AN-NUUR
Na.157 Rabi' Awal 1419, Julai 10 - 16, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Makala
 

Uinjilisti wa Mbuni haufai 

Na Rajabu Mbambwa, Kigoma 

Nimesoma makala yenye lugha nzuri ya Mwinjilisti Kamara Kasupa katika AN-NUUR toleo Na. 152 kwa anuani ya "POLENI NDUGU ZANGU WAISLAMU, IBILISI HANA RAFIKI". 

Kwa mtazamo wangu, nimekuona Mwinjilisti Kusupa kama mbuni ambaye hujikinga na madhara mwili wake (Taifa) kwa kuficha kichwa chake ndani ya mchanga na huku akiamini hiyo ni njia itakayoleta amani. 

Kwakuwa ulikuwa nahaki ya kutoa maoni yako kuhusu madai ya haki za Waislamu nami ningependa kutoa mawazo yangu kuhusu makala yako. Kwanza nitaanza na "UKOLONI". 

Katika makala yako umetoa ufafanuzi kuonyesha ukoloni uko namna mbili. 

Mosi, Ukoloni wa Mwingereza na wenzake na B. Ukoloni wa Bwana Yesu "Apostolos". 

Ukautakasa ukoloni wa Bwana Yesu na ukaunga mkono wapigania uhuru wa bara la Afrika dhidi ya matendo ya wakoloni wa Kiingereza. 

Kuhusu ukoloni wa Bwana Yesu "Apostolos", mimi sitatia neno kwakuwa ni jambo nisilolijua vema. 

Ama kuhusu ukoloni wa Waingereza nina ungana na wewe kukiri juu ya dhulma iliyokuwapo katika utawala huo. 

Ama kwa upande wangu sehemu kubwa ya dhulma hiyo iliwahusu sana Waislamu na hasa katika sekta ya elimu na kodi kubwa walizotozwa ambazo kwa ubaguzi wa Waingereza na kwa kujua fika lengo la makanisa la kuandaa "wacha-Mungu" watakaorithi hatamu za uongozi wakabeba dhima na kugawa sehemu ya kutosha ya kodi hiyo kuendesha makanisa na mashule yake. (Rejea Tahariri ya gazeti la AN-NUUR toleo Na.152) Padri Sivalon anatuambia ilifika mahala huwezi kuona mpaka wa kanisa na serikali. 

Kushamiri kwa ubaguzi wa kidini katika ukoloni wa Waingereza huku Wakristo wakipewa elimu kwa kodi za wananchi na Waislamu wakinyimwa kwa hoja ya kupinga ubatizo,hali hiyo iligawa nchi kwa tabaka la wanaosoma (Wakristo) na tabaka la wasiosoma (Waislamu) na huo ulikuwa mzizi mkubwa wa fitina. 

Kwa kuzingatia hali hii, Waislamu kama wananchi walikutana katika madrasa zao na humo wakabuni fikra ya harakati za kudai uhuru. 

Hili lilipobainika kwa Wakoloni na viongozi wa Kikristo ilipitishwa sera makanisani kuwaasa Wakristo wasijihusishe na harakati za uhuru. 

Zilipochipuka harakati na kuleta sura ya mafanikio, Waislamu waliwashirikisha Wakristo, Wapagani na wengine bila kujali udini ukabila, jinsia na bila kujali rasilimali nyingi walizotoa na ubaguzi wanaotendewa. Na ziliponoga harakati Wakristo walipewa hata urais. Hapa zingatia Waislamu ndio waliokuwa wengi na wenye nguvu katika mabaraza ya maamuzi na vyama vya siasa. 

Kwa mantiki hii swali lako "kwanini mnadai haki za Waislamu tu hamdai za wengine" ambalo liliambatana na hitimisho la ubaguzi, ni kutoelewa sera za kudai haki katika Uislamu. 

Waislamu wanapopata haki matunda huwa kwa wote. Nikupe yakini kwamba, endapo nguvu za uwiano ndani ya taasisi za maamuzi ya dola zingekuwa sawa kati ya Waislamu na Wakristo au za Waislamu zaidi, pasingevunjwa Tanganyika Federation of Labour, E.A.M.W.S. wala vyama vya ushirika vya wakulima, kwakuwa azma ya uhuru kwa Waislamu haikuambatana na ajenda za siri sawa na kanisa ambalo lilimuandaa Mwalimu Nyerere kushika uongozi kwa madhumuni ya kupata kile walichokiita "Good chance" na sio maslahi ya wote. 

Nilichotaka welewe kwanza ni uzalendo wa Waislamu katika utawala wa kubaguliwa kidini (wa Wakoloni), na pili ukumbuke mpaka Tanganyika inapata uhuru tayari kulikuwa na matabaka mawii ya Wakristo waliopewa elimu na Waislamu walionyimwa elimu. 
  

Ubaguzi ndani ya nchi huru 

Ubaguzi wa kidini ulishamiri enzi za mkoloni Wakristo wakibebwa nadola Waislamu wakitengwa. Hili lilikuwa tatizo zito lenya muelekeo wa kilele cha matokeo ya ndugu zetu Wahutu na Watusi. 

