGU la maonesho ya mavazi ya Wanawake wa Kiislamu (Hijab) mjini Songea linazidi kupamba moto. 

Maonesho hayo ambayo yatafanyika Julai 25, 1998 mjini Songea ni ya aina yake na ya kwanza kufanyika hapa nchini. 

Waandaaji wa maonesho hayo Ofisi ya AL-MALLID Kanda ya Kusini yenye Makao yake mjini hapa wamesema maonesho hayo yatawashirikisha Wanawake kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo idadi yao inakadiriwa kufikia elfu ishirini (20,000/-). 

Wanawake wengi mkoani hapa wamekuwa wakifurika katika ofisi hizo ili pamoja na kutaka kujua utaratibu wa maonesho hayo pia washoneshe vazi hilo. 

Wanawake waliohojiwa na Mwandishi wa Habari hizi wamesema wamefurahishwa kwa kuandaliwa maonesho hayo ambayo wameyaita kuwa ni ya kihistoria hapa nchini kwani vazi la Hijab machoni mwa watu linaonekana kuwa ni vazi ambalo limepitwa na wakati. 

"Vazi la Hijab ni la lazima kwa mwanamke kwani ni amri ya Mwenyezi Mungu hivyo anasema kuwa vazi hilo limepitwa na wakati basi yeye mwenye kusema maneno hayo ndiye aliyepitwa na wakati", wamesema wanawake hao. 

Maonesho ya Songea yanafanyika huku kukiwa na wimbi la maonesho yanayoshusha hadhi ya mwanamke nchini kote na hasa katika jiji la Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa maonesho hayo ya Songea ni changamoto kwa vikundi na jumuiya za wanawake zenye kupigania hadhi ya mwanamke. 

Katika maonesho hayo pia kutakuwa na kongamano ambalo litajadili haki za mwanamke wa Kiislamu na miradi mbalimbali ya wanawake itazinduliwa. 

Ili kufanikisha maonesho hayo, wanawake wa mkoa wa Ruvuma wameunda jumuiya yao ya wanawake wa Kiislamu na kuchagua viongozi watakaoongoza jumuiya hiyo. 

Waliochaguliwa kuongoza jumuiya hiyo ni kama ifuatavyo:- 

Bi Hidaya Haji, Mwenyekiti, Bi. Mwanaidi Saidi, Makamu Mwenyekiti, Bi Zalia A. Gaula, Katibu, Bi Sophia Mdoka, Katibu Msaidizi na Mwajuma Tafai, Mweka Hazina. 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Maoni yetu: Prof. Juma Kapuya, vipi Muislamu usijue agenda za Waislamu? 

Hatimaye Mzee Katambo, Chata waachiwa
Na Mwandishi wetu

Polisi Newala wajenga Msikiti 

Sheikh Bafadhil aitaka Bakwata iwe mtetezi wa Waislamu
Na mwandishi wetu

Makala: Uinjilisti wa Mbuni haufai
Na Rajabu Mbambwa, Kigoma

Mussa Katambo: Mzee aliyewekwa rumande kwa kuandaa mihadhara

Ukweli usiachwe 

Makala: Elimu ya ngono yapenyezwa tena Zanzibar 
Na Saidi Mzee 

Arusha wasema: Hongera Mhe. KK kwa kuwa mfano mwema 
Na Hussein M.,  Arusha 

Wanawake Songea kuandaa maonesho 
Na. Jumah Mbwana, Songea 

Kesi ya mgogoro wa Ardhi
Na. Mustafa Adam 

AN-NUUR marufuku gerezani? 
Na Mwandishi Wetu 

Waislamu Karagwe wadai kusalishwa na imamu asiyejua kutawadha 
Na. Abu Abdallah 

Ofisi mpya za Rabita 
Na Mwandishi Wetu

Barua za wasomaji

Habari za Madrasa

Masomo

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita