|
|
| Polisi Newala
wajenga Msikiti
WAKATI polisi na askari Magereza jijini Dar es Salaam wakiua na kuwatesa Waislamu kana kwamba wao hawana dini au hawamtambui Mungu, hali ni tofauti katika baadhi ya mikoa na wilaya. Habari ambazo AN-NUUR imezipata kutoka Newala zimeeleza kwamba, askari polisi wakishirikiana na askari Magereza wamejenga Msikiti karibu na ofisi na makazi yao ili waweze kufanya ibada kikamilifu. Msikiti huo ambao wameujenga katika eneo la Nangwala upo katika hatua za mwisho tayari kwa kuswaliwa. Askari hao imeelezwa kwamba wamechukua hatua hiyo baada ya kuwa miskiti mikuu miwili ya mjini Newala kuwa mbali na maeneo yao na hivyo kuwa taabu kwao kuwahi kuswali swala za jamaa. Lakufurahisha na kutia moyo ni kuwa, askari hao wamejenga msikiti huo kwa nguvu zao wenyewe za hali na mali. Habari za hivi karibuni zimeeleza kwamba msikiti huo hivi sasa unahitaji milango, madirisha na mazulia tayari kwa kuanza kuswaliwa. Waislamu wameombwa kuunga mkono juhudi za askari hao kwa kusaidia vifaa hivyo. Msaada wowote waweza kupitishiwa kwa uongozi wa Masjid Hidaya wa mjini Newala. |
Maoni yetu: Prof. Juma Kapuya, vipi Muislamu usijue agenda za Waislamu? Hatimaye Mzee Katambo, Chata waachiwa
Sheikh Bafadhil aitaka Bakwata iwe
mtetezi wa Waislamu
Makala: Uinjilisti wa Mbuni haufai
Mussa Katambo: Mzee aliyewekwa rumande kwa kuandaa mihadhara Makala: Elimu ya ngono yapenyezwa
tena Zanzibar
Arusha wasema: Hongera Mhe. KK kwa
kuwa mfano mwema
Wanawake Songea kuandaa maonesho
Kesi ya mgogoro wa Ardhi
AN-NUUR marufuku
gerezani?
Waislamu Karagwe wadai kusalishwa
na imamu asiyejua kutawadha
Ofisi mpya za Rabita
|