Katikavikao vya awali vya serikali huru Waislamu kama sehemukubwa ya jamii waliitanabaisha serikali juu ya madhara ya tatizo hili.Hatimae uzito wake ulionekana na serikali ikachukua ahadi ya kutoa kipaumbele cha elimu kwa Waislamu ili kuleta uwiano utakaoleta demokrasia katika maamuzi ndani yavikao vya kiserikali na kisiasa. 

Mwalimu Nyerere kama Rais, alikuwa na dhima ya kutekelezwa makubaliano mpaka anaondoka madarakani hana ushahidi wowote wa kiutendaji wala wa mabadiliko katika jamii yanayothibitisha kutekelezwa kwa azimio hilo. 

Sera iliendelea ileile (ya Wakoloni) nafasi na wizara nyeti (za elimu n.k.) kwa Wakristo na katika mashule darasa lenye Waislamu (40) Wakristo (10) washindao mtihani ni Wakristo (7) Waislamu (2). 

Waislamu wanao ushahidi mwingi tu wa viongozi na watendaji serikalini Wakristo waliosoma na kujinyakulia shahada za juu kwa kuchotewa nafasi za Waialsmu. Haya ni maelezo machache ya marudio, na hakika katika matoleo ya nyuma ya gazeti la AN-NUUR na majarida ya BARAZA Kuu umesoma uchambuzi wa ushahidi huu. 

Mwinjilisti umetoa kigezo cha wafanyakazi na wakulimakama hoja kwetu kuwa nao waliporwa haki zao sasa vipi na wao? Tunasema wafanyakazi na wakulima wao pia wana dini. Kwa wale ambao dini yao imehodhi haki za wengine wao hawakupoteza ila sehemu ndogo na huko kupoteza kwao ilikuwa ni kipindi cha mpito kwani sasa wanafaidi matunda makubwa yaliyopatikana katika jamii yao. Na wale wa tabaka la kugandamizwa ndio hao tunao dai hakii kwa ujumla wetu bila kujali huyu mfanyakazi, mkulima, Sheikh kwakuwa tatizo mama lililotuathiri ni udini. Aidha umehoji Nyerere kuwafukuza Kasela Bantu (Mkatoliki) Kasanga Tumbo (Mkatoliki) na wengine kama wao, kuwa ".sasa katika sakata la aina hii udini uko wapi?" Unachotakiwa kuelewa Mwalimu kama wakala wa kanisa aliahidi kulipa kanisa Tanzania "beter chance". Hilo ndilo lengo. Pamoja nae alikuwa wa timu iliyoitwa "..watu wanaofaa.." 

Katika midani ambayo ilitandikwa busati la siasa kikwazo kilikuwa ni "adui". Na "adui" (kwa mujibu wa maandiko yenu) alikua ni Uislamu. Lakini pia katika midani hiyo mwalimu alikabiliwa na hatari ya Wakristo wasomi wasiofahamu lengo. Wao aidha kwa kujali maslahi ya wote walikuwa na mtazamo zaidi katika lile "koti" siasa. Mwalimu kama kamanda kamwe hawezi kufanya kazi na watu kama hawajapokuwa ni Wakatoliki wenzake. 

Hutaweza kuona tatizo la udini kwa mizani ya kufukuzwa Wakristo kwa sababu wao tatizo lao ni watu wasiofaa katika kufikia lengo na sio dini zao. 

Haiyumkini Mkatoliki aliewajibika ipasavyo katika kufikia lengo awe adai kwa mtawala anaekusudia kuipa nchi muelekeo wa Kikatoliki. Kwa kuwa akina Kasela Bantu hawana ushahidi wa kubaguliwa kidini lakini wanao ushahidi wa kufukuzwa kisiasa lazima walalamike kama wanasiasa. 

Katika sura hii tuliyoionyesha hutakuta tabaka lingine lililoporwa haki kwa mtazamo wa imani isipokuwa Waislamu tu. 
  

Kuwekeza katika elimu 

Muinjilisti Kasupa ulipogusia nukta ya Waislamu kubaki nyuma kielimu hukuona mwanyawa serikali kulaumiwa. Ukasema "….wala watu wasingengoja serikali ndio iwajengee mashule na kuyagharimia bali wangejenga shule sawa na makumbi…." Aidha ukaonyesha umuhimu wa watu kuwekeza katika elimu kama njia pekee ya kujiendeleza. Kwanza tunauliza katika mfumo wa utawala uliokuwepo kwa nini watu wasingetegemea serikali kuwajengea mashule? Kodi walizotozwa zilikuwa za nini? Serikali hakuwatoza wananchi kodi ikawaahidi mashule na elimu sawa kwa wote? 

Ama suala la kuwekeza katika elimu unatonesha donda letu. Mara baadaya Waislamu kubaini Mwalimu Nyerere hayuko tayari kutekeleza azimio la kupewa haki za kielimu Waislamu walizoporwa huko nyuma na kujuafika kuwa anaendeleza sera ile ile ya ubaguzi dhidi yao, walitafuta ufumbuzi wa amani. 

