|
|
|
Hongera Mhe. KK kwa kuwa mfano mwema Na Hussein M. Arusha Pongezi kwa Mhe. Kitwana Kondo zimetolewa na wananchi mbalimbali wa mkoani Arusha kufuatia nasaha zake alizozitoa kwa serikali katika kikao cha Bunge la Bajeti ya Serikali kinachoendelea sasa hivi mjini Dodoma. Mhe. Mbunge wa Kigamboni aliituhumu serikali katika utendaji wake pale inapotoa upendeleo miongoni mwa wananchi. Akitoa mfano wa upendeleo, Mhe. Kondo alisema kwamba, "Mhe. Waziri Mkuu aliposhughulikia tatizo la wananchi wa Arumeru waliokataa kulipa kodi, alikwenda na lugha ya kuwabembeleza akitoa ahadi kwamba. Serikali haitakuwa tayari kupambana nao; japo walifanya ghasia; kuchoma nyumba ya Mwenyekiti wao na kuharibu mali. Lakini kwa suala la Mwembechai mhe. Kondo anasema Waziri Mkuu alitangaza vita dhidi ya Waislamu na kuahidi kwamba hapatakuwa na huruma bali wataadhibiwa vikali". Katika kutoa pongezi zake kwa mhe. Kondo, mzee Joachim Mollel alisema kwamba, "Mhe. Kitwana Kondo ametoa changamoto ya dhati kwa viongozi wengineo wanaoshindwa kusema kweli japokuwa wanaiona kwa kuhofia mambo mbalimbali kama, kunyang’anywa madaraka; kuambiwa wana udini, ukabila, n.k. Linalotakiwa kwa viongozi wetu ni kuongea kweli kwa kutumia hoja zenye nguvu na kwa lengo la kutengeneza na kuelimisha na wala si kutumia jazba, uzuishi, hila aya uchochezi",alingeza mzee Mollel. Naye Mzee Hashim Issa alisema kuwa kiongozi maana yake ni kufanyaUadilifu. Na Uadilifu unamaana pana sana ikiwa ni pamoja na kutoa hukumu bila upendeleo; kutoa haki sawa bila kuongozwa na hisia zozote za kubagua". Kijana Mustafa Omari alisema kuwa, "Wabunge na viongozi wetu wasisahau kuwa walikula kiapo cha kulitumikia taifa letu kwa uaminifu. Kutumikia kwa uaminifu ni pamoja na kutobagua au kutopendelea baadhi ya wananchi. Hisia zozote katika kuhukumu au utendaji zinazoelekezwa dhidi ya Ukristo ama dhidi ya Uislamu penginehata dhidi ya imani binafsi ya mtendaji au hakimu ni kinyume kabisa nauadilifu au maadili ya uongozi kwa sababu zinalenga kuwafurahisha wakuu wachache ama tabaka fulani katika jamii. Hivyo waliopewa dhamana wasisahau kiapo walichokula kwa kuwa wataulizwa na Mwenyezi Mungu kama walitekeleza waliyowaahidi wananchi". Alikumbusha Musatafa. "Ni vema Rais wetu akawa makini na wale viongozi wanaonekana kuhatarisha amani na usalama wa nchi yetu katika utendaji wao", alimalizia Mustafa. Naye Muhidin Mwalimu alisema, "Ni wengi wanaohitaji sana madaraka kwa kuwa mamlaka yake ni matamu. Lakini wanapopata wanasahau kaisa sharti lake kuu ambalo ni "Uadilifu’. Hivyo, viongozi wetu wasisahau kuwa huo ni mtihani waliopewa na Mwenyezi Mungu. Na alipowateua amewaacha wengine wenye uwezo pengine zaidi yao." Akizungumzia suala hili Mzee Abasi Haji wa Ngara Mtoni alihoji, "Ni
vipi katika zama hizi za uwazi na ukweli vyombo vingi vya habari havikutoa
kipaumbele katika hoja hii ya Mhe. Kondo kwa kuwa inalenga kulitengeneza
taifa letu? "Hii inamaana moja tu, kuwa vyombo vyetu vingi vya habari vinatilia
umuhimu mkubwa zaidi matakwa ya watu binafsi wachache na umuhimu kidogo
kwa baadhi ya wananchi au maslahi ya aifa letu", alimaliza Mzee Abas.
|
TAHARIRI Maoni yetu: Prof. Juma Kapuya, vipi Muislamu usijue agenda za Waislamu? Hatimaye Mzee Katambo, Chata waachiwa
Sheikh Bafadhil aitaka Bakwata iwe
mtetezi wa Waislamu
Makala: Uinjilisti wa Mbuni haufai
Mussa Katambo: Mzee aliyewekwa rumande kwa kuandaa mihadhara Makala: Elimu ya ngono yapenyezwa
tena Zanzibar
Arusha wasema: Hongera Mhe. KK kwa
kuwa mfano mwema
Wanawake Songea kuandaa maonesho
Kesi ya mgogoro wa Ardhi
AN-NUUR marufuku
gerezani?
Waislamu Karagwe wadai kusalishwa
na imamu asiyejua kutawadha
Ofisi mpya za Rabita
|