Kwa nia ile ile ya kuitakia nchi salama na umoja wa kitaifa waliamua kujinyima na kuwekeza katika elimu kupitia E.A.M.W.S. Wakajenga shule mikoa mingi toka za msingi, sekondari na kumiliki ardhi kwa aajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu mjini Dar es Salaam. Wale wale ambao padri Sivalon anatoa ushahidi kuwa waliandaliwa na wale waliosema "tatizo ni Uislamu" wakavamia na kuvuja EAMWS chombo ambacho Waislamu waliwekeza katika elimu. Zaidi ya hapo wakawaundia BAKWATA kuwashikisha hakuna kufurukuta wala maendeleo. Hali hii iliwawezesha kuendeleza sera ya tabaka la Wakristo wasomao na tabaka la Waislamu wanaoendelea kubanwa kielimu na kiutawala. 

Hili Muinjilist Kasupa anaweza kuliona kwa maamuzi yahivi karibuni ya serikali kuunda bodi "Parole" ya wajumbe wengi Wakristo wakiwemo mababa Askofu watano. Tukizama katika ukweli Mwinjilisti Kusupa bodi hii ya serikali yenye viongozi wa Kuu wa kanisa inge wajibika kwa nani. Ni kweli kwamba ingewajibika kwa wananchi wote wakiwemo Waislamu? Mimi narudisha pole kwako kwa kufumbia macho ukweli. Mantiki ipi iliyotumika kwa watawala mpaka nchi ikafaulu kupata maafisa tawala wa mikoa Muisilamu (1) Wakristo (19). Au teknolojia ipi iliyotumika mpaka tume ya jiji ikaibuka na Muslamu(0) Wakristo (9). 

Hakuna tatizo la wapagani hapa nchini,sura iliyowazi hata kwa baadhiya mapadri ni tatizo la Ukristo dhidi ya Uislamu kupitia utawala. 

Kama ulivyotutahadharisha kuwa ibilisi huingia ndani ya mwili wa mtu wa kumdanganya kontena lake, Mwinjilisti Kasupa jiangalie isijekuwa katika suala hili umekuwa kontena. 

Maana sioni vipi kwa mtu ambae hajawa kontena la Ibilisi awaone Waislmau ni tatizo wanapodai kutendewa dhulma na serikali. Katika makala yako ulitupa swali kupitia kwa mwenzetu ukahoji "….Mohamedi Saidi anataka lifanyike nini hasa ili mambo yawe mazuri…."Tunasema popote pale duniani njia bora na ya hakika ya kujua na kulipatia ufumbuzi tatizo ni mazungumzo nauchunguzi wa kina. Waislamu hapa nchini mara kadhaa wamejitahidi kuwasiliana na serikali kuitaka iunde tume kupokea ushahidi wa madai yao, serikali ina kwepa. 

Katika kumbukumbu zangu ujumbe na simu wa Waislamu uliwasilishwa kwa Waziri Mkuu (wakati huo) Mhe. John S. Malecela mpaka leo hapana jibu. Hili ni la muhimu kufanywa "ili mambo yawe mazuri". 

Kanisa katoliki na siasa Tanzania Bara. 

Humo amekusanya nyaraka mbalimbali za maazimio, mikakati na stratejia za muda mfupi na muda mrefu za kuwadhoofisha, kuwaengua na kuwamaliza Waislamu zinazowahusisha Wakoloni na kanisa. 

Aidha, Padri amehitimisha humo kwa kuonyesha kufaulu kwa kiasi kikubwa mikakati hiyo katika utawala wa Mwalimu. Nyerere na sasa mambo yaajiendesha wenyewe. 

Kwa hiyo kwakuwa tatizo kubwa na la hatari linaliikabili nchi ni ubaguzi wa kidini, Waislamu wana haki kabisa ya kushughulikia kwanza hilo maana tusipoziba ufa tutajenga ukuta. 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Maoni yetu: Prof. Juma Kapuya, vipi Muislamu usijue agenda za Waislamu? 

Hatimaye Mzee Katambo, Chata waachiwa
Na Mwandishi wetu

Polisi Newala wajenga Msikiti 

Sheikh Bafadhil aitaka Bakwata iwe mtetezi wa Waislamu
Na mwandishi wetu

Makala: Uinjilisti wa Mbuni haufai
Na Rajabu Mbambwa, Kigoma

Mussa Katambo: Mzee aliyewekwa rumande kwa kuandaa mihadhara

Ukweli usiachwe 

Makala: Elimu ya ngono yapenyezwa tena Zanzibar 
Na Saidi Mzee 

Arusha wasema: Hongera Mhe. KK kwa kuwa mfano mwema 
Na Hussein M.,  Arusha 

Wanawake Songea kuandaa maonesho 
Na. Jumah Mbwana, Songea 

Kesi ya mgogoro wa Ardhi
Na. Mustafa Adam 

AN-NUUR marufuku gerezani? 
Na Mwandishi Wetu 

Waislamu Karagwe wadai kusalishwa na imamu asiyejua kutawadha 
Na. Abu Abdallah 

Ofisi mpya za Rabita 
Na Mwandishi Wetu

Barua za wasomaji

Habari za Madrasa

Masomo

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita